14 January 2011

Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Na Peter Mwenda
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema
kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.

55 comments:

  1. Asante, baba Kadinali Pengo, kwa msimamo wa kanisa, japokuwa wanambinu chafu ya kulipaka kanisa na mambo ya siasa msikate tamaa na wala msikae kimya katika kuwasaidia wananchi kutetea haki zao. Kwetu sisi wanyonge hiki ndio chombo cha kuweza kutusemea, kutusaidia kututetea maisha yetu na tunalolihihataji. Panapokuwa na tatizo lazima serikali itambue na kulishughulikia kwa wakati sio mpaka watusubiri tunafanya nini ndio waanze kutu miminia risasi hivyo ni kukomoana wakati mtanzania hana kosa. Hapa lazima serikali ijiulize kwanini wananchi wamekasirika hivyo ni nini kimewakwaza. Badala ya kutusaidia wanatumiminia risasi ili tuache kuwasumbua.

    ReplyDelete
  2. Asante Cardinal kwa maneno ya upole, busara na yaliyojaa hekima. Viongozi kama wewe ni muhimu katika kutetea uhai wa watanzania. tunaomba wanasiasa wasikilize kwa makini wanayoyasema viongozi wa dini ambao pia tunaamini ni manabii. Hivyo mtuepushe na maafa yanayoweza kutokeas tanzania.

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru Kadinali kuombea Taifa letu mema, na kukemea maovu hayo yote ni kutokana na mapungufu ya kibinadamu sidhani kama hawa askari walitumwa kufanya hayo mauaji ila ni utashi wao wasivyokamata mafunzo na maadili ya kazi yao. Mungu awalaze mahala pema peponi Amiin,Kadinali inabidi pia kukemea viongozi wanaodharau amri au maelekezo ya Serikali kwa mwamvuli wa upinzani, upinzani maana yake si kukaidi kila linalotoka kwa uongozi wa Serikali na pia Tumefurahi kuona safari hii mmeweza kukemea mauaji ilipotokea miaka ya nyuma kule Pemba kwa kuuwawa wanachama wa CUF zaidi ya 30 mlikuwa kimya safari hii mko makini!!

    ReplyDelete
  4. Pengo ukweli utabaki kua ukweli, polisi hawakuuwa raia kwenye maandamano ya amani, usitake kudanganya umma kwa kisingizio cha ukadinali wako. Slaa ndio kaua watu maana ni yeye aliyesema mtakubali vp Mbowe akamatwe? twendeni tukamtoe, na wale watu walikua wanakwena kituoni kwa jazba ndipo polisi walipoamua kutumia nguvu za ziada kujihami. Kama ni kweli unayosema Baba kadinali ni kweli jiulize hao watu wameuwawa wapi? kama si mita chache tu kutoka ktuoni. Au hayoo maandamano yenu yalikua yanafikia kilele kituo cha polisi? Acheni kutudanganya bwana, hayo ni maumivu ya kukosa urais wenu na ndio mnaanza kuweweseka sasa.

    ReplyDelete
  5. Ndiyo Kadinary Pengo, hata mimi ninaungana na wewe hata kama Polisi watadai kwamba walioandamana walikuwa wamekiuka sheria adhabu yao haikuwa kuwapiga risasi wananchi wasio nahatia. Hukumu yao haikuwa kuchukua uhai wao kwa njia ya kuwapiga risasi la hata kidogo. Ni kweli kabisa haijalishi walikuwa wamekosa kiasi gani. Wale waliokuwa kimbelembele wangeweza kukamatwa hata kesho yake na kufunguliwa mashitaka ya kuandamana bila kibali. Na sasa wameuwa Polisi wamejichukulia sheria mkononi badala ya kuwapeleka wahalifu mahakamani. Hapa ni lazima sheria ichukue mkondo wake. Hata kama haitakuwa leo au kesho lakini ni lazima waliomwaga damu ya watanzania wawajibishe wapewe haki ya malipo ya kumwaga damu za binadamu wenzao kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali. Ni wazi kabisa mauaji haya yalipangwa ili kuwapa hofu watanzania wanaounga mkono upinzani. Na hasa kwa kipindi hiki ambacho mafisadi wanataka kuchota fedha za watanzania kupitia Dowasons campuni feki. Wanajua wasipoua wananchi wataandamana kupinga malipo hayo hewa. Watanzania tusikubali hata kidogo ni bora watumalize sote tuishe. Kuliko kuendelea kutawaliwa na watu ambao ni makatili wa kutisha. Tulipigania uhuru wa nchi yetu ili tujitawale tuondoe ukatili wa mkoloni sasa badala ya kufanyiwa ukatili na mzungu tunafanyiwa ukatili na mtu mweuzi kama sisi. Jamani ukatili hauna rangi ndugu roho mbaya iko kwa wote tuwakatae hawa CCM kwa sababu wameacha maadili ya muasisi wa taifa letu.

    ReplyDelete
  6. MUADHAMA KADINALI PENGO,POLISI HAWAKUANZA KUUA LEO,WAMEUA PEMBA,WAMEUA WAISLAMU MWEMBECHAI,KUNA SHEIKH KASSIM BIN JUMAA WALIOTIWA NDANI HADI KUKARIBIA KUFA WAKATOLEWA,NI VIPI KAULI YAKO HII INATOKA LEO HAIKUTOKA WAKATI ULE? NDIPO TUNAPOTIA SHAKA KAULI ZENU VIONGOZI WA DINI YA KIKRISTO,SABABU MAISHA NI MAISHA TU YAWE YA MUISLAMU YAWE MKRISTO AU ASIYE NA DINI,HIVYO UKEMEAJI LAZIMA UWE WA HAKI,TUSIGEUZE NCHI KUWA NA MWELEKEO WA WAMERAKANI PALE AMBAPO WAISRAELI WANAWAUA WAPALESTINA WASIO NA SILAHA NA WALIOWEKEWA VIKWAZO VYA KUTOKUWA NA SILAHA HAWAKEMEI.HAKI HAIJI KWA MISINGI HIYO. 2. INASIKITISHA HUKUMKEMEA PADRI SLAA KWA KUAMRISHA WAFUASI WAKE WAKAVAMIE KITUO CHA POLISI ILI KUWATOA VIONGOZI WAO,UMESEMA KIJANJAJANJA TU ATI HATA WAKOSAJE BADO WANA HAKI YA KULINDWA MAISHA YAO.PADRI SLAA NDIO CHANZO CHA MACHAFUKO NCHINI NA BILA KUMKEMEA TUTAWAELEWA MKO PAMOJA NAYE KWENYE MIKAKATI YA KUHAKIKISHA NCHI HAITAWALIKI

    ReplyDelete
  7. Kama kila mkosaji anauawa na polisi, ni nani kumbe anatakiwa apelekwe mahakamani? Polisi wanang'ang'ania kwamba CHADEMA wana makosa, sawa. Lakini mkosaji hupelekwa wapi? Mbona kuua sio sehemu ya sheria za nchi hii? Tena kuua kunakofanywa na walinzi wa amani?

    Tukubaliane kwamba huu ni uvunjaji wa sheria. Kila mtenda kosa huwana maelezo. Hata makaburu enzi zao walikuwa na maelezo kwamba watu weusi wana asili ya kutenda maovu, na hiyo ikawa sababu ya kuwaua ovyoovyo. Kama walichofanya Polisi ni sahihi kwa nini dunia iliungana kuwashambulia makaburu?

    Tafakari, chukua hatua!!

    ReplyDelete
  8. Tatizo makadinali na maprofesa nchini hawako tayari kuunga mkono na kujitokeza kushiriki kwa vitendo katika maandamano ya kuzikomboa njia kuu za demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora nchini. Mafisadi huwa hawaogopi maombi, hotuba, wala mahakama, wanaogopa maandamano na mikutano ya hadhara maana hizo ndizo njia pekee zenye nguvu ya kusanya na kuratibu nguvu za umma unaodhurumiwa ili kufanya maamuzi. Mahakama, bunge na polisi vyote bado haviko huru mpaka sasa. Pengo na wenzako njooni barabarani tuandamane tuunganishe nguvu mafisadi hawataacha kwa kukemea madhabahuni na kuongea na vyombo vya habari tu. Labla maaskofu na mashehe na maprofesa wa vyuo vikuu na wazee maarufu nchini wangeshiriki maandamano yale hadothi ingekuwa tofauti leo, huwenda risasi zisingerushwa, n.k. Kila mtu anatambua kuna tatizo lakini hataki kuchukua hatua. Hutaenda peponi ukiwa hai, lazima ufe kwanza, watu wanahubiri pepo lakini kufa hawataki! maajabu hayo! Mashehe, maaskofu, wasomi, mzee Warioba, Msuya, Bomani, Butiku na wazee wengine msioridhishwa na mambo nchini unganeni na vijana wetu ktk maandamano ili kuikomboa demokrasia, haki na rasilimali zetu zinazoporwa na watu wachache.

    Hakuna chochote serikali wala polisi watakachosema kuhusu mauaji wakati wa maandamano yale. Sisi sote tujajua chanzo cha mauaji yale ni zile taarifa feki za kiintelegensia zilizotumika kufuta haki ya kikatiba ya wananchi ya kufanya maandamano na kukusanyika. Taarifa yoyote ile haikubaliki na hakuna mjinga sasa hivi. Heshima ya polisi imeanza kushuka mbele ya wananchi, ndiyo maana wananchi wanaua watuhumiwa wa uhalifu badala ya kuwapeleka polisi, wananchi wanachoma vituo vya polisi kwakuwa haviwasaidii lolote, wananchi wanaifahamu bei ya polisi hivyo wakikamatwa wanatoa pesa maana wanaijua bei yao ni sh. 2000, 5000 na akikosa chenchi ni sh. 10000 basi. Kazi ipo tuungane acheni porojo za madhabahuni na vyombo vya habari hazisaidii kuikomboa nchi hii.

    ReplyDelete
  9. Pengo umekwisha. Umesahau uchochezi mmeuanza nyie watu wa makanisa tokea awali kwa kukikumbatia chama. Mmewafukuza na kuwatenga watu kwa kukikataa chama cha Chadema. Mmetoa kauli kali pale Chadema wanaposhindwa lakini pale wanaposhinda mnakaa kimya au kupongeza.

    Mumemchagua padri agombee urais, yote hayo hamkuyaona, mlijiona wababe, tena mbele ya dola.Haya ndio matokeo yake. Kanisa ndio lakulaaniwa na inaonesha hata mungu wenu amechukia na kukuadhibuni.

    Pengo, utubu na utubu. Roho ni roho iwe Pemba au Bara na kama wewe ni mtu wa mungu ungelikemea polisi waliouwa watu zaidi ya 21 kule Pemba. Au kwa vile waliouwa walikuwa wanauwauliza wapemba "NANI MWENYE NGUVU MIMI AU ALLAH WAKO?"
    Tumesamehe lakini hatujasahau. Pengo umekosa heshima, tubu na utubie

    ReplyDelete
  10. asante baba ila nawashauri vijana msidanganywe na wanasiasa.Mimi nimepoteza mchumba wangu kenya ingawa harusi tulikuwa kwenye tangazo la kwanza. Wazazi hadi leo hawajapata hata shilingi wakati kina raila wanakunywa pombe.Zanzibar sefu wa wenzake wala chips wanyonge wako ahera. Chadema, CCm, CuF nk hakuna mwenye mapenzi mema, wote wezi, fanyeni kazi vijana, siku zitakuja ukoloni utakwisha hakuna serikali inayodumu milele ni Mungu pekee, kina kikwete wataondoka na ishaalah tutapata viongozi wema.

    ReplyDelete
  11. Kwanini Mbowe alikamatwa? Mbowe ni mwenyekiti taifa CHADEMA chenye wafuasi wengi nchini na hususani kanda ya kaskanini, hivyo kumkamata Mbowe ni kuchochea vurugu, hivi hata elimu ndogo hiyo polisi hamna? Hivi wanachama wa CCM watakaa kimya kama mwenyekiti wao taifa atakamatwa na kuwekwa mahabusu bila sababu? Ndesamburo anafahamika kwa umaarufu wake, ni mbunge na anao wapigakura wengi, hivi wapiga kura wake wangekaa kimya mbunge na mwajiri wao akiswekwa rumande? Hii inamaana police yetu ni mbumbumbu katika projection na anticipation? Police ingeyalinda maandamano yale kwa hali na mali kwa kulingana na taarifa za kiintelegensia walizonazo, kisha baada ya maandamano siku inayofuata ingewakamata akina Mbowe na wenzake waliokaidi amri halali ya polisi ya kusitisha maandamano, hapo wangepunguza harm na kukwepa mob psychology ya waandamanaji. Na hii inahitaji kwenda shule?

    ReplyDelete
  12. Wewe unayemshutumu Kadinali kuwa na adabu! Jenga hoja si kutusi kama ulivyocomment hapo juu. Baadhi ya comment yako ni hii nanukuhu!

    "usitake kudanganya umma kwa kisingizio cha ukadinali wako".

    Hii si kauli ya kistaarabu na umetumwa kuleta chokochoko. Mbona sisi wakristo tunamheshimu Shehe Mkuu na Mashehe wenzake wote hatuwabaguwi. Wanatoa mafunzo mema, mawaidha nk au mnadhani sisi wakristo hatuwasikilizi katika mihadhara yao? Kwa mfano mbona mpaka kesho sisi wakristo pamoja na ninyi waislamu tunamlilia sana Marehemu Shehe Gologosi! Ni kwa sababu ya mawaidha yake ya kutuunganisha kutuelimisha na kutuasa kiutu.

    Iweje leo Kadinali anapotoa maoni yake wewe umtusi kama hivyo?! Ujuwe inatuuma sana na kama nchi hii ingekuwa ya kidini nadhani kwa kauli yako leo pasingekalika Tanzania. Nenda kaulize Sudan, Afghanistan nk, mtu anapigwa mawe hadi kufa kwa kutoa maoni ya kukashifu kiongozi wa dini. Unataka tufike huko? Usilete udini katika Tanzania yetu yenye umoja.

    Tulijadili tatizo hili liishe kwa kueleza ukweli nani chanzo cha tatizo kisheria, na wajibike vipi katika tatizo hilo. Je anayosema Kadinali ya dalili ya machafuko Tanzania ni kweli au la ndipo tupate jibu la nini cha kufanya kusudi tusifike huko.

    Nakuonya tena, Chunga mkono wako, Tanzania si ya kihivyo unavyotaka tuelekee!

    By Carwin

    ReplyDelete
  13. Kweli elimu ni muhimu na elimu siyo kujua kusoma na kuanndika tu au kujua kusoma Pita kushoto au hiki ni choo cha wanaume ! elimu ni uchambuzi makini kuna watoa maoni wengine niwateja wa kahawa majadiliano yao ni ya kikahawa ! hawajui nchi hii iko wapi sasa wanafikiri udini ni tija hawajui dini ni kama chakula ulichomkuta mama yako anakula ndicho utakachokula na wewe si busara kumtukana kikwete kwa sababu tu ni muislaumu au slaa ni mkatoliki tukika kwenye mawazo kama hayo ni upuuzi mkubwa wewe ni muislaum kwa sababu fursa hiyo umeipata kwa mama yako! mimi ni mkristo kwa sababu mama yangu ni mkristo yeye , yule wale nk niupuzi kusema mwembechai pemba ,au wapi kwani serikali iliyoua pembe au mwembe chai ilikuwa yakristo tu au bila utafiti hunahaki ya kusema kitu chochote! tafute MUNGU ukiwa na elimu Kwani yeye ni NURU sio giza nene la ubaguzi Tukemee maovu bila kujali mama zetu dini zetu rangi kabila na hata maeneo Omary aliye wa Arusha ni mkristo nashanga kutaka kuandamana tena eti kaimbiwa mapambio ! elimu! elimu! Hata Mtume SWA hakuwa mjinga je iweje baadhi ya wafuasi wake wawe wajinga! wekezeni kwenye elimu sio ubaguzi ! madai yakijinga utayatambua na mtu mjinga hukimbilia udini nchi hii ni ya wote waislamu wakristo wapagani wahindu, wabudha ,washinto, watao nk DINI zote zinapinga mauaji iweje leo uwatetee polisi ni kwamba udhalimu ufisadi umepofusha watu wala hajui dhambi ni nini au koasa ni lipi nenda ubungo utakuta polisi wapo raia wapo lakini mtu anachukua anaiba mafuta kwenye lori namtu huyo anaitwa mjanja asiyefanyahayo ni kondoo au zoba! endeleeni . yatawafika Pengo kanena NENA BABA usiogope kuogopa hata YESU alisema msiwaogope wauuao mwili bali roho F Rooselvert wa marekani alisema The only thing to fear is fear itself ! \\\\\\aluta continua chochea >>>>chochea karama yake! BRAVO guru of TZ

    ReplyDelete
  14. KADINALI PENGO UMEONGEA KWELI WAACHE WANAOTOA MANENO YA KASHFA JUU YAKO HAWANA LA MAANA HAYO NDIYO MALEZI YAO YA NYUMBANI WANASHINDWA KUTOA MAONI WANAKASFU.KWANI MTU AKIKOSEA TANZANIA NDIYO ANAUWAWA NA POLISI AU ANAPELEKWA MAHAKAMANI NA NDIYO WENYE JUKUMU LA KUTOA ADHABU?

    ReplyDelete
  15. kaeni muyazungumze achenikutupiana lawama hazijengi kitu chochote bali nikuletachuki udini na ukabila namiombea kwa mwenyezi muache malumbano muishi kamazamani musilam mkrisito na asiekua nadini muishi kwpamoja naushiriano umoja ninguvu

    ReplyDelete
  16. Mawazo ya watu wote ninaafiki kwa asilimia mia moja. Wenzangu mimi nasema kuliko watu wachache waendelee kututesa NA kututesa kwa ajili ya kutaka madaraka katika nchi hii nafuu tuuwane tubaki hata mmoja ili nchi ianze utawala mpya.

    LAKINI NATAKA KUMUULIZA MHARIRI WA GAZETI HILI KUWA ANANUFAIKA VIPI NA MAONI YETU TUNAYOTOA KILA SIKU MAANA SIYONI NI KWA NAMNA GANI ANAYAFIKISHA KWA WAHUSIKA ILI WATAMBUE KUWA WANAYOYAFANYA YANAWACHUKIZA WATU WOTE!!!

    ReplyDelete
  17. Nadhani Watanzania wanasikitishwa kama Kardinali Pengo na matukio ya Arusha.Lakini Kardinali kakosea. Angesubiri hadi hapo upelelezi kamili ufanyikapo ndipo atoe maoni yake. Hapo ametoa hukumu dhidi ya polisi bila ushahidi. Wazo kwamba polisi hawajali na wanadhamiria kuwauwa raia holela si la ukweli. Ingilikuwa hivyo basi kila siku mauwaji yaliyofanywa na polisi yangekithiri. Kwa hiyo tukubali hii ni exceptional case.Kardinali angelisema anasikitishwa na maafa,angewaomba Watanzania kuishi kwa amani na kuomba upelelezi kamili kufanyika bila kulaumu upande wowote. Na akilaumu basi angelaumu pande zote mbili. Waingereza husema it takes two to tango. Yaani dansi ya tango yahitaji wawili kuicheza. Na kusema kwamba dunia imeshangaa, haya hutokea pia Ulaya, Marekani na kwingineko. Hivi juzi juzi polisi waliwashambulia wanafunzi Uingereza. Kuna maswali mengi kwa mfano je maisha ya polisi au raia wengine yalikuwa hatarini. Twasikitishwa na maafa, lakini polisi wanaweza kuleta ushahidi kwamba hatua waliyochukua ni nusu shari (the lesser evil) iliyozuia shari kubwa zaidi. Nadhani tusirukie maswala nyeti kama haya kabla ya upelelezi kamili. Kama kiongozi wa dini Kardinali anawajibika kufikiria sana anayoyasema.La sivyo, ataonekana ni mdau wa upande fulani. Matamshi yake ni ya kusikitisha.

    ReplyDelete
  18. kwanza yawafikie Maaskofu na mapadri waone wanachokitetea na kudhulumu haki za wengine,pia anayejidai na kisomo ni bure kwani nchi ilipokuwa inaendeshwa na watu wenye kisomo cha wastan ilienda vizuri lakini baada ya kuingia nyie mnaojidai na usomi wenu nchi imekorogeka,unaweza kuwa na elimu usiwe na busara wala hekima,ukatumia kisomo chako kuiba,na ndivyo mnavyofanya sasa,nyie mnao laumu na walioko serikalini ni wezi tu hata mashirika na makampuni ya nje yanaogopa kuajiri Watanzania,kisomo si tija au mmemsahau PROFESA WENU BAREGU alivyomtetea mgombea mwenza wa Mbowe? mnasema nchi miaka 50 haina maendeleo na nchi hii ilikuwa mikononi mwa wasomi. MADA NI HII:- MZEE KADINALI PENGO HUTATENDA HAKI KWA WENGINE KAMA HUTAMKEMEA PADRI SLAA NANUKUU TENA MANENO YAKE " Nawaambia polisi wawaachie haraka sana viongozi wetu waliowakamata la sivyo umati huu uliopo hapa utakuja polisi kuwatoa kwa nguvu ya umma,na kitakachotokea huko mimi nisilaumiwe" la pili baada ya mkutano akawaamuru wafuasi wake waelekee kituo cha polisi cha central ndipo balaa lilipoanza, MBONA HILI MUADHAMA HULIKEMEI? VIONGOZI WA DINI MNAHITAJI HESHIMA NA MSIPOILINDA HESHIMA HII MLIOPEWA MTAHUKUMIWA NA MUNGU HAPAHAPA DUNIANI. PADRI SLAA HAKWEPI LAWAMA HAPA.

    ReplyDelete
  19. KARDINALI PENGO NI KIONGOZI ANAYE HESHIMIKA SANA TANZANIA, AFRICA NA DUNIANI KOTE. NI MTU MNYENYEKEVU, ANAYEJITOA NA MWENYE UCHUNGU NA UHAI NA MAISHA YA MWANADAMU BILA KUJALI DINI, RANGI WALA KABILA.

    WALIOUAWA ARUSHA NI WAKRISTO NA WAISLAMU, HAJALI DINI ZAO ANAGUSWA NA JINSI AMBAVYO WALIOAMINIWA KULINDA UHAI WANAKUWA WEPESI KUTOA UHAI HUO. HUYU NI BABA, ANANIONYA MIMI, WEWE NA WAO. BILA WATU KAMA KARDINALI PENGO, NA MAREHEMU SHEKHE GOROGOSI TANZANIA ISINGEKUWA KISIWA CHA AMANI.

    ReplyDelete
  20. Nchi hii haitatawalika, bado kidogo tu hiili linakuja, wameua watu kwa sababu eti wanaviwanja wamepora na fedha kedekede, wanaogopa akiingia mtu mwingine siri itafichuka. Nasema hivi, sasa hivi hatutapigana tena sisi wanyonge. Msafala utaanza na watoto wao, wake zao na vitega uchumi vyao pamoja na vya makaburu wenzao waliowaleta hapa TANZANIA.

    ReplyDelete
  21. Nafikiri matusi dhidi ya viongozi wa kikristo sasa yamekuwa hayavumiliki, siku zinakuja hayo matusi mnayopandikiziwa na walioshindwa kuongoza nchi mtayatafuta pa kuyapeleka.

    ReplyDelete
  22. Kuna mwimbishaji kaanzisha wimbo wa udini na baadhi yetu tunafuatisha tu kuimba kwa nguvu zetu zote kama chiliku. Yeyote anayeongea sasa anatazamwa kwa mtazamo wa dini zetu, tunaelekea wapi watanzania????? Naona sasa tumeamua kuelekeza nguvu zetu zote katika ubomoaji wa taifa letu, kwa mtazamo wangu tungefanya kinyume chake yaani tujenge Taifa letu moja na hicho pekee kiwe akilini mwetu. Tusilazimishe kuona tunachotaka kuona!

    ReplyDelete
  23. Msuya Cleopa David: Sijui kwa nini tuilipe Dowans (Mwananchi paper 14/01/2011)

    MZEE MSUYA UMENENA VEMA YAFUATAYO. 1. TATIZO LA OMBWE LA UONGOZI WA TAZANIA WA RAIS KIKWETE. 2. KUTOKUWA NIA YOYOTE YA KUPIGA VITA RUSHWA KWA SERIKALI YA SASA ZAIDI YA VIONGOZI KUJINUFAISHA KIBINAFSI NA KUTETEANA WAO KIFAMILIA NA KIRAFIKI. 3. UMUHIMU WA KATIBA MPYA NA TUME YA RAIS KUSHIRIKISHA WAPINZANI (4) TUWE NA VIWANDA TANZANIA (5) FAGIO LA CHUMA LIPITE CCM KUSAFISHA NJIA (6) DOWANS KUTOSTAHILI MALIPO. YA NINI? (7) NCHI KUKOSA DIRA YA MAENDELEO (8) KIKOSEKANA VIONGOZI WAZALENDO KAMA KINA SITTA, MEAKYEMBE, NK (8) SIASA ZA NCHI KUINGILIWA WA WATU WACHAFU KAMA KINA RA,EL NK (8)UMENENA VEMA KWAMBA HUKUTAKA KULAZIMISHA WANAO KUINGIA SIASA MAANA KUWATUMIKIA WATU NI WITO. HAWA KINA JI (RZ1) WAO NI DILI. (9)WASIWASI WA AHADI HEWA ZA VIONGOZO WA CCA HASA JK, KWAMBA VIJANA WANACHUKIA SANA, SSA WAKIPATA MTU WA KUWAELIMISHA WANAGEUKA KABISA AGAINST CCM. (10) KWAMBA BADO UNA TUMAINI LA RAIS TOKA CCM (11) KWAMBA CCM IMEPOTEZA UBUNGE CONTROL YA ALL THE ECONOMIC AND POLITICAL STRATEGIC AREAS KAMA DSM, MWANZA,ARUSHA, MBEYA, IRINGA, KIGOMA, NK. NI KOSA LA KUWA NA KATIBU MKUU MPUUZI KAMA MAKAMBA NA RAIS/MWENYEKITI WA CCM MBABAISHAJI KAMA JK. PIA UONGOZI WA WAZEE WALIOISHA KAMA KINA MSEKWA, VIONGOZI WAPU-UZI KAMA KINA CHITANDA, MASHA, BURIANI NK.
    AMBACHO HUKUSEMA NI KWAMBA (1) UNAWAGANDAMIZA CHADEMA KWA SABABU TU YA UTAWALA WA SHERIA. UTAWALA WA SHERIA PIA UNARUHUSU MAANDAMANO YA AMANI. (2) ULIKUWA KIONGOZI MBAGUZI, HASA KUWABAGUA WAPARE YA KUSINI (3) ULIKUWA KINARA WA MVURUGANO KATIKA DAYOSISI YA KKKT PARE UKITAKA DAYOSISI YA MWANGA YAKO NA SAME KATIKA AGENDA YAKO YA KUWABAGUA WAPARE WA KUSINI (4) KWAMBA WAZIRI DAVID MATHAYO NI MWANAO ULIYEMZAA PARE KUSINI UKIWA OFISA UTUMISHI KULE, NDIO MAAN BARAZA LA MAWAZIRI UNALIPENDA (5) ULIJITAHIDI SANA KUMPIGA VITA WAZIRI MAGHEMBE KATIKA UBUNGE WA MWANGA ILI UPATE UHAKIKA WA MWANAO DAVID KUPATA UWAZIRI KUPITIA UPARE. (6) WEWE NI MMOJA WA VIONGOZI WAKATILI TANZANIA HII, HAIJAPATA KUTOKEA. UNANIELEWA NADHANI. (7) KASORO HIZI MUNGU AKUSAMEHE HATA WEWE NI MWANADAMU. JIPIME MWENYEWE.

    ReplyDelete
  24. Kadinali Pengo,Je kisu kimegusa mfupa ? zanzibar waliuwawa watu zaidi ya 20 na hakuna kauli ilotoka ? au sio watu wale ? kama unataka kusema haki basi sema yote sio nusu nusu.

    ReplyDelete
  25. HIVI WATANZANIA MLISHA KALILIHWA ELIMU YA UCHUNGUZI HATA KAMA UNAPIGWA KOFI NAPOLISI MBELE YA MKEO SERIKALI ITAKUAMBIA TUNAUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI MASIKINI AFRIKA POLICE WANAUWA KWA LISASI DUNIA NZIMA INAONA ETI TUNAFANYA UCHUNGUZI DU HERI UKOSE MALI UPATE ELIMU ALINIFUNDISHA BABU YANGU,MIMI SI JUI HAWA MAOFISA WA JESHI KWELI KAMA WANAMAADILI YA KAZI YANI MMEUWA HIVI HIVI MCHANA LAKINI MNAGOMA NA MAKAMBA WENU NA CHITANDA KAMAMA HAKO KANAWAAMBIA WAZEE WAVUE MAJOHO BASI WEWE VUA KACHUPI HAKO WAKAKUPAPASE POLISI.

    ReplyDelete
  26. HATUKATAI KADINALI PENGO NI MTU WA HESHIMA NA ANAHESHIMIKA TATIZO LIPO PALE PADRI SLAA ANAPOAMRISHA WATU WAVAMIE KITUO CHA POLISI NA KUONEKANA SI KOSA,HATA HUKO ULAYA KWENYE DEMOKRASIA ILIYOKOMAA NENDENI MKAJARIBU KUVAMIA KITUO CHA POLISI KAMA HAMKUONA CHA MOTO? MIMI NASEMA SI BUSARA KUWATUKANA HAO VIONGOZI WA DINI AU DINI YA MTU MWINGINE LAKINI KUNA NDUGU YANGU HAPO JUU ANAONA WANAOTUKANWA NI VIONGOZI WA DINI YA KIKRISTO TU WAKATI HATA WA KIISLAMU NA DINI YAO WANATUKANWA HUMU NA NYIE MLIOLELEWA BILA ADABU WALA HESHIMA,LAKINI KUWAKOSOA KWA ADABU NDIO SAWA KWANI WAO SI MALAIKA KUWA HAWAKOSI. NAMKUMBUSHIA MZEE KADINALI PENGO KUWA MAUAJI YA RWANDA HAYAKUWA YA WAISLAMU NA WAKRISTO,SEHEMU KUBWA ILIKUWA WAKRISTO KWA WAKRISTO KUTOKANA NA KANISA KUJIKITA UPANDE MMOJA NA KUACHA MAONGOZO YA DINI NA MATOKEO YAKE NI MAPADRI KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA,HATA HAPO KENYA KANISA LILIHUSIKA NA VURUGU ZA HAPO,HII INATOKANA NA KUTOTENDA HAKI NA KUEGEMEA UPANDE MMOJA,NI KWELI PADRI SLAA KAHUSIKA KWA SEHEMU KUBWA KWA KADHIA YA ARUSHA NA HATA MAASKOFU KULE WALISEMA CHADEMA HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA LA KADHIA HIYO.TUWE WAKWELI TUPATE KUTATUA TATIZO.

    ReplyDelete
  27. Je hatukusema? kuna mjinga mmoja anaanza na ile ya dayosisi ya pare,na hii ni ya wakristo kwa wakristo,mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi ni sumu na sasa ndiyo initafuna nchi hii.

    ReplyDelete
  28. Mhh nchi imeoza kuanzia viongozi wa siasa wa vyama vyote,wa serikali na wa dini,hapa kuna tatizo gani kubwa,serkali imezuia maandamano ni kosa.Slaa kuamrisha wafuasi wake kuvamia kituo cha polisi ni kosa,wakuu wa dini kukemea upande mmoja na kuacha upande mwingine ni kosa na watoaji maoni nao ni hovyooo kabisa

    ReplyDelete
  29. Tulipigania uhuru wa nchi yetu ili tujitawale tuondoe ukatili wa mkoloni sasa badala ya kufanyiwa ukatili na mzungu tunafanyiwa ukatili na mtu mweuzi kama sisi. Ndugu Watanzania tuwakatae hawa ccm kwa sababu wameacha maadili ya muasisi wa taifa letu wakageuka wezi, wauaji, wakoloni, mabeberu, majangili, wanyama, wahuni na Mafisadi !

    Kuliko kuendelea kutawaliwa na watu ambao ni na WAUAJI tupotayari kupambana nao hadi tufe wote. Mungu jujalie nguvu ya kuwaondoa hawa wezi serikalini ! Amen

    by Adallah Farouk

    ReplyDelete
  30. Huna wa kupambana naye mwehu wee,kapambane na umasikini kijijini kwenu mliowakimbia mama zenu huko vijijini,mmewageuza mama zenu na dada zenu matrekta na punda wa kuwalimia na kuwabebea mizigo ya kuni halafu mnalia umasikini,Kikwete yupo juu sana ya huyo mbwa wenu wala hamuwezi kumuondoa,nasi iko siku tutaamua kuingia mitaani kuwaambia enough is enough,kama tuzungumzie dowans iwe ni dowans tusichanganye mambo,PADRI WENU SLAA NI HARAMIA NA MUUAJI ALIYEDHAMIRIA KUPATA UMAARUFU KWA ROHO ZA WATU,KAMWE MZINIFU NA MWIZI WA WAKE ZA WATU HATOIONA IKULU KWA LAANA YA MUNGU

    ReplyDelete
  31. Hizi hoja za udini sasa naona zinapunguwa kupitia makala hii. Mjumbe mmoja kesha onya kuwa tuache kutukanana wala kukashifiana kwa misingi ya Dini, ukabila wala ukanda.

    Nimemwelewa vizuri kuwa sasa yule anayejaribu kutumbukiza nyongo ya Udini tusichangie mada yake, ni sahihi japo hii itaendelea kuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya Watanzania.

    Mi ninachosisitiza viongozi wa dini lazima tuwaheshimu, pamoja na viongozi wengine wote wa vyama vya siasa na serikali.

    Kama mttu anatoa maoni yake hayo ni maoni yake tumwache, lakini kama tutachukulia maoni hayo kuwa ndiyo msimamo wa CHADEMA au SERIKALI au KANISA hapo tutakosea.

    Kwa mfano Baba Askofu Kadinali Pengo anapoeleza kuwa anasikitishwa na jeshi la polisi kuuwa raia wasio na hatia, hii ni kauli pana kwa maono yake. Inawezekana alitarajia Polisi itumie weeledi wake wote kuepusha damu hata tone moja na roho za raia wa Tanzania isimwagike kama alivyozoea. Lakini ameona kipindi hiki ni tofauti hivyo amestaajabu kwa haya kutokea Tanzania. Ndiyo maana akasema kama hali hii hatutaichukulia kwa makini na kwa Watanzania kutomtanguliza Mungu ipo hatari ya machafuko makubwa kutokea mbeleni. Haya naamini kwa maoni yangu ni maoni yake na hayana mafungamano na msimamo wa kanisa japo kanisa linamsikiliza na kuheshimu maoni yake sana. Kadinali ni Binadamu mwenye nyongo kama mimi na wewe, anaumia na anapopata wasaa wa kuzungumza ndiyo anaeleza kilichopo moyoni mwake na mtazamo wake kutufaidisha wengi wetu.

    Kama Kadinali angesema IGP mpumbavu, Serikali ya Kidhalimu NK hilo lingekuwa ni tatizo kubwa. Sijuwi ni wapi alipokosea Kiongozi wa kanisa katoliki hapa Nchini. Haya yalikuwa ni maoni yake na mafundisho kwetu sisi watanzania wote. Kadinali Pengo analingana kabisa na Mabalozi waliomweka kitimoto Benard Membe kuhusu hayo hayo! Mbona Membe amekuwa mpole wakati Mabalozi wanashutumu weledi finyu wa polisi katika kushughulikia hadhara kama hii ya Arusha hata kusababisha umwagaji wa damu!

    Nao mabalozi ni Wakatoliki? Suala la kumwaga damu tusilitazame kwa jicho moja, tulitazame kwa macho mapana iwezewkanavyo!

    Binafsi sikatai kuwa CHADEMA wana la kujibu katika hili na hasa kama kweli watu mliopo Arusha siku ya maandamano mtatuthibitishia kuwa DR. Slaa aliamuru watu wakamtowe Mbowe kituo cha Polisi. katika mazingira kama haya lazima itatokea vurugu na Dr. Slaa analijuwa hili. Yeye kama Kiongozi wetu alipaswa kutuliza wanachama na wapenzi wa CHADEMA katika wakati huu mgumu. Hata kujuwa hatima ya Mbowe na wenzake. Lakini jitihada hizi lazima ziwe za kidiplomasia. Kiongozi bora ni yule anayeweza kuvumilia na kufanya maamuzi ya busara hasa katika kipindi kigumu. Ili kuepuka mifarakano inayoweza jitokeza.

    Tunawaomba Watanzania mliopo Arusha mtuthibitishie haya ili tupime nafasi ya CHADEMA katika vurugu hizo. Hatutaki hapa Udini uingie kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake mwenyewe.

    Kama kweli Dr. Slaa aliamuru hivyo, tukumbuke kwamba ndani ya CHADEMA haikutoa msimamo huo. huu ulikuwa msimamo wa DR. Slaa na si CHADEMA. Kama Dr angetulia katika kipindi hiki kigumu kwa chama pengine hizi vurugu zisingetokea. Mkitaka kuthibitisha haya angalieni jukwaa kuu pengine wakati, anatoa amri hiyo itakuwa si wote waliokaa jukwaa kuu na Wapenzi wote wa CHADEMA waliafiki, ila kwa sababu tayari imeshatolewa na kinahotafutwa ni umoja na uaminifu ndani ya Chama ilibidi wote wakurupuke kutekeleza amri/maelekezo ya mkubwa wao!!

    By Carwin 1

    ReplyDelete
  32. Hivyo nasema kwa kifupi ukiuliza sana hata CHADEMA wao hawaafiki kwenda kumtoa Mbowe polisi kwa nguvu kwani walijuwa nini kingetokea!

    Kwa Serikali tatizo ni hizi kauli tu za kujichanganya mara mfanye maandamano na vibali vimetolewa, lakini with no time maandamano yanafutwa bila kufuata sheria. Basi ni vurumai tupu kana kwamba nchi haiongozwi na sheria. Ndipo tunapofikia hapo leo hii! Lakini kama Polisi na taarifa zao za Kiinteligesia wangezifuatilia kwa makini kubaini vyanzo vya vurugu vilivyojificha ndani nyuma ya pazia la CHADEMA na kuwachukulia hatua kimya kimya mpaka maandamano yaishe hili la leo tusingefika hapa!

    Mimi naamini maoni bora yote naamini ni msimamo wa serikali lakini maoni ya kusema waache wafe wafuasi wa CHADEMA ni wakaidi yatakuwa ni maoni ya mtu binafsi hata kama mtu huyo anaheshimika namna gani ndani ya Chama na Serikali yataendelea kuwa maoni yake binafsi.

    Kikubwa ni tuta-controll vp maoni hayo yasiathiri ustawi wa jamii ndilo jambo la kulizungumza na kulitafutia mwafaka!

    Jk ameshaonesha njia, Wasira ameonesha njia, Benard Membe pia! Ni changamoto kwa serikali kuponya vidonda vya CHADEMA ili wajenge imani kwa serikali na vyommbo vyake ili kukubali kukaa meza moja ya mazungumzo kumaliza tatizo la kisiasa Tanzania.

    Hofu yangu ni kuwa Arusha imeanza na moto huu utaenea Nchi nzima. Tuwasikilize CHADEMA wana madai gani, tukubaliane mchakato wa madai hayo uwe vipi, kama ni katiba mpya au suala la umeya tushirikiane vipi na watanzania wote kwa ujumla katika kutatuwa matatizo yetu ya kisheria, utawala, uchumi siasa na demokrasia. Ili huko tunakotaka kuelekea sasa tusifike.

    Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania.

    By Carwin 2

    ReplyDelete
  33. Membe alituambia kwamba mabalozi walimkemea. Mabalozi wa kigeni mpaka sasa hawajatoa taarifa ya kushutumu serikali au kuzungumzia matukio ya Arusha. Sasa nauliza huyu Membe amekuwa spokesman wa mabalozi wa nchi za kigeni au ni spokesman wa Tanzania.Walizungumza naye kisirisiri - na kwa kawaida maana hawana uthibitisho walikuwa wanataka taarifa rasmi. Membe naona alikuwa anatafuta kisingizio ili kushutumu viongozi wenzake katika serikali ili pengine kuonyesha kwamba hakusiki.Basi kuonyesha ujasiri wake si ajiuzulu kutoka baraza la mawaziri. Unafiki mtupu.

    ReplyDelete
  34. CCM wasifikiri ndio tupo mtaani tunaimba CCM, CCM, CCM, tulisha choka. Tena choka mbaya tumewaachia vigogo na mapolisi mle kama mchwa. Sisi tutakomba makombo tuu msipate shida. Sisi tunabaki na Dr SLAA WETU NA MBOWE Wetu nyinyi tafuneni tu tutaonana 2015. Na kama mnataka ushindani haki iwepo kwa vyama vyote. Lakini ninakubali CHADEMA wako makini kuliko CHAMA CHA MAJAMBAZI.

    ReplyDelete
  35. Mtoa maoni hujamaliza kwani hao wafuasi wa chadema,wameharibu magari na mali za watu ,jiulize baada ya mkutano hao watu walikuwa wanaelekea wapi? mimi nipo kituoni hapo central nakuhakikishia kama wangesogea mpaka mita 50 tu binafsi ningemaliza magazine yangu yote kuwamaliza,mimi ni binaadamu kama wao ati ningoje wanidhuru halafu ndio maaskofu waseme,hapana kwa hilo na ninatoa onyo atakaekaribia kituo cha polisi kufanya fujo tutakula naye sahani moja

    ReplyDelete
  36. KADINALI PENGO NI MZUSHI, MUONGO NA MCHOCHEZI SANA. ANAATARISHA AMANI NCHINI NI BORA AENDE VATICAN. MARA NGAPI ANAIPONGEZA SERIKALI KWA MAUAJI DHIDI YA WANANCHI(REJEA MAANDAMANO YA WAISLAM NA MAUAJI PEMBA) WANAOJIHAMI KWA MAWE? LEO PADRI MWENZAKE KAKAMATWA AMESAHAU YALIYOPITA!
    UDINI UNAMSUMBUA KWA VILE SERIKALI YA JK IMEKATA MIRIJA YA PESA WALIYOKUWA WANAPATA TOKA HAZINA NDIO CHUKI IKAANZA. LET BE FAIR PLAY MUSLIN AND CHRISTAIN. MTAMKUMBUKA SANA NYERERE. MMEKWISHA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  37. MNATAKA NINI ZAIDI HAKUNA SABABU YA KUMLINDA PADRI SLAA NA NDESANBURO KWENYE HILO KAMA MNATAKA SULUHU YA KWELI.Katika mkutano wa hadhara wa Chadema ulioongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani.

    Kwa kauli yake, Dk. Slaa aliwataka wafuasi wake kuandamana hadi kituo kikuu cha Polisi walikokuwa wameshikiliwa viongozi wao wa kitaifa.

    “Mbali na kauli hiyo, pia Dk. Slaa alitoa kauli mbaya zaidi ya kuwa kila kijana aliyeko katika mkutano ule, apite njia yake wakutane Polisi huku akiwahadharisha wanawake wenye watoto,
    kutokwenda huko kwa kuwa kungetokea mapigano,”

    Kutokana na kauli hizo ni wazi kuwa viongozi hao walikuwa wamedhamiria na walifahamu nini kitatokea, baada ya wao kuamuru vijana na wafuasi hao kuvamia kituo cha Polisi wakiwa na mawe na silaha zingine. (TUTAMLINDA KIKWETE KWA NGUVU ZOTE NI RAIS HALALI WA NCHI HII)

    ReplyDelete
  38. Kumshambulia Muadhama Kadinali Polycap Pengo na viongozi wengine wa dini ni kukosa adabu na ni upuuzi usiovumilika. Alichosema Pengo ni kweli na kitabakia kuwa ukweli. Tatizo hapa si urais ni watu waliouawa na polisi ambao wana dhima ya kuwalinda raia. Kupenyeza udini katika suala lililo wazi ni ufinyu wa mawazo. Mhe. Pengo mimi nakupongeza na usisite kukemea kila jambo lililo ovu

    ReplyDelete
  39. NYINYI CHAMA CHA MAGAIDI NA CHAMA CHA MATAPELI ACHENI KUMZONGA NA KUMSUMBUA BABA YETU. KAMA MMEKASIRIKA MFUATENI NA GOBOLE KAMA KAWAIDA YENU NYINYI HAMKWEPI WAUWAJI WAKUBWA.

    ReplyDelete
  40. Hapa msibadili mada na siungani mkono na wanaotukana dini nyingine au kiongozi wake kama huyo mpuuzi hapo juu. Tunataka jawabu "KWA NINI PADRI SLAA NA NDESAMBURO HAWAKEMEWI KWA KATIKA KADHIA HII YA ARUSHA? HILI NDIO LA MSINGI KWETU. MALEZI YA HOVYO KWA VIJANA WETU HASA HAO WALIONGIA MJINI MIAKA YA KARIBUNI NA KUIGA MAMBO YA HOVYO NDIO YANAYOSABABISHA KUTUKANA HOVYO BILA ADABU. KADINALI PENGO ANA HESHIMA KATIKA JAMII LAKINI YEYE SI MALAIKA KUWA HAKOSEI ILA TUNAPOJADILI ALILOKOSEA TUNAPASWA KUWA WAUNGWANA,KUMLINDIA HESHIMA YAKE NA YEYE AONE KOSA LIKO WAPI,HAWA WATU WANAMTUKANA RAIS KAMA VILE NCHI HAINA SHERIA,HUYU RAIS KAAPISHWA KWA MUJIBU WA KATIBA NA SHERIA ZILIZOKO ZIWE MBAYA AU NZURI LAKINI NDIZO ZINAZOTUMIKA SASA,VIONGOZI WA DINI MNAONA HILI WALA HAMLIKEMEI NA MNAONA NI JAMBO LA KAWAIDA, NI JAMII GANI MNAYOIONGOZA? KUEGEMEA UPANDE MMOJA LEO YUPO KIKWETE NI DHAMBI KUBWA AMBAYO ITAWATAFUNA BAADAYE MTAKUJA KUBISHANIA HUYU HATUFAI KWA SABABU SI MKATOLIKI AU MLUTHERAN AU PRETESTANT AU ANGLIKAN. KADINALI NI KWELI KEMEA MAOVU LAKINI UJITENGE KUEGEMEA UPANDE MMOJA. TUJIFUNZE YA RUANDA NA MAJUZI TU KENYA HAPO

    ReplyDelete
  41. Ndiyo Kadinary Pengo, hata mimi ninaungana na wewe hata kama Polisi watadai kwamba walioandamana walikuwa wamekiuka sheria adhabu yao haikuwa kuwapiga risasi wananchi wasio nahatia. Hukumu yao haikuwa kuchukua uhai wao kwa njia ya kuwapiga risasi la hata kidogo. Ni kweli kabisa haijalishi walikuwa wamekosa kiasi gani. Wale waliokuwa kimbelembele wangeweza kukamatwa hata kesho yake na kufunguliwa mashitaka ya kuandamana bila kibali. Na sasa wameuwa Polisi wamejichukulia sheria mkononi badala ya kuwapeleka wahalifu mahakamani. Hapa ni lazima sheria ichukue mkondo wake. Hata kama haitakuwa leo au kesho lakini ni lazima waliomwaga damu ya watanzania wawajibishe wapewe haki ya malipo ya kumwaga damu za binadamu wenzao kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali. Ni wazi kabisa mauaji haya yalipangwa ili kuwapa hofu watanzania wanaounga mkono upinzani. Na hasa kwa kipindi hiki ambacho mafisadi wanataka kuchota fedha za watanzania kupitia Dowasons campuni feki. Wanajua wasipoua wananchi wataandamana kupinga malipo hayo hewa. Watanzania tusikubali hata kidogo ni bora watumalize sote tuishe. Kuliko kuendelea kutawaliwa na watu ambao ni makatili wa kutisha. Tulipigania uhuru wa nchi yetu ili tujitawale tuondoe ukatili wa mkoloni sasa badala ya kufanyiwa ukatili na mzungu tunafanyiwa ukatili na mtu mweuzi kama sisi. Jamani ukatili hauna rangi ndugu roho mbaya iko kwa wote tuwakatae hawa CCM kwa sababu wameacha maadili ya muasisi wa taifa letu.

    ReplyDelete
  42. HUJAKOSEA KUSEMA MAUAJI YALIPANGWA ILA UMEKOSEA KUSEMA ILI KUWATISHA WATANZANIA KWA HILO HAPANA YALIPANGWA ILI WATU WAPOTEZE MAISHA YAO KWA KUJIPATIA UMAARUFU NA MTAJI WA KISIASA NAO KINA SLAA NA GENGE LAKE LA WACHAGA IKO SIKU WATAFIKISHWA MBELE YA HAKI----MNATAKA NINI ZAIDI HAKUNA SABABU YA KUMLINDA PADRI SLAA NA NDESANBURO KWENYE HILO KAMA MNATAKA SULUHU YA KWELI.Katika mkutano wa hadhara wa Chadema ulioongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani.

    Kwa kauli yake, Dk. Slaa aliwataka wafuasi wake kuandamana hadi kituo kikuu cha Polisi walikokuwa wameshikiliwa viongozi wao wa kitaifa.

    “Mbali na kauli hiyo, pia Dk. Slaa alitoa kauli mbaya zaidi ya kuwa kila kijana aliyeko katika mkutano ule, apite njia yake wakutane Polisi huku akiwahadharisha wanawake wenye watoto,
    kutokwenda huko kwa kuwa kungetokea mapigano,”

    Kutokana na kauli hizo ni wazi kuwa viongozi hao walikuwa wamedhamiria na walifahamu nini kitatokea, baada ya wao kuamuru vijana na wafuasi hao kuvamia kituo cha Polisi wakiwa na mawe na silaha zingine. (TUTAMLINDA KIKWETE KWA NGUVU ZOTE NI RAIS HALALI WA NCHI HII)

    Tunawaambia tena Kikwete ni Rais wa nchi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi,haondolewi na makanisa wala wahuni.

    TUNAMHESHIMU MUADHAMA KADINALI PENGO NA TUNAWATAKA WATU WANAOMKOSOA WASIMVUNJIE HESHIMA NI VEMA TUSIWAIGE WAPUMBAVU WANAOTUKANA VIONGOZI WA DINI NA VIONGOZI WA SERIKALI KWA UNAZI WAO WA KISIASA.

    ReplyDelete
  43. Pengo na madhalimu wengine wa Kanisa wote [Neno Baya] WANAFIKI. Mnatakiwa muwashukuru Polisi kwa kuepusha mauaji zaidi kwa uvamizi wenu wa kituo cha Polisi.

    CUF na wanachama wake walipouawa mliyabariki mauaji na kuona ni sawa. Mwembe Chai walipouawa waislamu tena kwa kufuatwa mliyabariki mauaji na kuona sawa. CUF walipotaka tume ya mauaji ya wafuasi yao na waislamu walipotaka tume ya wafuasi wao, nyote mlikuwa mbele kukemea na kushinikiza Serikali na hatimaye madai yote yakapuuzwa! Leo mnapiga kelele kwa watu watatu tu! Walikuwa ni wavamizi kwa maneno ya uchochezi wa Padri wenu Slaa. Nyinyi na Padri wenu ndio mnaostahili lawama zote. Nawashauri Polisi kuwa WAVAMIZI hao wakijaribu kuvamia tena ueni zaidi.

    ReplyDelete
  44. Jamani tuache matusi hayana maana hapa zaidi ya kupalilia chuki.mimi bado namganda Dr Slaa na Ndesamburo ndio wabanwe kwa kusababisha mauaji,hapa hapana suluhu bila ya kuwahusisha hawa.HAKI HAIJI KWA KUANGALIA UPANDE MMOJA. LEO TUNAANZA KUYAKUMBUKA YA NYUMA KUTOKANA NA HAKI KUTOTENDEKA SOMA HILI TAMKO LA VIONGOZI WA KIISLAM:- TAMKO LA VIONGOZI WA KIISLAMU
    Alisema mfano mzuri ni tukio la hivi karibuni la mauaji ya Arusha, ambapo maaskofu walijitokeza na kutoa tamko la kulaani mauaji hayo, wakati yapo mauaji ambayo yamekuwa yakifanywa na polisi na wao kukaa kimya.

    “Hivi sasa hatulali kutokana na mauaji ya Arusha lakini wapo watu waliuawa Micheweni, Pemba mwaka 2001, lakini hakuna aliyelaani mauaji hayo.

    Polisi walifanya mauaji mengine Msikiti wa Mwembechai, lakini hilo nalo lilifumbiwa macho … leo ni kipi cha ajabu kilichotokea Arusha hadi iwe hatulali?” alihoji.( jamani ni vyema kuangalia haki,ni kweli watu wamekufa inasikitisha lakini kama huyu Slaa na Ndesamburo hawakuwaambia wafuasi wao waende kituo cha polisi kuwatoa watu wao kwa nguvu ya uma kama vile nchi haina sheria HAYA YANGETOKEA? kama wangekwenda wao wawili na kuwawekea dhamana haya yangetokea? kuweni wakweli hii ni nchi yetu sote tunapotaka kurekebisha kitu lazima tuangalie pande zote za shilingi,bila shaka pasingekuwa na malumbano haya ambayo ni ya kijinga na yasiyo na tija kwa nchi hii nadhani wengine ni wavuta bangi maadhali anajua kutumia internet huamua kuandika chochote,tujenge heshima kwa viongozi wa dini na wa serikali kwani hata kama hamtaki Kikwete ni Rais.

    ReplyDelete
  45. Hivi mbona nyinyi waislamu mnapenda kuwafuatafuata sana wakristo? Kwa ushauri wangu hao wazee wa kiislamu waliokaa jana wangechukua majembe wakalime. Walichoongea hatukuelewa kama walikuwa na lengo la uchochezi au wanamshtaki nani. Sasa mmeshatoa tamko lenu na msimamo wenu ya kwamba mapolisi wafyeke wakristo wote kwa sababu hawataki kuifajilia CUF. Wewe unataka amani, amani ya namna gani. Sasa ujue jinsi mlivyo watu wa ajabu eti serikali isiruhusu dini kuingilia mambo ya serikali wakati mnatoa tamko la pamoja. Ujue jinsi mnavyojichanganya kama ugali na maharagwe mnakataza na bado mnajadili katiba. Kaeni kimya basi hamuoni mnaingilia mambo ya serikali wakati mnasubiri serikali iwa pangie. Sasa tuwaelewe vipi?

    Sijawahi kusikia hata siku moja kiongozi wa kikirsto anashambuliana na waislamu nyinyi waislamu mnaagenda gani na wakristo? Wakrito wako kimya nyinyi mnakwenda kuwajadili, mnawajadili kama nani? Chukueni hatua basi kama kimewauma sana Baba Kardinali Pengo alivyoongea nendeni mkamshitaki. Huyo Yahaya wenu hajatuma mijitu yake ikatabiri. Halafu mnauliza sijui mauaji ya Zanzibar na mwembe chai mnauliza serikali au mnauliza wakristo kwani wakristo ndio waliwaua. Kwani hakuna mahakama nendeni mahakamani mkaulize huko.

    Fungueni hayo mabomu yenu kiunoni kwanza na hao wenye tabia kama za akina yahaya wasali na kumtumainia mungu mmoja atawapa jibu. Na mtajisikia kuishi kwa amani rohoni mwenu.

    ReplyDelete
  46. Watanzania msichezee shilingi chooni. Hivi mkianza zuga pale manzese, kigogo, unga limited nk ambapo kila nyumba kwa asilimia kubwa kuna mkristu na mwislam mtafika wapi?
    Vyama vyote tanzania ni wezi na mjizi acheni kuchanganya dini wote kwa Mungu tutafika kwa upendo wetu si kuiba madini ya taifa.Halafu ninyi mnaotoa maoni wengi wenu punguani. Mnafikiri tukianza vita mtaenda somalia au afganisatgani, acheni hizo, limeni ndugu zangu.

    ReplyDelete
  47. Kweli bado tuna safari ndefu,wajinga nchi hii ni wengi hebu someni ya huyo mtu wa pili juu anaropoka tu hajui anachokisema.

    ReplyDelete
  48. DINI IKIINGILIA SERIKALI NA SIASA NDIPO INAPOJIKUTA PABAYA. SLAA ANA MAKOSA YAKE NA POLISI KAMA HAWAKUWA PROVOKED AU KISINGIZIO NI SELF DEFENSE? KADINALI ACHA TU WEWE ULISHATOA TAMKO KWA MAKABRASHA KUWA LAZIMA 2010 NA 2015 RAIS AWE MKRISTO SASA SLAA KAKOSA MUACHE AJARIBU TENA 2015, KABLA YA MZEE RUKSA 1985 MKRISTO AMETAWALA TANZANIA YA MUUNGANO MIAKA 1966-1985, MKRISTO AMETAWALA TENA 1995-2005 IMEKUWA KIOJA KUTAWALA JK! ACHENI KULITIA KANISA AIBU KANISA LAZIMA LITIZAME HAKI IKO WAPI SIO LIKAE UPANDE MMOJA WA DINI, WAKATI BABA YENU WA TAIFA ALISHASEMA SERIKALI TA TANZANIA HAINA DINI!

    ReplyDelete
  49. padri slaa anasema anatayarisha mkanda wa video ili kuonyesha polisi walivyo chakachua ukweli,ama kweli huyu padri kachanganyikiwa kwa kukosa urais.sasa amegeuka mzee small anatengeneza mkanda wa kukidhi haja yake ili awadanganye kondoo wake,hivi kweli wewe padri unaweza kutengeneza mkanda utakao kuonyesha makosa yako? nenda kajiunge na wasanii kina anti ezekieli na original comedy wakuvishe shanga na wigi pengine ndio fani yako. HATA UFANYEJE WEWE NA NDESAMBURO MNA HATIA YA KUCHOCHEA WATU WAVAMIE KITUO CHA POLISI WATOE WATUHUMIWA

    ReplyDelete
  50. watanzania sasa tufanye kama tunisia tuiondoa ccm kwa maandamano kupinga udhalimu wao.. ufisadi, umeme,shida za walimu,ajira hakuna,madini yananufaisha waliomadrakani, watanzania tusidanganywe na kuwa hii ni nchi ya amani! amani wapi hali wengine wanafaidi nchi, matajiri wachache, wengi wetu ni hohe hahe, tunadanganywa na hii ni nchi ya amani!!!YALIFANYIKA TUNISIA HATA SISI TUNAWEZA!!!

    ReplyDelete
  51. padre Slaa mwenyekekiti wa chadema ni mwehu na ni dalili ya fitna katika historia ya Tanzania kwa hivyo watu wanatakiwa kumuepuka la sivyo watakuja juta baadae. Vilevile yuko wapi msajili wa vyama vya siasa Tanzania,Chadema ni chama cha kidini kwa nini kinaruhurisiwa kuendeleza shughuli za kisiasa kama kingelikuwa cha kiislamu basi zamani tu kishafungiwa na viongozi wake wapo ndani.padre slaa,mtikila,cadinali pengo wote ni wachafuzi wa amani na hawafai kuwa viongozi wa jammii iliostarabika kama tanzania.

    ReplyDelete
  52. huyo anayesema tuna matajiri wachache nchi hii anajua kuwa mkwewe mbowe ni mmoja kati ya hao matajiri? hivi kuna kosa kuwa tajiri? mbowe huyo anamiliki bilicanas nyumba nhc ya umma kaipata kwa urahisi kabisa,wewe unaweza? kakopeshwa mamilioni na nssf wewe unaweza kupewa? acheni ujinga nchi intafunwa na wajanja wengi tu

    ReplyDelete
  53. WATANZANIA HAMWEZI KUFANYA KITU DHIDI YA NGUVU ZA DOLA, TUMEZOEA KUINGIA VILABUNI SAA SITA MCHANA TUNABUGIA SERENGETI, TUSKER NA KILMANJARO HAYO YANAYOTUTOSHA WAKATI SERIKALI ZA AKINA CCM, CHADEMA, CUF,NA MATAIFA YA MAGHARIBI NJAMA YAO MOJA WAKIWA MADARAKANI KUFISIDI KUPORA NCHI KIUCHUMI NA KIAKILI (BRAIN DRAIN KATIKA DIASPORA)TUNISI WALE WATU WANA UMOJA HAPANA CHA KABILA WALA DINI PALE, WALE WARBU WOTE WAMECHANGANYIKA WAISLAMU NA WAKRISTO KUMUONDOA BEN ALI KWA KUWA ANAFISIDI NCHI! VIONGOZI WA DINI WAKAE MAKANISANI NA MISIKITINI WAWAACHE VIJANA WAKISASA WENYE NGUVU NA IMANI MPYA WAFANYE MIPANGO YAO BILA KUMWAGA DAMU!

    ReplyDelete
  54. Mawazo ya wadau wengine yamejaa chuki binafsi. Inabidi tutoe mawazo ya kujenga badala ya kubomoa,kuhukumu sana hakusaidii, jaribu kuona urudishe vp imani ya watanzania ambao wengi wamekataa tamaa. tuwe makini kwa hilo na Mungu atuongoze. Amin!!!

    ReplyDelete
  55. sasa tz amani iko wapi? sasa waisalamu munataka kumua mwadhama? ha ha ha ha sasa mulizoea kuua kule shauritanga sasa munachezea pabaya. muchoka kuua kule sudan Libia na kwingine kote munakofanya vita mujuwe vita hivyomfanyavyo vitakuwa juu ya vichwa vyenu daima. oneni viganja vyenu vimejaa damu munaua hadi america hamuna haya nyinyi dini za upanga kama shetani, lakini hata hivyosishagai kwani kuua kwenu ni kawaida imekuwa ni heri dunia iongeze bara moja kwaajiri ya waislamu ili kwauwane wenyewe kwa wenyewe. mtakufa kama wanyama na kuua kwenu huko sasa hamuoni baba yenu sadamu husein sasa he nakule Egpto je? hamuoni au hamuelewi hamuna aibu kila kunako vita ni mkono wakiislamu dunia imewachoka heri mujikusanye sehemu moja ili muuane wenyewe. ni vema zaidi

    ReplyDelete