21 February 2011

CRDB yatoa msaada wathirika wa mabomu

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imeguswa na tukio la mlipuko wa mabomu lililotokea katika Kambi ya Jeshi la Wananchi JWTZ Gongo la Mboto jijni Dar es Salaam na
kutoa msaada wenye thamani sh. milioni 20.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Bi.Tully Mwambapa akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Galawa kwenye uwanja wa Uhuru, alisema benki hiyo  imepokea kwa masikitiko tukio hilo na inaungana na Watanzania wote kuwapa pole wale wote walioathrika na mabomu.

"Tunaungana na Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi na Watanzania wote kuwafariji na kuwapa pole waliopeza watoto, ndugu na wale walipoteza ndugu waliopoteza maisha kutokana, tunatoa msaafa huu uweze kuwasaidia wale wote walioathrika na mabomu.

Bi.Tully alisema kuwa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya hiyo Dkt. Charles Kimei wameguswa na tukio hilo hivyo wanatoa msaada wa blakenti na mashuka 200, na vyakula mbalimbali kwa wale walioathirika na mabomu.

Naye,Bi. Galawa aliipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa msaada huo umeonesha kuwajali na upendo kwa Watanzania, vilevile alisema kuwa wanaendelea kuwahudumia watu walioko Uwanja wa Uhuru kusaidia kuwapata wale ambao wamepotelewa na watoto na ndugu zao pia akatoa wito kwa watu kuchangia zaidi kwa kuwa mahitaji yanahitajika zaidi kwa waathrika.

No comments:

Post a Comment