25 November 2010

Ufupi wa Twiga Stars wailiza Nigeria.

LAGOS, Nigeria

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria 'Super Falcons', Perpetual Nkwocha amesema katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini, Tanzania iliwapa
wakati mgumu kutokana maumbile yao mafupi.

Mshambuliaji huyo alisema mashindano hayo ya wanawake yaliyomalizika hivi karibuni, yalikuwa ya mafanikio na yaliwapa uzoefu.

Akizungumza na gazeti la Saturday Sports, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murutala Mohammed, Jumatatu iliyopita, Nkwocha alisema jambo hilo pia limewapa uzoefu hususani ukweli ni kwamba wachezaji hao wa Tanzania walikuwa ni wafupi kwa vimo vyao.

Alisema hali hiyo pia ndiyo iliyowafanya 'Twiga Stars' kupoteza mechi zao.

“Najisikia kujivunia sana na ni lazima niwape shukrani marafiki zangu ni kati ya walionisukuma kufunga mabao 11. Kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo nampa sifa Mungu," alisema nyota huyo.

Alisema kuwa mechi yao ngumu katika mashindano hayo ilikuwa ni dhidi ya  Tanzania, kutokana na wachezaji wote kuwa wafupi jambo ambalo lilifanya  kila kitu kwao kuwa kigumu.

"Hatukuweza kucheza, kwani tulijikuta katika wakati mgumu kutokana na kushindwa kufahamu ni wapi pa kuwazuia, licha ya kuwashambulia," alisema.

Alipohojiwa kuhusu siri ya ufungaji mabao yake, alisema siri kubwa ya mabao hayo katika fainali za Kombe la Dunia ni marafiki zake ambao walimfanya afunge mabao 11 na ndiyo maana akafunga mabao hayo.

"Sikuwa chini ya shinikizo la kufunga mabao 15, bali ni msukumo. Katika fainali za Kombe la Afrika zijazo natumaini kufuata njia hii tena," alisema.

Nkwocha alisema pia anadhani kama Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF), likiandaa  mechi ya kirafiki iwe nje Afrika kwani anadhani kama watacheza na Ujerumani kila kitu kitakwenda sawa.

1 comment:

  1. What a bull*** issue hapa ni kushinda na kusonga mbele. Complements za kujidanganya hazisaidii. Ndio maana timu za Tanzania hazifiki popote kwenye mashindano. Figure out how to win. Don't look for some unsound excuses to justify failures.

    ReplyDelete