MADRID, Hispania
KLABU za Arsenal na Barcelona, zimeingia katika bifu jingine huku zikikabiliwa na mechi ya marudiano.Miamba ya Hispania, Barca imekasirishwa na
kitendo cha Arsenala kutaka kumsaini mchezaji wake kinda mwenye umri wa miaka
16, Jon Miquel Toral Harper kutoka kwenye shule yao ya soka kama walivyofanya kwa Cesc Fabregas.
Gazeti la SunSport limesema klabu hizo zilianza kukorofishana kabla ya mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, iliyochezwa Jumatano iliyopita katika Uwanja wa Emirates ambapo Rais wa Barca, Sandro Rosell alieleza hisia zake kwa mtendaji wa Gunners, Ivan Gazidis.
Shuhuda alisema: "Rosell alionekana kupaza sauti yake kwa Gazidis, ambaye alionekana kukaa kimya na kutojibu. Ilikuwa wazi kwamba Rosell alikuwa amekasirika."
Miamba ya Catalan imekasirishwa na
Gunners kwa kujaribu kumchukua mchezaji wa kiungo Toral. Mchezaji huyo mama yake ni Mwingereza, inaeleweka kuwa sasa ni karibu kusaini mkataba wa kuanza kucheza soka ya kulipwa akiwa na Gunners.
Mchezaji huyo tayari alishatolewa kwenye tangazo la Nike, akiwa pamoja na Fabregas!
Hali hiyo inaweza kuongeza upinzani zaidi kwa klabu hiyo katika mechi ya marudiano katika Uwanja wa Nou Camp ambapo, Arsenal itakuwa ikitetea ushindi wake wa mabao 2-1.
Hadi sasa hakuna kitu ambacho kimefanyika, lakini miamba ya Hispania haitaki kuona mchezaji wao akiondoka.
Hasa Rosell ambaye alikuwa Makamu Rais wakati Gunners ilipomchukua, Fabregas mwaka 2003.
Kwa sasa inaonekana Arsena inataka kuwazunguka tena Barcelona kwa kutaka kumchukua kinda huyo.
Barcelona imekuwa ikitangaza kuwa inamtaka, Fabregas na katika majira ya joto ilitangaza ofa ya pauni 31, lakini kocha wa Gunners, Arsene Wenger alikataa kumuuza.
Wenger amekuwa na hasira akituhumu
Barcelona kwa kutumia mbinu chafu kumnasa Cesc.
Arsenal na Barcelona, zitapambana katika Uwanja wa Nou Camp Machi 8, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment