Na Suleiman Abeid, Shinyanga
KAULI ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini, Dkt. Hussein Mwinyi ya kugoma kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na tukio la
milipuko ya mabomu lilitokea katika Kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 511 KJ, Gongolamboto, Dar es Salaam imepokelewa kwa maoni tofauti na wakazi wa mji wa Shinyanga.
Baadhi ya wakazi hao wamelieleza Majira kushangazwa na kauli hiyo wakihoji waziri huyo anapata wapi jeuri hiyo wakati wanaomtaka ajiuzulu ndiyo hao hao waliomchagua kuwa mbunge na kupata nafasi hiyo ya uwaziri.
Walisema ushauri unaotolewa na Watanzania wengi wa kumtaka waziri mwenye dhamana na ulinzi nchini kujiuzulu kutokana na kashfa ya mlipuko wa mabomu hapa nchini haukulenga kumkomoa wala kumdhalilisha, bali ni kutaka kuonesha jinsi gani ameguswa na tukio hilo.
“Kwa kweli kama kweli maneno yaliyotangazwa kupitia vyombo vya habari vikinukuu kauli ya waziri kugoma kujiuzulu ni sahihi, basi ni wazi hakutumia busara katika kutoa tamko hilo, alipaswa kuelewa kuwa wanaomuomba ajiuzulu ndiyo hao hao waliomchagua kuwa mbunge.
"Anapaswa akumbuke kuwa ili kuweza kuupata uwaziri alionao hivi sasa kwanza alipita kwa wananchi huku akiwapigia magoti kuomba achaguliwe kuwatumikia, bahati nzuri ubunge kapata na rais kamuona anafaa kuwa waziri kamteua, lakini chanzo cha ni wapiga kura," alisema.
"Wapigakura waliomchangua ndiyo wanaomshauri kuwa katika kulinda heshima yake ni vyema akajiuzulu katika wadhifa wake kutokana na kadhia hiyo ya mabomu. Ni aibu, akumbuke tukio hilo sasa limetokea mara mbili akiwa waziri wa wizara husika, alipaswa kutafakari na kufikia uamuzi wa busara," alieleza mkazi mmoja wa mjini Shinyanga.
Naye mkazi wa mtaa wa Luhende kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga aliyejitambulisha kwa jina moja la Bw. Charles alisema umefika wakati hivi sasa kwa viongozi wakuu wa kitaifa kujenga utamaduni wa kuwajibika kila linapotokea tatizo ambalo siyo zuri katika wizara au idara zao wanazoziongoza.
"Hawa viongozi wetu wanapaswa kuelewa kuwa wanawekwa madarakani kwa mujibu wa katiba ya nchi, katiba inaeleza wazi kuwa wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho katika masuala muhimu yanayogusa mstakabali wa nchi, leo wanapogoma kujiuzulu wanakuwa
wanamtegemea nani kama siyo wananchi?" alihoji Bw. Charles.
Hatua ya wakazi hao kulaani kitendo cha Dkt. Mwinyi inatokana na uamuzi wake alioutangaza juzi kuwa hawezi kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na kadhia ya mlipuko wa mabomu uliotokea kwa mara ya pili huko Gongolamboto jijini Dar es Salaam baada ya ule uliotokea Aprili 29, 2009.
WAZIRI MWINYI KWELI NI WAZIRI MWENYE DHAMANA KTK JESHI AMBALO WATU WAKE WAMEFANYA UZEMBE AU NI AJALI KUKALIPUKA SASA IWEJE YEYE AWAJIBIKE? ILIPOTOKEA MLIPUKO MBAGALA 2009 KULIKUWA NA JOPO LA WAKAGUZI WATAALAMU WENYE UJUZI WA KAZI YAO WALIKAGUWA KAMBI ZOTE ZENYE SILAHA NA WALITOA RIPOTI ZAO KUWA ZIKO SALAMA, SASA HAO WALIOKAGUWA BILA UWAANGALIFU NDIO WAADHIBIWE NA KUWAJIBIKA SIO YEYE TENA UKIZINGATIA HANA UJUZI NA MABO YA KIJESHI YEYE NI DAKTARI!!HILI SI LA KISIASA NI LAUTENDAJI ZAIDI
ReplyDeleteWewe mtoa comment hapo juu nawe unajichanganya!! kama waziri Mwinyi hana ujuzi wa vifaa vya jeshi/mabomu na fani yake ni Udaktari, sasa huoni kuwa nayo pia inachangia kwake kukosa ufanisi wa wizara anayoongoza?? na zaidi yeye kama kiranja wa wizara husika ilopotokea ya Mbagala alitoa tamko nadhani baada ya kupata report ya wachunguzi na kujiridhisha kuwa halitatoe tena, na sasa limetokea akiwa bado kwenye wizara hiyohiyo kama kiranja!! Ndiyo maana kuonyesha uwajibikaji yeye inabidi AJIUZURU ili, kwanza kutunza heshima yake, pili kuonyesha uwajibikaji!! tatu kupisha uchunguzi huru!! nne kupisha wenye fani/ujuzi wa vifaa/mabomu kuongoza wizara.!! na ikibidi yeye asubili kule ambako atafiti kwa taaluma yake....! IMEFIKA WAKATI UJEURI WA VIONGOZI UTAKOMESHWA KWA MAANDAMANO, MAANA WANANCHI TUMECHOKA!! Wanajivika ngozi ya kondoo wakiwa wanaomba kura kwa wananchi, lakini ni masimba rohoni wakipata uongozi!! Wanang'ang'ania nini huku watu wanapoteza maisha, viungo, mali kwa uzembe wao????????????
ReplyDeleteNDUGU ZANGU SWALA LA MABOMU NI ZITO, HUU WAWEZA KUWA MPANGO.
ReplyDeleteMWINYI SI KING`ANGANIZI ILA KUNA VIGOGO NYUMA YAKE WANAOMLINDA.MSIMLAUMU YEYE MLAUMUNI ALIYEMPA MADARAKA HAYO YA SILAHA BADALA YA YDAKTARI.
ReplyDeleteKWA TAARIFA YENU ANAANDALIWA KUMPOKEA KIJITI JAMAA KULE KWENYE VISIWA VYA KARAFUDU
HALAFU AJE HUKU BARA KAMA BABAAKE ALIVOFANYA.. MAMBO YA KINA GADDAFI FAMILIA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA.
ReplyDeleteawajibike, yeye, mkuu wa majeshi, na ikibidi mama makinda afuate
ReplyDeletendugu muhariri wa gazeti hili la majira nakushukuru kwa kazi yako nzuri sana mungu akujalie sana lkn mimi ushauri wangu kwako nadhani hujawa na watu wenye upeo mzuri wa kutoa comment si gazeti lako tu karibu yote jitahididi sana kuwafundisha watu wenu jinsi ya kuandika comment zao kwani nyingi haziendani na habari iliyo andikwa na kutolewa comment elimu kwa watu waliowengi bado siasa ni nyingi
ReplyDelete