01 December 2010

Kili Stars yachanua Chalenji

*Yaizabua Somali 3-0

Na Elizabeth Mayemba.

WENYEJI wa michuano ya Chalenji Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' jana imechanua katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kuifunga Somali mabao
2-0.

Kwa matokeo hayo, Kili Stars angalau imeresha matumaini kwa mashabiki wake ambao walipoteza, baada ya kufungwa bao 1-0 na Zambia katika mechi ya ufunguzi.

Mchezo huo wa jana uliweza kushuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani hapo, baada ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), inayosimamia michuano hiyo kuondoa viingilio kuanzia jana hadi Jumamosi.

Kilimanjaro Stars ililazimika kusbiri hadi dakika ya 43, kupata bao kwa mkwaju wa penalti baada ya uliowekwa kimiani na Henry Joseph. Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi wa mchezo huo kutokana na Shaban Nditi kuangushwa eneo la hatari.

Kabla ya bao hilo Kilimanjaro Stars ilikosa mabao dakika ya 7, 17, 25 na 37 nafasi ambazo washambuliaji wake, Salum Machaku, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa kushindwa kuzitumia.

Timu ya Bara ilipata bao lake la pili dakika ya 76 kupitia kwa John Boko ambaye alikutana mpira uliotemwa na kipa Somalia ambaye alishindwa kuudaka.

Kilimanjaro Stars ilihitimisha mabao yake dakika ya 88 kupitia kwa Nurdin Bakari aliyefungwa kwa kichwa baada ya kazi nzuri ya Ngassa, ambaye alipiga krosi nzuri iliyotua kwa mfungaji.

Katika mechi hiyo kama Stars ingekuwa makini ingeweza kuondoka na ushindi mnono kutokana na mabeki wa Somalia kujichanganya mara kwa mara kila mashambulizi yalipopelekwa golini kwao.

Mechi nyingine iliyochezwa mchana katika uwanja huo, timu za Zambia 'Chipolopolo' ma Burundi zilitoka suluhu katika mchezo mkali uliokuwa wa vuta nikuvute.

Michuano hiyo itaendelea tena leo ambapo mechi ya kwanza itazikutanisha Sudan na Rwanda na mechi ya jioni itakuwa kati ya Zanzibar na Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment