Na Shaban Mbegu
BAADA ya kufanikiwa kufunga bao katika mechi waliyoibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya AFC Leopards, mshambuliji mpya wa timu ya Simba, Ally Ahmed 'Shiboli', ametamba kuwa, huo ni mwanzo mzuri kwake.Shiboli amesajiliwa na
mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara akitokea katika timu ya KMKM ya visiwani zanzibar, wakati wa usajili wa dirisha dogo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Shiboli alisema amefarijika baada ya kufanikiwa kufunga bao hilo katika mchezo wake wa kwanza akiwa amevaa jezi ya timu yake mpya.
Alisema bao hilo limekuwa kama ni zawadi kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wao wao, waliacha kusherehekea sikukuu ya Krismasi na familia zao na kwenda uwanjani kuangalia mchezo huo.
"Huu ni mwanzo mzuri kwangu, na kufanikiwa kufunga bao dakika za mwanzo ni dalili nzuri, natumaini nitaisaidia Simba katika kutetea ubingwa wake," alisema.
Aliwashukuru wachezaji wenzake kwa kupata ushirikiano na kuahidi kujituma zaidi ili kuzidi kufanya vizuri katika timu hiyo.Mchezaji huyo na Mbwana Samatta, ambaye ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuichezea timu hiyo, waliifungia timu hiyo mabao mawili yaliyoipa ushindi.
No comments:
Post a Comment