28 February 2011

Familia ya Nyerere yawapongeza CHADEMA

Na Suleiman Abeid, Butiama

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana walitembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambako walipewa
matumaini kuwa wanaweza kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 na kuongoza nchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 ya uhuru.

Ubashiri huo umetolewa jana kijijini Butiama na mmoja wa watoto wa hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. Magige Kambarage alipokuwa akitoa shukrani zake kwa viongozi wa CHADEMA waliokuwa wamekwenda kijijini Butiama kuzuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kumjulia hali mjane wake, Mama Maria Nyerere.

Msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa uliwasili kijijini Butiama saa 6.00 mchana jana na kupokewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, Bw. Makongoro Nyerere ambaye pia ni mmoja wa watoto wa hayati baba wa taifa.

Akiukaribisha msafara huo uliojumuisha wabunge mbalimbali wa chama hicho, Bw. Makongoro aliupongeza ujumbe huo kwa kuona umuhimu wa kufika Butihama, na hasa nyumbani kwao, kuwajulia hali na kutembelea kaburi la marehemu baba yao, kwa kuwa siasa si uadui.

Baada ya kutembelea kaburi hilo na kuweka mashada ya maua, Bw. Kambarage aliwapongeza viongozi wa CHADEMA kwa uamuzi wao wa kuendesha maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima ili kuzungumzia mstakabali wa Taifa la Tanzania.

Kugombana ndani ya siasa ni ujinga tu ndiyo unaotusumbua, mimi nasema kitendo hiki cha maandamano mlichokifanya ni kitendo kizuri sana, pamoja na kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakupongezeni, alisema.

Hizi safari za kutembea kwa miguu na kushirikiana na wananchi ni kitu muhimu, eleweni kwamba mna dhamana kubwa hivi sasa mbele ya umma wa Tanzania, kwani ninyi ndiyo kambi kuu ya upinzani hapa nchini, fanyeni kazi msije mkapoteza dhamana mliyokabidhiwa na wananchi, umma umeishawakubali,รข€ alieleza Bw. Kambarage.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, watu wengi hawakujitokeza kupiga kura, lakini wapo zaidi ya milioni 20 wenye haki ya kupiga kura, ambapo aliwataka viongozi hao wa CHADEMA wafanye kazi kubwa ya kuwatafuta waliko ili ifikapo mwaka 2015 waweze kupiga kura.

Mimi nasema hawa ambao hawakupiga kura wapo wengi sana, watafuteni waliko, 2010 CCM tulipata kura milioni tano za urais, lakini naamini mkiwatafuta hawa waliopotea, katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 CHADEMA mtazoa zaidi ya kura milioni sita na CCM tutaambulia kura milioni nne, naamini hivyo, alieleza Bw. Kambarage.

Alisema moja ya kazi wa vyama vya upinzani nchini ni kuwainua watanzania katika mambo ambayo serikali iliyoko madarakani imeshindwa kuwatekelezea na kwamba hivi sasa Watanzania wameishakikubali chama cha CHADEMA na ndiyo maana wanakiunga mkono badala ya CCM," nakuombeeni Mungu aibariki kazi yenu, alisema.

Awali, mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alimweleza mama Maria Nyerere kuwa lengo la ziara yao hiyo ni kumjulia hali yeye na familia yake, kudhuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kuomba dua katika kaburi lake ikiwa ni katika kuenzi heshima aliyokuwa nayo katika Taifa la Tanzania.

Nachukua fursa hii kukushukuru kwa heshima kubwa uliyotupatia ya kukubali kuja kukujulia hali pamoja na kutembelea kaburi la hayati baba wa Taifa, tunasema hii ni heshima kubwa kwetu sisi CHADEMA wakati tukiwa katika mkoa wa Mara kuendesha maandamano ya amani na mikutano ya hadhara kuzungumzia mstakabali wa taifa letu,

Tunaomba utuombee kwa Mungu ili tuweze kufanya kazi zetu vizuri na ikibidi kutuunga mkono, basi utuunge katika lolote lile ambalo tutahitaji kuungwa mkono na wewe, lengo letu ni moja tu kuwatumikia Watanzania ili waweze na kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yetu, alieleza Bw. Mbowe.

Kwa upande wake mama Maria Nyerere aliwashukuru viongozi hao wa CHADEMA kwa uamuzi wa kumtembelea ili kumjulia hali ambapo aliwaombea kwa Mungu aweze kuwapa afya njema na waendelee kuwatumikia wananchi kwa haki bila ya upendeleo wowote.

Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo juzi, Bw. Mbowe alisema chama hicho hakina mpango wa kumchukulia hatua Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga, Bw. John Shibuda kwa vile kinaamini hakijawa na mgogoro naye.

Bw. Mbowe alilazimika kutoa ufafanuzi huo wa kuhusiana na Bw. Shibuda baada ya kutakiwa na wananchi aeleze nini hatma ya mbunge huyo ambaye amekuwa akionesha dalili za kupingana na maelekezo ya chama mara kwa mara.

Mwenyekiti huyo alijikuta akiulizwa swali hilo mara baada ya yeye kutoa ufafanuzi wa kitendo cha spika kubadili kanuni za bunge na kutaka kuilazimisha CHADEMA kuungana na vyama vingine kuunda kambi ya upinzani bungeni, wananchi hao walipiga kelele wakisema, na Shibuda, Shibudaaaa.

Kutokana na kelele hizo, Bw. Mbowe alilazimika kuwauliza wananchi hao iwapo walikuwa wakimtaka Bw. Shibuda aongee nao, nao walijibu kwamba wanachohitaji ni yeye kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya kutaka kupingana na viongozi wake ndani ya CHADEMA.

Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi kwamba Bw. Shibuda hana tatizo lolote ndani ya chama na kwama mambo yaliyokuwa yamejitokeza ni mambo madogo madogo ambayo hayawezi kusababisha mbunge huyo kufukuzwa ndani ya Chama.

Ndugu zangu napenda nikufahamisheni wazi kuwa tupo humu ndani ya vyama vya siasa kwa sura na tabia tofauti, inaweza kutokea Bw. Shibuda akashindwa kuelewana lugha na Bw. Wenje, huu huwezi kuuita kuwa ni ugomvi, ni kutofautiana kwa lugha tu ni suala la kibanadamu, ninachowaomba, tuvumiliane, Bw. Shibuda bado ni mwenzetu, alieleza Bw. Mbowe.

Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi hao kuhusiana na suala la msimamo wa CHADEMA kukataa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ndani ya bunge kwa vile baadhi ya vyama hivyo havina msimamo kutokana na vingine kufunga ndoa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha alieleza kushangazwa kwake na huruma ya machozi ya mamba kwa binadamu iliyooneshwa na Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda ndani ya bunge kwa kuvitaka vyama vya upinzani kushirikiana kwa lengo la kuwa na nguvu imara, kitendo ambacho alisema si huruma ya kweli.

Ndugu zangu haiwezi kutokea hata siku moja, adui yako akakupa ushauri wa jinsi ya kupata nguvu ili uweze kumteketeza kama alivyojaribu kufanya spika wetu wa bunge. Huyo anadai wapinzani tuungane ili tuwe na nguvu bungeni, si kweli maana tukiwa na nguvu zaidi tutakishinda chama chake.

Hizi zilikuwa ni mbinu tu za CCM katika kujaribu kusambaratisha upinzani hapa nchini, lakini sisi CHADEMA tumekataa na kubaki na msimamo wetu, hata mawaziri vivuli wote wanatokana CHADEMA, bado tunawapima hawa wenzetu ili tuone kama kweli wana dhati ya kuwa wapinzani dhidi ya CCM, alieleza Bw. Mbowe.

10 comments:

  1. lazima mjiulize nyie hapo mnaonekena kama kunguru wa zenji mwenzenu kapiga jezi yake nyie zenu mbona hazifanani nanyi ?mnajidanganya tena poleni sana tu safari ni ndefu sana tu

    ReplyDelete
  2. HATA mie ninazo jezi za namna hiyo kadi juu lakini mawazo yangu yoooooooote yako CHADEMA nguo haziwasilishi mawazo yako, wafanyabiashara kibao nje picha ya Kikwete waulize ndani ya roho zao kuna nini? Maanna ninyi CCM hamchelewi kusumbua watu ndo maana mmevaa ngozi ya KONDOO lakini nje ni MBWA MWITU WAKALI, angalia, KAGODA, EPA, MWANANCHI GOLD, MEREMETA, RICHMOND, DOWANS, KASHFA ZA MAGOGO, NOTI MPYA, MASHANGINGI YA WABUNGE na BAJAJI ZA WAJAWAZITO, MABOMU MBAGALA & GONGOLAMBOTO na mengine mengi. TUSHASHTUKA

    ReplyDelete
  3. mimi ni afisa wa serkali lakini kila nikitoka tu gari yangu ina kipeperushi cha chadema... kila wiki endi niko ndani ya kombati..yaani ndo kasho wea yangu....kadi yangu haibanduki kwenye mfuko wango wa shati...anayenidadishi humwonyesha mara moja!! msiomamo wangu si siri..nimeuweka wazi...viva chadema!

    ReplyDelete
  4. chadema hoyeeeee!!!!!!!!!!!!pigananeni 2015 mwendo mdundo kuingia ikulu

    ReplyDelete
  5. utwatambua kwa matendo na si mavaz wala bendera zao. ccm ya leo nya kuganga njaa lakn kiroho na kihisia weng wakho chadema. tena sku hz utaonekana taahra ukijinadi kama mwana ccm.ni wasom wachache sana wako ccm na ukchunguza hata hao wanaganga njaa tu na c kwamba wana mapenz na chama. kla mwenye utsh na utmamu wa akl haez hata skju moja akabak ccm kwan n sawa na kujizka mwenyeswe. vjana wote wajuz wa mambo chadema na walio ccm wanaona aibu kwa washkaj zao

    ReplyDelete
  6. Ukiona mtu kavaa sare ya CCM hajajitambua bado na ni mzigo kwa taifa.
    Jaribu kufikiri nilikutana na mama mmoja kariakoo kavaa ndala na kanga imeandikwa chagua ccm, anatembea kwa miguu. Kachoka Je anafahamu analolitenda? Kaangalie mateja wa mbagala nao wamevaa! Hawa huwezi kutofautisha wenye akili timamu, watu safi, watu wachafu, wajinga na werevu

    ReplyDelete
  7. Tuombe MUNGU kwan bila yeye ss hatuwezi chochote km chadema ni ya kupata madaraka itapata tu ila c kwa mababe.

    ReplyDelete
  8. Loo poleni Watanganyika ,kama mkiruhusu hawa chadema (wakatoliki)wakutawaleni mmekwisha,na labda ndio huo mwisho wa dunia,babu alisema "sikio la kufa halisikii dawa".

    ReplyDelete
  9. Mtoa maoni Februari 28, 11:24 am ni mdini,mimi ni wa imani yako,lakini mbona maaskofu waliposema Jk ni chaguo la Mungu hukusema Jk ni mkatoliki?Yani hata kama nchi inauzwa wazi wazi watu wasiseme? ni halali kwako kukamuliwa bili kubwa dowans alipwe?

    ReplyDelete
  10. Acha uwongo ndugu yangu wa February 28, 2011 1.58 PM. Ni maaskofu gani hao waliosema JK ni chaguo la mungu na niu mungu yupi huyo? Hivi wewe unawajua maaskofu wakanisa katoliki au unawasikia? Tamko hutolewa na muadhama Kardinali Pengo tu baada ya maamuzi kutolewa Tanzania Episcopal Centre Kurasini.

    Rais akiwa mkatoliki akienda kanisani yeye yu chini ya kiongozi wake wa kanisa ambaye huweza hata kumfutia dhambi zake, lakini akiwa muislamu hata yeye akienda msikitini anaweza kusimama pale mbele akawa imamu na kuwaongoza waumini walio nyuma yake. Hii ndio tofauti kubwa iliyopo kwa hiyo hizo propaganda za kusema sijui walisema chaguo la mungu kadanganye wengine wasojua mfumo wenu wa utawala wa KANISA ulivyo.

    ReplyDelete