14 January 2011

Polisi waua tena wawili Mbarali

*Wajitetea kwa mauaji ya Arusha

Na Rashid Mkwinda, Mbarali
VURUGU kubwa imeibuka wilayani Mbarali mkoani Mbeya katika kata ya Ubaruku baada ya kundi la wananchi kuvamia lori la mafuta na kulichoma moto na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kumfyatulia
risasi mtu mmoja na kusababisha kifo chake.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimedai kuwa chanzo cha vurugu hizo ambazo zimetokea majira ya mchana jana zimetokana na kundi hilo la wananchi kukerwa na lori lenye uzito wa tani 10, kuruhusiwa kupita katika barabara ambayo imezuiwa kupitisha magari yanayozidi tani 8.

Barabara hiyo ya Rujewa-Ubaruku ilipigwa marufuku kupitisha magari yenye uzito wa zaidi ya tani 8 ambapo wafanyabiashara kadhaa wa mpunga wameshindwa kusafirisha mpunga wa wananchi kutokana na kuzuiwa kutumia barabara hiyo, lakini wakashangaa kuona lori la mafuta likipita bila kuzuiwa.

Kutokana na hali hiyo, walipoliona gari la mafuta lenye uzito wa tani 10 mali ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Munif likiwa likitumia barabara hiyo, wananchi hao walilivamia na kuzuia lisiingie kijijini, ndipo polisi walipoingilia kati kuwatawanya wananchi hao.

Kabla ya wananchi hao kulivamia na kulichoma moto gari na kituo cha mafuta, FFU walifika eneo hilo na kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi, lakini askari hao walikaidi na walipolemewa nguvu, waliamua kufyatua risasi za moto zilizosababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Justin, na mwingine kujeruhiwa.

Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Bw. Cosmas Kayombo alisema kuwa vurugu hizo zimeibuka baada ya wananchi kulizuia gari hilo lenye uzito wa tani 10 ambapo mtu mmoja alipigwa risasi ya moto na kuuawa na mwingine ambaye bado hajafahamika jina lake alijeruhiwa kwa risasi.

Taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni ni kwamba majeruhi huyo naye alifia katika Hospitali ya Misheni ya Rujewa.

Bw. Kayombo alisema kuwa amelazimika kuwasiliana na uongozi wa mkoa wa Mbeya ili kuongeza nguvu ya ulinzi katika kata hiyo ambapo makundi ya wananchi wenye hasira wameonekana wakizagaa huku na huko katika mitaa ya mji wa Ubaruku.

Kamanda wa Polisi mkao wa Mbeya, Bw. Advocate Nyombi alipoulizwa jana, alisema yupo njia kuelekea eneo la tukio na kuwa angetoa taarifa leo.

Wakati huo huo, Agnes Mwaijega anaripoti kuwa Jeshi la Polisi limejikosha kwa hatua yake ya kurusha risasi za moto na kuua watu watatu kuwa haikusababishwa na kitendo cha kusitisha maandamano ya wafuasi wa CHADEMA, bali uchochezi wa viongozi wa chama hicho katika mkutano wao ndiyo chanzo cha yote yaliyotokea mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Operesheni maalumu nchini, Bw. Paulo Chagonja alisema Jeshi la Polisi lilisitisha maandamano kwa amani na kuwakamata viongozi, na kuwaruhusu CHADEMA kwenda kuendelea na mkutano wao ambako huko ndiko vurugu zilikoanzia.

Alisema viongozi wa kitaifa wa chama hicho akiwemo Dkt. Willibrod Slaa (Katibu Mkuu), Bw. Philemon Ndesamburo (Mbunge Moshi Mjini) na Samson Mwigamba ambaye ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha walipandikiza maneno ya uchochezi na kuwahamasisha wafuasi wao kwenda kuvamia kituo kikuu cha polisi ili kuwatoa watuhumiwa saba waliokamatwa kwa kupuuza amri ya jeshi la polisi kuwataka kusitisha maandamano.

Kwa mujibu wa CHADEMA, amri hiyo ya polisi kusitisha maandamano hayo ilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa njia ya vyombo vya habari, saa chache kabla ya maandamano hayo, wakati Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha alikuwa ameshatoa barua kuyaruhusu.

Bw. Chagonja ambaye alikataa kuulizwa maswali, alisema kufuatia hamasa waliyotoa viongozi hao, wafuasi wa CHADEMA wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 3,000 walifanya matukio mengi ya uhalifu wakiwa wanaelekea kituoni kama vile kuchoma duka la Bw. Salum Ally kuvamia vituo vidogo vya polisi Unga Limited, Maraa na Kaloleni; uhalibifu wa ofisi ya CCM, magari, miundombinu ya shule ya msingi Kaloleni na kuwabughudhi raia wengine ambao hawakuwemo kwenye maandamano yao.

Kama ambavyo imekuwa ikidaiwa kuwa kama polisi wasingezuia maandamano, vurugu na mauaji yasingetokea, Bw. Chagonja naye alidai kuwa kama viongozi wa CHADEMA wasingepandikiza maneno ya uchochezi kwa wafuasi wao, watu wasingekufa wala kujeruhiwa.

Wakati anakiri kuwa risasi za moto zilifyatuliwa na polisi na kuwaua watu na wengine kujeruhiwa, Bw. Chagonja aalihamisha lawama hizo kwa CHADEMA: "Jeshi la polisi halikusababisha watu kufa wala kujeruhiwa, bali matukio yao ya fujo ambayo yalichangiwa na uchochezi kutoka kwa viongozi wao wa juu, ndiyo chanzo kikubwa.

"Jazba zilizopandikizwa kwa wafuasi na kutaka kushindana na jeshi la polisi ndizo zilizochangia yote yaliyotokea," alisema.

Alisisitiza kuwa kama jeshi la polisi lingekuwa limezuia maandamano kwa kutumia nguvu, ni dhairi kwamba wafuasi wa chama hicho wasingeweza kufanya mkutano walioufanya jioni.

Pia alisema awali maandamano hayo yalisitishwa na jeshi hilo baada ya taarifa za kiintelenjisia kuonesha kuwa yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani mjini Arusha.

Hata hivyo, wafuasi wa CHADEMA katika hali isiyo ya halali Januari 5, mwaka huu waliandamana zaidi ya kilomita moja wakitokea hoteli ya Mount Meru kwenda viwanja vya NMC kwa ajili ya mkutano huku wakiwa na jazba, hatua iliyosababisha jeshi hilo kusitisha maandamano hayo.

Alisema kingine kilichochangia kusitisha kwa maandamano hayo ni ukiukaji wa makubaliano waliyokuwa wameyaweka kati ya jeshi la polisi na CHADEMA ambayo yaliwataka kutumia njia moja wakati wa kuandamana, ingawa hakueleza kama maandamano hayo yalikuwa yamesababisha ub=vunjifu wowote wa amani.

 "Waliandika barua ambayo haikuonesha kuchagua njia mojawapo kati ya zilizopendekwa, bali waliongeza nyingine ambayo ingeongozwa na Dkt. Slaa ikianzia uwanja wa ndege mgogo wa kisongo kinyume na maelekezo ya jeshi la polisi Arusha," alisema.

Bw. Chagonja alisema taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa tangu kutokea kwa vurugu zilielemea upande mmoja wa kulilaani jeshi hilo bila kuangalia nani chanzo.

Alisema operesheni ya kurudisha taswira ya mji wa Arusha katika hali yake umekamilika ila Mkurugenzi wa makosa ya jinai kwa kushirikiana na timu ya wadau wengine kama vile Haki jinai, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na mwanasheria mkuu wa serikali wanaendelea na upelelezi juu ya makosa mengine ya kijinai yaliyotemwa kwa upande wa CHADEMA.

12 comments:

  1. Acha ujinga. Laana hizo zinawanyemelea wote walioua. Mkwere kakaa kimya na Mungu atamwonyesha.Yupo anafikiria mgao wa Dowans. Hivi makamba, mkwere walilelewa na wazazi kweli???

    ReplyDelete
  2. Labda wewe ndio mtoto wa mitaani maana hutaki ukweli,huko kituo cha polisi mlikuwa mnaenda kufanya nini?

    ReplyDelete
  3. Chagonja mungu akusamehe je?angekuwa mwanao amepigwa Risasi ungeongea maneno hayo?Ninaimani mungu atulipia tu.Ukumbuke kuwa CCM haitatawala milele.Ninakuomba ukae kimya kama Mh.Rais alivyo kaakimya

    ReplyDelete
  4. haya sasa wanaolitetea jeshi la polisi kuwauwa waandamanaji wa chadema Arusha wajitokeze tena.Haiingi akili jeshi kuua badala ya kulinda raia.huko mbeya mtu kapasuliwa kichwa kwa risasi ndo polisi jamii gani hii mnatuambia watanzania.

    ReplyDelete
  5. Waache kutufanya mafala, tumeiona wenyewe halafu unatuletea stori za kijinga hapa.

    ReplyDelete
  6. Amri Jeshi Mkuu amka kumesha kucha. Vijana wako wanajifunza kulenga shaba kama wanaweza. Sasa hii haivumiliki, kazi ya polisi wanaijua lakini wanafanya makusudi, na wanatupima tunauwezo gani?
    Sasa wananchi wakijibu itakuwaje, mimi ninajiwe langu mfukoni ole wake aniguse. ninamuwahi kabla hajaniwahi.

    ReplyDelete
  7. Sasa walichokuwa wanakataa hawa polisi kwamba hawafanyi kazi za CCM ni nini? Kwa hiyo walipigwa risasi kwa sababu ni wanachama wa chadema wangekuwa wa CCM mpaka godoro wangepewa.

    ReplyDelete
  8. Chagonja
    Pale Mount Meru Hotel mlipokuwa mnapasua vioo vya Land cruiser nyekundu si kabla ya watu hawajafika uwanjani? re play kanda za matukio ya mauwaji Arusha. kuwa mwangalifu sana unapotowa taarifa you can fool the people all the time.

    ReplyDelete
  9. Stupid polisi! tena msitufanye hatuna akili. tumeyaona wenyewe huku Arusha hatukusimuliwa na nyie kuchukua mkinda ya video mkachakachua. Mlianza kutoa kipondo kule juu, hata kituo cha polisi ni mbali kutoka mliopoanza kutoa kipondo, na watu walikuwa wanaelekea uwanjani. Changonja kumbe hata wewe huna akili! siye wanainchi tuna akili kuliko mnavyodhani. Taratibu na uchakachuaji wenu. Nyambafuuuuuuuuu!

    ReplyDelete
  10. Chagonja kwa nini ukatae maswali.hii nchi ni ya Mungu sio ccm.msijisahau

    ReplyDelete
  11. Saidi Mwema na wenzako, makamba na mama Chatanda Hakika naomba mjue kuwa Mungu Yupo na malipo ni hapa hapa Duniani. Si siku nyingi mtajutia haya mliyofanya. Machungu waliopata Watanzani mlioua ndugu zao yatawapata mara dufu. Si hata nyie mna watoto?

    ReplyDelete
  12. SERIKALI ACHENI KUFANYA UNYAMA KWA KUFUNIKA KWA NGOZI YA KONDOO VUENI HIYO NGOZI YA CHUI. KIKWETE MAHAKAMA YA OCAMPO INAKUSUBIRI. TUNAOMBA MASHIRIKA YANAYATAFUTA HAKI ZA BINADAMU MUWE NA KUMBUKUMBU ZA KUTOSHA. ACHENI POLISI ACHENI KUUWA WATANZANIA KAMA NGEDERE. KWANZA MNAPOTEZA SIFA YA JESHI LENU.

    Walidai kwamba baadhi ya viongozi wa wa serikali ngazi ya wilaya pamoja na baadhi ya polisi, ndiyo chanzo cha vurugu hizo zilizosababisha mauaji ya mtu mmoja.

    Wakielezea jinsi mwezao alivyouawa, walisema kuwa aliyeuawa alikuwa akibiashana na polisi na baada ya mvutano ndipo alipochukua bunduki na kumpiga risasi kwenye paji la uso.

    ReplyDelete