11 February 2011

Lowassa ametuma salamu-Lipumba

Na Grace Michael

SIKU moja baada Mbunge wa Jimbo la Monduli, Bw. Edward Lowassa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, imeelezwa kuwa
hiyo ni salamu aliyoitoa kuonesha nguvu aliyonayo ndani ya Chama cha Mapinduzi na ndani ya bunge.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, alisema kuwa pamoja na uchaguzi huo kufanywa na wabunge wenyewe lakini hiyo ndio salamu ya nguvu kubwa aliyonayo.

Pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuacha kumpa nafasi yoyote katika awamu hii lakini amejaribu kuonesha nguvu aliyonayo ndani ya chama hicho na kwa wabunge wenzake...hivyo hizi salamu tunatakiwa kuzipokea na kujipanga, alisema Prof. Lipumba.

Kutokana na hatua hiyo aliwataka wananchi kujipanga kwa kukabiliana na hilo katika chaguzi zijazo kwa kuwa CCM kimepoteza dira na mwelekeo na hakina uwezo wa kusimamia maslahi ya taifa.

Watanzania tunatakiwa tujipange kupata uongozi ambao watakuwa na uwezo wa kusimamia hata rasilimali za nchi hii, usioegemea upande mmoja, unaojali maslahi ya wananchi wake, ambao hautoki ndani ya CCM, alisema Prof. Lipumba.

Hata hivyo wananchi mbalimbali waliotoa maoni yao juu ya uchaguzi huo kwenye tovuti ya gazeti hili, wametofautiana kimsimamo ambapo wapo wanaopongeza kuchaguliwa kwa Bw. Lowassa na wapo wanaooponda.

Mmoja wa wasomaji wa Majira ambaye ametoa maoni yake amewataka watanzania kujadili hoja na si kupaka matope watu wengine, kamati ziachwe kama zilivyopangwa na uongozi uliopatikana na kinachotakiwa ni kusubiri matunda ya kazi yao.

Tunatakiwa kujadili hoja tena za msingi lakini kinachotakiwa kuangaliwa ni uwezo na umakini wa viongozi na sio kujadili upuuzi...tuwaachie wanakamati wenyewe waendelee na kamati zao, tusiwe na haraka ya kutoa yanayokuja mbele na huku hatujui hapa tulipo,รข€ alisema msomaji huyo.

Kamati zingine zilizotolewa maoni ni pamoja na kamati ya Hesabu za Serikali za Mtaa inayoongozwa na Augustino Mrema, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma  Bw. Kabwe Zitto na Kamati ya Hesabu za Serikali inayoongozwa na Bw. John Cheyo ambao wamedaiwa kuwa hawatasaidia chochote kwa kuwa ni vibaraka wa Rais Jakaya Kikwete.

13 comments:

  1. SWALA SI LOWASSA KASHINDAJE, ILA HII NI UTHIBITISHO WA HALI YA UNAFIKI WA WABUNGE WA CCM. NI KWA UNAFIKI HUU HUU TAIFA HALIJAPATA KUSIMAMA KWA MIGUU YAKE MIWILI TANGU LIZALIWE. NJAA, WOGA NA UNAFIKI NDANI YA CCM VIMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUHARIBU MIUNDOMBINU YA KIMAENDELEO YA TAIFA. NDIYO MAANA UNAONA WATU KAMA ROSTAM WAPO NEC, WATU KAMA MRAMBA WANAPIGIWA KAMPENI, WATU KAMA SITTA WANAPIGWA VITA, N.K. KWA KUTUMIA UKIMYA WA WATANZANIA, NA KWA MABAVU WALIYOZOEA KUTUMIA, HAITAKUWA AJABU KWA CCM KUMSIMAMISHA LOWASSA KUGOMBEA URAISI 2015! MAANA NDIYO MTAJI PEKEE WALIO NAO, NA HIYO NDIYO NJIA YA KUMREJESHA. TUKAE MACHO!

    ReplyDelete
  2. KWELI KABISA HAPO JUU. NAKUUNGA MKONO. WATANZANIA WANANUKA KWA UNAFIKI, WOGA, KUTISHANA, NA KUJIDANGANYA WENYEWE (SELF-DECEPTION) HUKU TUKIPENDA SANA KUONEA WANYONGE. DHAMBI HIZI TUSIPOACHA, TUTAHUKUMIWA SIKU MOJA.

    ReplyDelete
  3. YA NGOSWE MWACHIE NGOSWE MWENYEWE USEMI HUU SASA UNASTAHILI KUPINGWA...HAWA AKINA NGOSWE WASIACHIWE WAFANYE WANAVYOTAKA ,WATATUMALIZA

    ReplyDelete
  4. NAsikia na Peter Serukamba mwandani wa mafisadi kapewa kamati ya miundo mbinu. Tim imejipanga tusubiri mchezo sasa. Hamna kulia, na kwa nn tulie wakati tumechagua kwa kishindo??? Unduminakuwili oyeee ccm.

    ReplyDelete
  5. nyie wasenge hakuna mnachosema kwa vile nyie ndio wanafiki wenyewe.mbona nyie na wazinzi wakubwa hamna hoja huo ni ujinga kabisa

    ReplyDelete
  6. ndugu yangu hapo juu, tafadhali tumia lugha nzuri, usipopewa nafasi kama hii unalalama, hali hii ya mipasho imtua bungeni hasa kwa wabunge wa ccm huku mitambo yao ya mawasiliano ikwa hewani,na mhe spika wa bunge letu tukufu naye ameonekana kushabikia mipasho...yatamrudi..tuweni makini.. hao waheshimiwa wabunge wengine watakapoanza hasira zenu zitapanda na kuanza kutumia vifungu vya kuwahadhibu..lakini kwa ccm na cuf sasa ni rhuksa...mhe mama makinda kazi unayo lakini ni ya kujitakia

    ReplyDelete
  7. CCM wanatupeleka wapi jamani. Kwa nini kila mtu anayekitetea CCM huanza kwa matusi? Ina maana wao hawajui kuwa matusi ni kosa la jinai kisheria? au kwa vile wao wanatawala ndio na matusi ni rukhusa kwao?

    Kuna mambo mengi ya muhimu ya kujadili tunapopewa taarifa na hawa waandishi. Acheni kila mtu achangie kwa uhuri ili tujenge nchi. Unadhani nchi inajengwa kwa matofali? Nenda Somalia ukaone majengo yanavyokosa maana baada ya watu kuuana.

    Tunapomjadili mwenyekiti wa tume fulani kwenye bunge watu wanatoa mawazo yao ili yamkini yafanyiwe kazi. Lisemwalo lipo, kama halipo laja.

    Siku mambo yakiharibika hakuna atakayekuwa salama.
    Wacha tuseme:
    Hizi kamati zimeundwa kwa manufaa ya serikali na CCM, sio wananchi.

    Na kanuni za bunge zimerekebishwa kwa manufaa ya seikali ya CCM na CUF.

    ReplyDelete
  8. Nawashangaa sana wantanzania kukumbatia hawa mafisadi wakati nchi zingine kama Misri na Tunisia n.k. wanapambana nao sisi tunakubali kikundi cha watu wachache waaamue kujipangia matumizi ya ovyo katika bajeti ya nchi. Serikali ya CCM haiko tayari kupunguza matumizi ya anasa wakati mahitaji muhimu kama umeme na maji bado hayawafikii wananchi wote.Awali ya yote inatakiwa wananchi waelimishwe kuhusu umuhimu wa kuchagua serikalli itakayo wasikiliza si kwa kuwapa kanga na t-shirti kabla ya uchaguzi ila kwa kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.

    ReplyDelete
  9. BRAVO MH LOWASSA SONGA MBELE TUKO PAMOJA NAWE...TUTAFIKA

    ReplyDelete
  10. IM Trying to image,That day when stupid Tanzanian will wake up!The day things will turn
    like what the Warrior of Egypt and Tunisian did,The day Loverboy Kikwete,Corrupt and celebrate Lowassa and all Fuking CCM Cabinet will be arrested,guess what gona happen!!,I cant wait,I got my fire wood ready to burn there fuking assy alive,Who know!let they carry on,but ONE DAY

    ReplyDelete
  11. Lipumba una yako bungeni yanakushinda unamkurupukia Lowassa. Lowassa alikuwa Waziri Mkuu mfuatiliaji wa kila jambo na mtendaji mzuri,hilo la Dowans mbona ndio linatesa sekta ya umeme baada ya kuvunja mkataba? Uswahili umezidi kwa Watanzania. Waamerika walifanya makosa kuvamia Iraq na Afghanistan lakini leo wako pamoja kutatua matatizo yanayowakabili kutokana na kadhia hiyo,hata baada ya kuingia Obama bado hali ni ngumu lakini kwa sababu liliishatokea wanaangalia mbele,nyie kila siku Dowans,Dowans,Dowans!!!!! hivi Lowassa alipokuwa kiongozi hana mazuri aliyoyafanya? mbona bado mnaweweseka na Dowans? mnalia shida ya umeme na mtambo mnayo ndani ya nchi yenu mmeizima.Mawazo dhaifu yaliyotawaliwa na wanasiasa huzaa fikra dhaifu

    ReplyDelete
  12. we said acha kuzungumzia mambo usiyo yajua mana yatakushinda!

    ReplyDelete
  13. Ni vizuri tukiendelea kujadili kile ambacho tunaona kina makosa na au mapungufu, hatuhitaji kujadili mada au mambo ambayo yanaenda vizuri kwasababu yanaenda vizuri, hivyo basi fanya tisini na tisa mazuri malizia moja tu baya litafuta yale yote mazuri uliyoyafanya, tatizo letu ni uelewa finyu katika mambo ya msingi na ninaamini kuwa BOMU aliloliunda LOWASA (shule za Kata zisizo na Walimu)ndilo litakalo igharimu CCM, na itaondolewa madarakani, Tanzania yetu ITAKOMBOLEWA KUTOKA MIKONONI MWA MAFISADI. Nchi yetu inaongozwa na Lowasa na Rostam na Kikwete hana kauli mbele yao, tunaendesha Nchi yetu Kiswahiba,kirafiki na zaidi sana kinafiki. na Nyerere alisema ukiwekwa madarakani kwa kutumia fedha za watu fulani utafanya yale wanayotaka wale waliokuweka madarakani na diyo yanayotokea, kashfa kibao, nchi ina tatizo kubwa la UMEME Raisi wetu ANACHEKACHEKA tu! hayuko makini, haoni kama kuna shida hapo, haoni kama linawaumiza Nchi yake na wananchi wake. Sasa natambua kwanini Nyerere alisema kuwa Kikwete hajakomaa (1995) kumbe hakuwa na maana ya umri alikuwa na maana ya AKILI YAKE.

    ReplyDelete