14 January 2011

Magufuli asaini mikataba ya barabara

Na Benjamin Masese

WAZIRI wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli amesaini mikataba ya ujenzi wa barabara za lami za urefu wa km 260 huku akiwajia juu makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoka nje kuifanya Tanzania kituo chao cha kuchota fedha kirahisi
na kujenga barabara chini ya kiwango.

Dkt. Magufuli alitoa tamko hilo  Dar es Salaam jana wakati wa kusaini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara kiwango cha lami kati ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kandarasi na wasimamizi kutoka kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Kabla ya kuweka saini Dkt. Magufuli alisitisha kwa dakika kadhaa na kusema kwamba anazo orodha ya kampuni nyingi kutoka nje zilizowahi kufanya kazi ya ujenzi na kuboronga ambapo hadi sasa zipo zinaendelea kuomba zabuni na kupewa huku zikishindwa kukamilisha kwa wakati.

Aliitaja Kampuni ya M/S China Sichuan International Cooperation co. Ltd kuwa ni moja ya kampuni inayofanya kazi kwa kuboronga.

Alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa kubabaisha huku ikibuni majina mengine na kuomba zabuni mbalimbali za ujenzi na kusisitiza kwamba hataivumilia kwa kipindi hiki cha uongozi wake kama itashindwa kutekeleza masharti iliyosaini jana

Dkt. Magufuli aliwataka wakandarasi wazalendo kuungana na kuomba zabuni ili kuokoa fedha zinazochukuliwa na wageni huku wao wakibaki kuwa wasimamizi wa ujenzi na si kunufaisha nchi zingine.

Alimtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Bw. Patrick Mfugale kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa ubora unaostahili na ikiwa atashindwa ni vema kunyonga na si kuachia madaraka kwa kuwa bado atakuwa anamwaibisha.

"Nashukuru tumeuanza mwaka mpya na ujenzi wa barabara mpya na wizara mpya, hili nalisema wazi anayefanya kazi na mimi ni vema akababadilika mapema kuhusu utendaji wake kabla sijamfikia kumwambia Bw. Mfugule naomba uwe mkali kusimamia shughuli za TANROADS sehemu inayotakiwa kubomolewa ibomolewe haraka na hakuna malipo yoyote kama nyumba imejengwa kwenye hifadhi ya barabara," alisema.

Dkt. Magufuli alisema kuwa Wizara inaandaa sheria zinazohusu ujenzi wa nyumba pamoja na barabara na kuzisambaza katika mahakama zote chini ili wanaopeleka madai ya kubomolewa nyumba zao wapewa uelewa zaidi.

Alisema kuwa katika utendaji wake hataangalia ukubwa wa kiongozi na nafasi aliyonayo kama hakufuata sheria na kuongeza kuwa ni vema kulaumiwa huku akitekeleza sheria.

Alisema kuwa serikali inatambua adai ya makandarasi na ambapo Rais Jakaya Kikwete amemhakikishia yatalipwa hivi karibuni.

Barabara hizo ambazo zilitiwa saini jana ni kutoka Iringa, Dodoma hadi Migori yenye urefu wa kilomita 95.2 itakayojengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya M/S China Sichuan International Cooperation co.Ltd  kwa gharama ya sh. 84, 216, 378, 355. 50 na itakayokamilika ndani ya miezi 35.

Nyingine ni Iringa,  Dodoma,  Migori  hadi  Fufu yenye kilomita 93 inayojengwa na kampuni hiyo hiyo kwa gharama ya sh. 73, 612, 329, 958. 67 pia barabara kutoka Iringa, Dodoma-Fufu yenye kilomita 70.9 inayojengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya M/S China Communications  Construction co. Ltd  kwa gharama ya sh. 64,327,389,129  ndani ya miezi 27.

Mbali na wakandarasi hao kutia saini ya ujenzi, TANROADS imewekeana saini na wasimamizi hapa nchini wa ujenzi wa barabara nyingine zilizokuwa zikijengwa bila kuwa wasimamizi.

Barabara hizo ni Nyanguge hadi Musoma, za-Musoma, Tabora - Nyahua hadi Chaya, Tabora-Nyahua, Nzega-Tabora, Puge - Tabora na Kyaka - Bugene - Kasulo.

8 comments:

  1. Magufuli big up kwa wewe hakuna wasiwasi ngoma imepata mchezaji

    ReplyDelete
  2. Ungekuwepo Miaka mitano iliyopita Tanzania ingekaribia kufanana na Dubai! Miaka Mitano ijayo si mingi lakini pia si haba kazi tutaiona.

    Nakuomba sana Mhe Waziri fautilia kwa karibu ile bara bara ya Arusha Namanga na ile ya Kusini isiyokamilika miaka nenda miaka rudi. Sisi wakazi wa kusini tumekuwa tukipanda ndege kila wakati utasema tunakwenda Europe? Na sisi tunataka kutumia bara bara kufurahia uoto wa asili na kufunuka kwa biashara na uchumi wa eneo hilo.

    Watanzania tunakuangalia kwa karibu sana kama mkombozi wetu. Jk ameamua kutupa wapiganaji makini wakubwa katika kipindi hiki chake cha mwisho, wewe na yule mama wa ardhi!

    Asante sana Jk!

    Carwin.

    ReplyDelete
  3. Hivi barabara ya kutokea Mwadui-Maswa-Bariadi-Ramadi itajengwa lini kwa kiwango cha lami? Mbona tuliahidiwa tangia miaka mingi sasa!!

    ReplyDelete
  4. Tunataka pia Tunduma-Sumbawanga-Mpanda-Kigoma. Fanya mambo Magufuli na wewe Pinda usisahau kwenu!

    ReplyDelete
  5. Hivi wananchi wa Kibondo na Kasulu si sehemu ya watanzania hadi kunyimwa haki ya kuwa na barabara nzuri tangu tupate Uhuru?
    Inasikitisha mno kuona serikali inajirudiarudia katika baadhi ya mikoa ambayo tayari angalau imepata kuwa na barabara za lami.
    Ni aibu, ni fedheha kuona serikali hii ikishindwa kutia lami barabara ya Kigoma Nyakanazi na kushupalia barabara wanakotoka vigogo wa serikali.

    ReplyDelete
  6. KWA KWELI MI MHESHIMIWA MAGUFULI NAKUFAGILIA SANA.LAITI KAMA TUNGEKUWA NA MAWAZIRI WATATU TU TANZANIA NZIMA KAMA WEWE LAITI TUNGEKUWA MBALI.KUTOKANA NA KAZI YAKO NZURI NAOMBA NIKUULIZE HAYA MASWALI MACHACHE NAHISI UTYAFANYIA KAZI KWA UFANISI WKO;
    1.SASA KWA NINI HII KAMPUNI YA KICHINA AMBAYO UMEKIRI MWENYEWE KUWA INAFANYA KAZI KWA UBABAISHAJI UKAWAPA TENA KAZI ,TENA KUBWA TU YA BARARBARA YA IRINGA?
    2.WAITE HAO WAKANDARASI WA HAPA NCHINI WAPE SHULE NA UWAWEKE KARIBU NA KUSIKIA MAWAZO YAO KWANI SI AJABU WANAKWAMISHWA NA WATENDAJI WAKO KWA KUWAWEKEA UKIRITIMBA WA KAZI HIZO ZA BARABARA.

    ReplyDelete
  7. Dr you make me happy whenever i read your news concerning road projects in Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Waziri tunaifurahia kazi yako, hao Wachina ni wababaishaji tafuta macontractior wa uhakika kama wale waliojenga barabara ya Uyole - Tukuyu WALE NDIO WAJENZI HASA ukiiangalia barabara leo utafikiri imetengenezwa mwaka jana kumbe ni ya miaka nenda rudi.Msitafute vya dezo navyo vina gharama yake

    ReplyDelete