MADRID, Hispania
KOCHA wa timu ya Real Madrid, Jose Mourinho amesema ilikuwa rahisi kuambulia kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Barcelona, kutokana na kuwa kikosi chake cha Blancos hakikucheza
vizuri katika mechi hiyo, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Katika mchezo huo uliofanyika usiku wa kuamkia jana, Barcelona ilikwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 2-0 na haikugeuka nyuma ikahakikisha inaondoka na ushindi huo, ambao uliifanya ichupe kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya Hispania.
"Timu ndiyo ilicheza vizuri na nyingine ikacheza vibaya mno," Mourinho alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari, mara baada ya mechi hiyo.
"Timu moja ilistahili kushinda na nyingine kushindwa," aliongeza na akasema ilikuwa ni rahisi kuepuka kipigo hicho, lakini hawakucheza vizuri," aliongeza.
Kwa ushindi huo, Barcelona kwa sasa inaongoza kwa pointi mbili kwenye msimamo mbele ya kikosi hicho cha Blancos.
No comments:
Post a Comment