Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya sh. milioni 24 zimepatikana katika maonesho ya mavazi ya Red Ribbon 2010 yaliyofanyika kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununua gari la watoto yatima wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, Tanzania Mitindo House (TMH).Fedha
hizo zimetokana na mnada wa vitu mbalimbali na maonesho ya mavazi yaliyoandaliwa na Mwenyekiti wa TMH, Khadija Mwanamboka kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo ya mavazi yaliwashirikisha wana-mitindo nyota nchini akiwemo Flaviana Matata ambaye alisafiri kutoka Marekani kuja kuendesha mnada huo ambao ulidhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania na Redd's.
Katika Mnada huo, Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji alichangia sh. milioni 7, na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, Tanga Januari Makamba alitoa sh. milioni 3.
Pia, Vodacom Foundation walitoa sh. milioni 5, Miss Tanga ambaye pia aliwahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania, Sophia Byanaku alitoa sh. milioni 1.6 na mtangazaji wa kituo cha redio cha Choice FM alitoa sh. 800,000.
Pia, kulikuwa na wadau wengine wa masuala ya maonesho ya mavazi ambao walichangia katika mnada huo na kufanikisha kupata fedha hizo.Mwenyekiti wa TMH, Khadija Mwanamboka, aliwashukuru wote waliotoa michango yao na kuahidi kutumia fedha hizo kwa kusudio hilo.
"Fani ya mitindo nchini inazidi kukua na ni jukumu letu kusaidia jamii, TMH inamiliki kituo hicho kilichopo Magomeni Mikumi, mpaka sasa kina jumla ya watoto 10. Natoa shukrani za dhati kwa Flaviana ambaye amesafiri kutoka Marekani kwa ajili ya shuguli hii, huyu ni Balozi wetu wa TMH," alisema.
Aliwataja wanamitindo walioshiriki maonesho hayo ni Mustafa Hassanali, Jamila Swai, Farha Sultan, Martin Kadinda, Subira Wahure na Binti Afrika.
Wengine ni Bianca Timoth, Zamda George, Franko Designs, Paka Wear, Gabriel Mollel, Manju Msita, Diana Magesa, Kim Dean na Khadija.Wadhamini wengine wa Red Ribbon 2010 ni View Media, Benchmarks Production, KCI, MJ Records, Double Tree By Hilton na Clouds Entertainment.
Kampuni ya Mohammed Enterparises Tanzania Limited (MeTL), EFFCO TANZANIA LTD, Azania Bank Limited, Uhuru One, Women in Power, BancABC, Summer Trends, Amina Designs, Ffron Line Management na Vijana Zaidi.
Dr. David Zakaria, Fiderine Iranga, Rehema Samo, Jenifa Pemba, Joket Mwegeleo, Mariam Khamis, Masha Seif, Nafisa Abbakar, Belina Mgeni na 8020 Fashions.
No comments:
Post a Comment