27 December 2010

M'kiti aliyechomewa nyumba achangia mil 16/-

Na Heckton Chuwa, Moshi

JUMLA ya shilingi milioni 16.25 zimekusanywa kumsaidia Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi mkoani Kilimanjaro, Bw. Andrea Lekule, aliyechomewa nyumba yake na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa
kuamkia Desemba 18, mwaka huu.

Hayo yako katika taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro na ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Taifa, Bw. Agustine Mrema ambaye ametoa wito kwa watu wenye mapenzi mema wajitolee kumsaidia kiongozi huyo.
Janga lililompata Bw. Lekule ni la kitaifa na hii inatokana na yeye kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo viovu kama vile uvutaji bangi, utengenezaji na unywaji wa pombe haramu ya gongo na pia ujambazi,รข€ alisema.

Katika taarifa hiyo ambayo nakala zake zimepelekwa kwa viongozi wa kidini na serikali wa ngazi mbalimbali, Bw. Mrema alisema kuwa mkasa huo umemuacha Bw. Lekule akiwa hana makazi, mavazi wala chakula na kwamba anahitaji misaada mikubwa ya kijamii.

Bw. Mrema alisema katika janga hilo, Bw. Lekule alimpoteza mke wake, Catherine Lekule (45), binti yake Flora Lekule, (6) na kwamba nyumba ya kakake aitwae Michael Lekule, nayo iliteketezwa kwa moto huo.
Bw. Mrema alitoa wito kwa wananchi kutokatishwa tamaa na mkasa huo na kwamba waendeleze juhudi za kupambana na maovu katika maeneo yao.

4 comments:

  1. HIZI NIFUJO ZA AUGUSTINE MREMA.....MREMA ACHA UPUMBAVU WA KUWALAZIMISHA RAIA WEMA WAJIINGIZE KWENYE MATATIZO YASIO NA TIJA KWAO....UMEANZA CHOKOCHOKO ZAKO....POLISI WAPO WANANCHI TUNALIPAKODI IWEJE WEWE UNAWASHAWISHI RAIA WAFANYE ULINZI SHIRIKISHI USIKU WAKATI HAWANA SILAHA?..KAMA JESHI LA POLISI LIMESHINDWA KUFANYA KAZI ZAKE PELEKA MAPENDEKEZO BUNGE KIKWETE ALIVUNJE KAMA AMIRI JESHI MKUU...ACHA KIZABINAZABINA...ONA SASA BWANA LEKULE AMEPATA PIGO AMBALO HATALISAHAU...MICHANGO ITMRUDISHIA MKE NA MTOTO...?NA WEWE JITOKEZE KWENYE HUO ULINZI SHIRIKISHI...UNAVUTA SHUKA WAKATI KUMECHA..?

    ReplyDelete
  2. Mzee wa masifa ya kijinga! Si ndiye huyu Mrema aliyekuwa anataka gongo ihalalishwe ili wanannji wa kipato cha chini wasiokuwa na uwezo wa bia wapate kuburudika? Sasa anatafuta njia ya kujichotea tena umaarufu....wabongo wa leo siyo wa enzi zile mzee wa kiraracha acha ulofa! Tulia kamata posho zako kipindi hiki cha lala salama

    ReplyDelete
  3. Pole sana Bw. Andrea Lekule kwa hayo yote yaliyokupata, mungu yuko nawe japokuwa kuwa na hali ya mwanzo ni vigumu.


    Wanaomsakama Mrema acheni kumpakazia mzee wa watu. Wala hana niambaya na usalama wa watanzania. Mimi ninadhani wewe unaesema kuhusu ulinzi shirikishi mimi sioni tatizo lolote kwake. Vijana wangi wanaaribika kwa kuiga mambo ambayo sio mazuri.


    Kwa sasa kuna mambo mengi yanaisuta Tanzania ambayo yanaharibu vijana wetu. Huwezi kumwandama kwa sababu eti wewe hutaki ulinzi tuache vijana wetu waharibike tuu kwa ajili yako ambaye unampiga vita Mrema tafuta points nyingine hapo umechemsha.

    Mbona huko Mwanza, kagera, nk wanauwana ni kwa ajili ya Mrema. Wewe unalako la chuki binafsi.

    Kwani hao polisi hawawajui wanaouza gongo, wanawajua sana lakini rushwa imezidi. Wewe subiri polisi aje aendeshe familia yako, na nyinyi ndio ambao watoto wenu wanawashinda mnakosa rizki. Kaza butu MREMA.

    Babu yetu Mrema kaza buti wanusuru vijana wetu wasiingie kwenye majanga ya ajabu. Hawa wanaokupiga vita ndio kila kukicha mchaga kapanda, mchaga kashuka. Hawana lolote baadae kukashifu, mchaga kapendelewa. Sisi tuko nyuma yako babaaaaaaaa.....

    ReplyDelete
  4. Yaani kuna watu wapumbavu kweli. Yaani Mrema kusaidia kuokoa jahazi la wizi, na ulevi kupindukia mnamsakama. Kweli watanzania hatuna shukrani. Hio gongo ni nzuri sana nini wewe unaesema anatafuta mijisifa. Basi wewe una kiwanda cha kuzalisha.

    ReplyDelete