21 February 2011

CHADEMA yatoa dawa Gongolamboto

Na Gladness Mboma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetembelea na kuwafariji majeruhi wa ajali ya milipuko ya mabomu iliyotokea Februari 16 katika
kambi ya 511 KJ Gongolamboto waliolazwa katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.

Mbali na kuwafariji chama hicho pia kimetoa msada wa dawa yenye thamani ya zaidi ya sh. 600.000 na shuka 166.

Ziara hiyo ya wabunge na viongozi mbalimbali wa CHADEMA iliongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa pia walikwenda kuaga miili ya familia moja ya watoto na mke wa Bw. Jacob Nyajiego waliofariki kwa milipuko hiyo.

Akikabidhi msaada huo wa madawa, Dkt. Slaa alisema kuwa CHADEMA wameguswa na matatizo hayo yaliyowakumba Watanzania wenzao na kwamba dawa walizotoa zinaendana na mahitaji halisi.

Dkt. Slaa alisema kuwa wakati walipokuwa katika Hospitali ya Amana walielezwa kwamba kuna upungufu wa mashuka na kwamba leo watapeleka mashuka 166 kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

"Kesho asubuhi tutapeleka mashuka 166 kwa sababu tumeelezwa kwamba kuna upungufu wa mashuka na tutamkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana,"alisema.

Alisema kuwa msaada wa dawa na mashuka yote wataelekeza katika Hospitali ya Amana ambako walitembelea na watendelea kutoa msaada zaidi pale itakapowezekana.

Wakati huo huo kampuni, taasisi mbalimbali zimeendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula nguo, mahema kwa wathirika wa mlipuko wa mabomu hayo.

Akitoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni saba. Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Dalali wa Mahakama ya Yono Auction Mart, Bi. Scholastica Kevela alisema  kutokana na tukio hilo imeguswa na janga hilo.

Bi. Kevela alisema kuwa kampuni hiyo inafanya kazi na jamii, hivyo ni wajibu wao kusaidia jamii kupitia janga hilo kwa hali na mali.Nao Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kupitia Shirikisho la Vyuo Vikuu Dar es Salaam walitoa msada wa sh. 400,000  kwa ajili ya kusaidia majeruhi hao na waathirika wa mlipuko huo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa tawi wa  shirikisho hilo, Bw. Kusekelo Melson alisema kuwa fedha hizo zimepatikana baada ya kuchangishana.

Taasisi zingine ambazo zimetoa misaada mbalimbali vyakula na nguo ni ni Jumuiya ya Memon, Taasisi ya dini ya kisabato kutoka Tabata Kisukulu, Hindu Mandal na  Lions Club ya Dar es Salaam

Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick alisema kuwa misada yote hiyo itakusanywa sehemu moja kwa lengo la kuhakikisha kwamba inawafikia wathirika wote.

"Michango yote ambayo inatolewa na wahisani na wasamaria wema tungependa ipitie katika mkondo mmoja ili uthibiti uweze kuwa mzuri na pasiwepo na malalamiko,"alisema.

Alisema kuwa wao ndio wanaojua waathirika wa mabomu hayo waliko na kusisitiza kwamba misaada yote hiyo itawafikia ambapo alitoa wito kwa wasamaria na taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada hiyo.

Naye Laurent Samatta naripoti kuwa Kampuni ya Mariedo inayojihusisha na mavazi imekabidhi misaada ya vyakula,nguo na maji kwa watoto waliyo athirika na milipuko ya mabomu
yenye thamani ya sh. milioni 3.

Akikabidhi msaada huo jana Mkurugezi wa kampuni hiyo, Bw. Edward Amri, alisema kwa upande wao wamepokea maafa hayo kama janga la kitaifa ambalo linahitaji huruma za kila Mtanzania kusaidia waathirika.

Alisema wataendelea kutoa misaada kwa watoto hao hadi pale serikali itakapo wapatiwa makazi ya kudumu ikiwa sambamba na kukutana na wazazi,ndugu au walezi wao.

Alisema kampuni yao ilikuwa inajihusisha na utoaji misaada kwa yatima na wamepanga kuongeza bajeti yao ili  kufanya kazi kwa umakini  ya kuwafikia walengwa wakuu.

5 comments:

  1. Napenda kuwapongeza sana CHADEMA kwa umakini wenu na busara yenu ambayo imeawavutia hata viongozi wa EU hasa baada ya CCM kuiba kura. mnazidi kuonyesha jinsi mnavyolipenda Taifa. msife moyo endeleeni kuwa na wanyonge ipo siku mtakaja ingia IKulu.
    BALAA ZOTE HIZI NIKWASABABU YA KIKWETE KUFANYA KAZI KWAUDICTETA NA KULUNDIKA MARAFIKI KAZINI NA HIVI HATA MAJUKUMU NYETI YANAFANYWA KWA MZAHA. UFISADI WA CCM DIO UTATUMALIZA WATANZANIA. NA UPOLE WETU SASA UMEKUWA UTUMWA WETU, KUKUMPA KURA KIWETE INGAWA EU IMESHUHUDIA KUWA ALIIBA KUURA BASI NDIYO MATOKEO HAYO. WAVAA KOFIA NA VITENGE VYA CCM MNAONA MATOKEO????

    ReplyDelete
  2. kwanza napenda sana kuwapongeza wale wote waliojitolea kuwasaidia waathirika wote wa mabomu kwani wameonyesha moyo wa ushirikiano na MUNGU awasaidie kwa huo moyo mliouonyesha mbarikiwe sana na MUNGU

    ReplyDelete
  3. hongera sana chadema. kikwete unaelinda uzembe na unaeongoza serekali isiyowajibika utafute pa kukimbilia!

    ReplyDelete
  4. Tuwe na Uzalendo na huruma kwa wenzetu waliofikwa na maafa.Nchi hii inapokwenda siko,hii sasa ni Domo krasia na si Demokrasia.Mtu anaambiwa toa maoni,anachotoa ni upupu mtupu mwanzo mwisho la maana hakuna ila propaganda za Siasa ooooh kikwete,oooh kura.Tuwe na akili ya kujua ni wakati gani tuseme nini.Hoja hapa ni ushiriki wa wenzetu katika kutoa misaada kwa waliofikwa na maafa,tulipaswa kushukuru na kujiimiza ili tuweze kuongeza misaada hiyo na si porojo.

    ReplyDelete
  5. Ninawapongeaza wote mliojitokeza kutoa misaada kwa wahanga wa janga hili la milipuko. Ila mimi ninapata wasiwasi kama kweli watanzania tutaweza kukabili majanga haya kwa kujitokeza kwa wingi kutoa misaada baada ya matukio, mimi nadhani tungejitokeza kwa wingi katika kushiriki kuzuia ingekuwa jambo bora kuliko hivi tufanyavyo sasa.

    Hainiingii akilini kwa nchi kama ya Tanzania yenye wanajeshi wasiozidi 25,000 na kambi za jeshi zisizozidi 500 kupata majanga makubwa kama haya mara 2 ndani ya miaka 2, mbona nchi kama Israel au Misri zenye idadi kubwa ya makambi ya jeshi na wanajeshi kwa nini mambo kama haya hayotekei? tatizo ni kambi za jeshi au sisi wenyewe?, hivi tunajichunguza tatizo liko wapi ili tulimalize au tukimbilie kupeleka mashuka na madawa na kutoa damu zetu bila kuangalia asili ya tatizo lenyewe?. Tangu tupate uhuru kambi hizi za jeshi zilipoanzishwa, kwa nini kipindi chote huko nyuma mambo haya hayakutokea yatokee sasa hivi? ingekuwa mara moja tungesema ni bahati mbaya kama tukio la MV Bukoba, ila kwa kuwa limetekoa mara ya pili si bahati mbaya; ama kuna mkono wa mtu, au ni uzembe uliokithiri. Kati ya haya mawili wewe unadhani lipi linafanana na tukio hili, na nini kifanyike ili kuzuia jambo hili na yanayofanana na hili yasitokee tena?, kauli za viongozi wetu kwamba hayatokei tena haziaminiki na kamwe tusizisikilize, kwa sababu baada ya tukio la Gongo la mbali, walisema kauli hizi hizi, la kusikitisha zaidi ni pale kauli kama hizi za kipuuzi zisizofanyiwa utafiti zinatoka mdomoni mwa rais wa nchi, na sasa anarudia tena maneno yale yale bila haya.[MKINICHANGIA NAULI, NITAKWENDA KUMPA JIBU MJOMBA PALE IKULU, AKIRUDI TOKA HUKO ALIKO]

    ReplyDelete