Na Elizabeth Mayemba
WACHEZAJI wa kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi, Patrick Ochan na Joseph Owino kesho hawatacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Akizungumza
Dar es Salaam jana Meneja wa timu hiyo, Innocent Njovu alisema katika mchezo huo watawakosa wachezaji hao kwasababu wanatarajiwa kutua nchini keshokutwa.
"Tutacheza mchezo huo bila nyota wetu wa kimataifa Okwi, Ochan na Owino lakini tunawahakikishia mashabiki wetu kuwa tutashinda mchezo huo," alisema Njovu.
Alisema wachezaji waliopo wanatosha kuisambaratisha timu hiyo kutoka Kenya, kutokana na mazoezi makali ambayo Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri, amekuwa akiwapa wachezaji wake mazoezi makali.
Njovu alisema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, kwani mashabiki wao watakuwa na shauku kubwa ya kuiona timu yao.
No comments:
Post a Comment