27 December 2010

Ghasia aagiza anayeambukiza Ukimwi abanwe

Na Martha Fataely, Moshi

MWENYEKITI wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya taifa ya takwimu ameagizwa kumchukulia hatua za kisheria mtumishi mmoja ambaye anadaiwa kuwaambukiza Ukimwi kwa makusudi watumishi wa taasisi hiyo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejment ya Utumishi, Bi. Hawa Ghasia alitoa agizo hilo katika ufunguzi wa kikao cha tatu cha wafanyakazi wa ofisi ya takwimu ya taifa ikiwa ni baada ya kupata taarifa za mtumishi huyo. Kutokana na malalamiko ya watumishi wengi na ukweli wa mambo yenyewe, namuachia mwenyekiti wa baraza wenu alishughulikie haraka iwezekanavyo ili kunusuru nguvu kazi ya taifa isiendelee kuteketea na ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Waziri Ghasia alisema amepokea malalamiko mengi juu ya tabia mbaya za mtumishi huyo ambaye inasemekana kutokana na uwezo wa kifedha alionao amekuwa akiwarubuni wasichana wafanye naye mapenzi huku akijua ni muathirika.
Hii sio tabia ya kiungwana lakini kwa kuwa kuna sheria za nchi ambazo zinaelekeza cha kufanya kwa watu kama hawa, hakuna haja ya kumfumbia macho, kwani huu ni mchezo mbaya,” alisema.
 
Alisema ni vyema kwa mwenyekiti huyo Dkt. Albina Chuwa kutomuonea haya mtumishi huyo kwa kuwa taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi na wazazi wametumia fedha nyingi kuwaelimisha watoto wao.

5 comments:

  1. Mh Kidume huyo hataki kufa peke yake! Na hao wasichana wajinga kwani hawawezi kukataa! hata kama ana mapesa!

    ReplyDelete
  2. Ohoo wengine tuna ndugu zetu katika taasisi hiyo isije chain ikawakumba,achukuliwe hatua faster huyo Mwanahizaya

    ReplyDelete
  3. jamani huyo anajulikana wapo wasiojulikana cha msingi watu ni kupima afya zao mapema ili wajilinde na maambuzi.

    ReplyDelete
  4. hao wanoambukizwa mbona hamuwasemi? wanatembeaje na mtu asiyekuwa mume au mke wao. tamaa hupelekea mauti, ndivyo visemavyo vitabu vitakatifu. anejua kama huyo mtu mgonjwa, mbona kamuacha afanye anavyotaka, na kwanza mmejuaje? na yeye je, aliyemuambukiza mbona hamumsemi? wakati mwingine kuna kabusara kwenye maneno ya mheshimiwa, pale aliposema wenye viherehere......

    ReplyDelete
  5. Kwani anawabaka? kwa nini wenyewe wanakubali?

    ReplyDelete