Na Mohamed Hamad, Kiteto
WANAFUNZI 27 Sekondari ya Matui Manyara wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kuanguka.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9.45 jioni kwa kuhusishwa gari lenye namba za usajili T.890 AUR mali ya Bw. Ibrahimu Gwangu mkazi wa Kijiji cha Matui.
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, Bw. Parmena Sumary alisema gari hilo lilikodishwa na uongozi wa shule ya Sekondari Matui kwenda
Sekondari ya jirani ya Engusero kucheza mpira.
Amesema wakiwa karibu kufika kilometa kadhaa shuleni hapo gari hilo lilianguka kuokana na ubovu wa barabara baada ya kuelemewa na mzigo na kusababisha 27 kati yao kuumia na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya kiteto.
Miongoni mwa majeruhi hao, watatu wamevunjika au kuteguka, akiwamo Jerald John (17) ambaye amevunjika mkono, Salimu Mohamed (20) ambaye ametenguka mkono na Husna Dosa (19) ambaye
ameumia mbavu.
No comments:
Post a Comment