06 December 2010

Wenger amvulia kofia Nasri

LONDON,England

KOCHA Arsene Wenger amemwagia sifa mchezaji wake Samir Nasri kwa mabao aliyoifungia na kuifanya timu hiyo ikwee kileleni mwa Ligi Kuu na kuifanya tena iingie katika mbio za kuwani taji la michuano hiyo.Nasri juzi alipachika bao lake la 10 na 11 msimu huu na kuifanya timu
hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao  Fulham.
Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa  Emirates uliifanya Gunners ikalie usukani huo na  Wenger anadai kufurahishwa na mchango uliotolewa na Mfaransa huyo mwenzake.

"Ni mchanganyiko wa kugusa, akili, vipaji maalum na umakini vile vile," alisema wakati akizungumzia mabao hayo ya Nasri.

Alihitaji kuwa na subira ya kumaliza nafasi hizo mbili na ninafuraha sana kwa sababu ulikuwa ni mchezo ambao ni muhimu tangu mwanzo,"aliongeza na akasema kuwa mchezaji huyo kwa sasa amekuwa na uwezo zaidi kutokana na kuwa anaweza kurudi nyuma  bila ya mpira na akapanda mbele baada ya kuchukua mpira.

No comments:

Post a Comment