Na Mwali Ibrahim
PROMOTA wa pambano la Francis Cheka na Mada Maugo, Kaike Siraju amewashupalia mabondia hao kwa kuwataka kuzidunda katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kama ilivyopangwa.Pambano hilo la fungua mwaka litakua la uzito wa kg. 72 ambapo, Cheka
atautoa mkanda wake wa ubingwa wa UBO ili ushindaniwe katika pambano hilo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaike alisema maandalizi kwa ajili ya pambano hilo, yanaendelea na litachezwa katika uwanja huo kama alivyopanga kwa kuwa wadhamini wake ndiyo waliopendekeza."Pambano litapiganiwa Jamhuri na si PTA kama anavyotaka Maugo na tayari nimeshaongea naye na tumekubaliana hivyo, tunaendelea na taratibu nyingine za maandalizi," alisema Kaike.
Alisema, leo anatarajia kuwakutanisha mabondia wote wawili katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari kwa ajili ya kuzungumzia pambano hilo, pamoja na kuwatambulisha.
No comments:
Post a Comment