17 January 2011

Ivory Coast, Congo kucheza fainali za Dunia Mexico

KIGALI, Rwanda

MABAO mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na Diarrasouba Drissa na Kouassi Evrard, yaliiwezesha Ivory Coast kukata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia la vijana wenye miaka chini ya 17.Katika mechi nyingine ya
Kundi B iliyopigwa kwenye Uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi, timu ya Congo nayo iliungana na Ivory Coast baada ya kuichapa Mali mabao 2-1 na kukamilisha timu zitakazocheza nusu fainali ya vijana wenye miaka chini ya 17 ya Afrika na kukata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za vijana wenye miaka hiyo.

Mexico itakuwa mwenye wa fainali za U-17, zitakazofanyika Juni 2011.Tembo hao wadogo 'Elephants na Nge watoto' waliokuwa wakicheza kwenye Uwanja wa Kigali, hawakufanya makosa katika mchezo huo.

Lakini ilikuwa Tembo wadogo waliopata bao la kwanza, lililofungwa na Drissa dakika ya 12 na kuifanya timu yao iongoze. Ivory Coast walipata bao la pili kupitia kwa Kouassi, dakika moja kabla ya mapumziko katika mechi iliyochezeshwa na mwamuzi kutoka  Angola, Martins Helder.

Bao la tatu la Ivory Coast lilifungwa na Lago Lionel na kuiweka timu yake katika hali nzuri ya kwenda nchini Mexico. Beki Sabally Adama, aliifungia Gambia bao, lakini beki wa timu hiyo Adama, aliunawa mpira ndani ya eneo la penalti na mwamuzi alimtoa nje kwa kadi nyekundu.

Bedi Guy Stephane aliifungia timu yake kwa mkwaju wa penalti na bao la nne liliwekwa kimiani na Guy Stephane.

Kwa ushindi huo, Ivory Coast itacheza na wenyeji Rwanda katika mechi ya nusu fainali ya michuano vijana ya Afrika wenye miaka chini ya 17.

Katika Uwanja wa Umuganda, Congo iliifunga Mali mabao 2-1 na kushika nafasi ta pili katika kundi lao.Congo walipata bao la kwanza dakika ya 50, lililofungwa na Christ Nkoukou na bao la pili liliwekwa kimiana dakika ya 55, kupitia kwa Stevy Epaku. Mali ilipata bao lake kupitia kwa Malick Berthe dakika ya 85.

Nusu fainali ya kwanza itachezwa kesho kwenye Uwanja wa Amahoro, kati ya mshindi wa Kundi A, Burkina Faso na Congo. Jumatano wenyeji Rwanda waliomaliza wakiwa wa pili katika Kundi A, wataumana na Ivory Coast waliokuwa wa kwanza katika Kundi B kwenye Uwanja wa Amahoro.

No comments:

Post a Comment