28 February 2011

Kabila anusurika kupinduliwa

Na Mwandishi Wetu

Rais Joseph Kabila amenusurika kupinduliwa jana katika jaribio lililoshindikana na kusababisha watu saba kuuawa.Habari kutoka Kinshasa zinaeleza jaribio la
kumpindua lilifanyika katika makazi yake na kuzimwa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC, Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa alithibitisha kumetokea taarifa hizo huku akisema watu waliohusika bado walikuwa bado hawajajulikana.

Rais Kabila aliyekuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo, aliingia madarakani baada ya kuuawa baba yake aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Laurent Kabila mwaka 2001.

"Tumeshuhudia jaribiwa la mapinduzi, alisema Waziri wa habari wa nchi hiyo, Bw. Lambert Mende alilieleza Shirila la habari la uingereza, Reuters na kuongeza:

"Kundi la watu wenye silaha kali lilivamia makazi ya rais. Walizuiwa kwenye kizuizi cha kwanza. Askari wetu walipambana nao, baadhi yao walikamatwa na wengine sita kuuawa."

Bw. Mende alisema hali imedhibitiwa na mamlaka za serikali zilikuwa zinachambua ili kubaini wahusika.

Hata hivyo, habari nyingine zilisema kuwa wakati wa jaribio hilo, Rais Kabila hakuwa kwenye makazi yake.

6 comments:

  1. Ukiua kwa upanga na wewe utauawa kwa upanga pia. Hakuna ajabu hapa.

    ReplyDelete
  2. Afrika kumekucha - kama si kwa maandamano, basi ni kwa risasi kupinduliwa kwa marais ambao wananchi wanaona hawana tija kwa maendeleo yao. Hivi zamu ya Tanzania bado haijafika? Tungefanya kama Misri tu kwa vile kwa sasa hivi jeshi la polisi limeshaelewa ni nini maana ya nguvu ya umma. Ona walivyowalinda wananchi kwenye maandamano ya CHADEMA Mwanza na Musoma. Jeshi la polisi hoyeeee! Hivyo hivyo, waungeni wananchi mkono ili kweli ifanyike. Hata JWTZ nao wanaelewa - ona wanavyoyaachia mabomu kulipuka hovyo - ilikuwa Mbagala mara mbili, Gongo la Mboto maara moja, nasikia juzi ilikuwa Sumbawanga. Hivyo hivyo, twende!.

    Tumechoka na uongozi wa JK usio na mwelekeo - amekuwa automatic pilot bwana huyu. Nchi inajiendea ko kote, na ki vyo vyote.

    Alipishana na Al Adawi angani akienda kusuluhisha kwa jirani wakati kwake kunabomoka na mabomu- yaani ni aibu tupu. Alimwalika huyu bwana, lakini akijua fika kuwa watapishana angani, na Rostam Azizi atakuwepo kumpokea mfadhili wao kwa kampeni za urais kwa Lowassa 2015. TUMEKWISHA!!!

    ReplyDelete
  3. Maoni ya msiri ya tarehe Feb,28/11 saa12.27AM kwangu yamenikera hususani unapofurahia vifo labda hujashika bunduki ukaona utamu wake.Jk hana la kufanya yanayotokea hukoZaire au kwingineko.unachotakiwa kuona mabadiliko Tanzania ni kutoka kwenda kupiga kura na uwahamasishe wote kujitokeza kwa hilo.Kikwete si Raisi wa maisha huchaguliwa na wapiga kura kama wewe na kipindi chake kikifika atateuliwa Rais mwingine kutokana na mapenzi ya watanzania.Vyama vya upinzani vianze kuungana kwa pamoja na kuwa na sauti moja vitashinda.Kwa wote wapinzani tamaa inawakaba koo ni kazi ngumu kwao kuwa pamoja kama Taifa.Mimi nipo nawatizama kama jicho la popo

    ReplyDelete
  4. Unajua,

    Katiba ndio mambo yote. Hebu tuungane kudai hili kwanza mengine yatafuata.

    ReplyDelete
  5. muuuuu.we hata za hivi au ya nchi yako unaijua mpaka uombe kubadilishwa shagala bahoooooo.

    ReplyDelete