ROME, Italia
KOCHA wa Klabu ya soka ya Internazionale Milan, Rafael Benitez anaamini kuwa timu yake inaweza kutwaa ubingwa wa Serie A na Klabu Bingwa ya Dunia katika msimu wake wa kwanza.Benitez anafurahishwa na uchezaji wa sasa wa timu yake, baada kufanya vibaya katika
mechi zilizopita na kuzua uvumi kuwa anaweza kutemwa na Rais wa timu, Massimo Moratti.
Alipoulizwa kuhusu maendeleo ya timu baada ya miezi sita, alisema inazidi kuimarika na kuongeza kuwa tatizo walilonalo ni kuwa na majeruhi na kwamba watakapopona kila kitu kitakuwa sawa."Ninafurahia jitihada ambazo timu imefanya katika mechi mbili zilizopita. Ninajivunia wachezaji waliopo katika kipindi hiki.Alisema anatumaini kufanya vizuri katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia kwa kuwa kuna wachezaji wazoefu waliokwisha kushiriki mashindano hayo.
Mashindano hayo hukutanisha klabu bingwa za mabara yote, ambapo Benitez alisema kuwa wachezaji ni muhimu katika kupata ushindi na si kocha peke yake."Ninaamini kuwa tunaweza kutwaa makombe mengine na hata Scudetto."Mwanzoni mwa msimu kila mmoja alikuwepo na tulicheza soka nzuri. Wachezaji wengi wazuri waliocheza vizuri mwaka jana waliokuwepo sasa ni Julio Cesar, Maicon, Diego Milito, Thiago Motta ambao watarejea."
Mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia yanatarajiwa kuanza Desemba 12 mjini Doha, Falme za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment