*Mosha atangaza kukaa pembeni
Na Elizabeth Mayemba
MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Davis Mosha amesema ameamua kujiweka pembeni na hatojishughulisha na jambo lolote ndani ya klabu hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mosha alisema kwa nia nzuri kabisa anaamua kujiweka pembeni na uongozi huo na kuwaachia Mwenyekiti wake na viongozi wengine, ili waendeleze jahazi hilo.
"Naona kila siku mambo ndani ya Yanga hayaendi vizuri, juzi Mwenyekiti wangu ametufunga midomo tusiongee lolote, hivyo sioni umuhimu wowote wa mimi kufanya chochote ndani ya Yanga, ngoja nijiweke pembeni wakinihitaji watanijulisha," alisema Mosha.
Alisema klabu hiyo imekuwa ikizungumzia usajili kwenye vyombo vya habari, lakini hakuna lolote linalotekelezeka na matokeo yake dirisha dogo litafungwa hakuna chochote kinachoendelea.
Mosha alisema anashangaa kuona anaambiwa afuatilie kibali cha Kenneth Asamoh, wakati hakuhusika katika kumsajili mchezaji huyo, pamoja na kumrudisha mchezaji wa Azam FC Mrisho Ngassa, lakini baadaye tena wametangaza kusitisha suala la mchezaji huyo, huku akiwa hafahamu lolote.
Makamu huyo alisema amekuwa hana imani na baadhi ya viongozi wenzake, hivyo suala lake hilo anawaachia wanachama wa Yanga ambao walimpigia kura ndiyo watakaoamua.
Kama alikuwa na mawazo au azma hiyo, kwa nini asiitoe mbele ya Kikao chenyewe ambako walalamikiwa wote walikuwako? Kwani kukatazwa kusema bila ya idhini ya Mwenyekiti ni kufungwa mdomo? Kwani kazi ya Makamu Mwenyekiti inajumuisha pia kuwa msemaji wa Klabu? Ana lake, aliseme. Wana-Yanga wasipumbazwe na gubu lake!
ReplyDeleteInawezekana yapo matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoambiwa. Lakini, makamu mwenyekiti kujitoa kwa sababu ya kuzuiwa kusema haiwezi kuwa sababu inayoingia akilini.
ReplyDeleteKwenye taasisi yoyote lazima kuwe na utaratibu wa kuongea na vyombo vya habari, vinginevyo, waandishi hao hao watawagonganisha kwa kauli tofauti toka kwa mwenyekiti, makamu, katibu, msemaji wa klabu.........
Mosha ni kibaraka wa Manji nini? Mbona kila wakati anapingana sana na Mwenyekiti wake na anakuwa upande mmoja na Manji? Hata kama ni hivyo,Yanga ina viongozi wake na Mfadhili:Manji.Linapokuja sula la fedha,Manji ana nguvu sana.Lakini suala la kiutawala,Kamati Tendaji ya Yanga chini ya Llyod Nchunga ina msemo wa mwisho.Mosha,soma Warumi 13.Acha fitina..kama vp 'sepa'tu...hatutakuita ng'o!
ReplyDeleteOya Yanga vipi? Kulikoni, mbona migogoro mnatakamuianzishe mpaema,mara mnamtaka Ngassa wakati ngasa mulimuuza Azam, inamaana Ngasa ndile alikuwa mzizi wa yanga,Fanyeni usajili wa dirisha dogo kwa umakini bila viongozi kuzozana.
ReplyDeleteMdau wa simba sc
Mwenyekiti wa Yanga atambue yanayomkuta ndiyo yaliyomkuta Madega.Mwenye pesa ndiye mwenye nguvu.Akae meza moja na Manji na Mosha wamalize tofauti zao ili wasajili vizuri, Papic aliboronga. Vinginevyo timu ikifungwa kwa uzembe atatimuliwa mapema kuliko Madega.
ReplyDelete