BARAZA LA MAWAZIRI 2010 | |||
NO | OFISI/WIZARA | WAZIRI | NAIBU |
1 | Ofisi ya Rais | . WN – OR – Utawala Bora Mathias Chikawe 2. WN – OR – Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira | |
2 | Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma | Hawa Ghasia | |
3 | Muungano. | Samia Suluhu | |
4 | Ofisi ya Waziri Mkuu | Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi | |
5 | Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | George Huruma Mkuchika | 1.Aggrey Mwanri 2. Kassim Majaliwa |
6 | Wizara ya Fedha | Mustapha Mkulo | 1. Gregory Teu 2. Pereira Ame Silima |
7 | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | Shamsi Vuai Nahodha | Hamisi Kagasheki |
8 | Wizara ya Katiba na Sheria | Celina Kombani | |
9 | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa | Bernard K. Membe | 1. Mahadhi Juma Mahadhi |
10 | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa | Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi | |
11 | Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi | Dr. Mathayo David Mathayo | 1. Benedict Ole Nangoro |
12 | Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia | Prof. Makame Mnyaa Mbarawa | 1. Charles Kitwanga |
13 | Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi | Prof. Anna Tibaijuka | Goodluck Ole Madeye |
14 | Wizara ya Maliasili na Utalii | Ezekiel Maige | |
15 | Wizara ya Nishati na Madini | William Mganga Ngeleja | 1. Adam Kigoma Malima |
16 | Wizara ya Ujenzi | Dr. John Pombe Magufuli | 1. Dr. Harrison Mwakyembe |
17 | Wizara ya Uchukuzi | Omari Nundu | 1. Athumani Mfutakamba |
18 | Wizara ya Viwanda na Biashara | Dr. Cyril Chami | Lazaro Nyalandu |
19 | Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi | Dr. Shukuru Kawambwa | 1. Philipo Mulugo |
20 | Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii | Dr. Haji Hussein Mpanda | 1. Dr. Lucy Nkya |
21 | Wizara ya Kazi na Ajira | Gaudensia Kabaka | Makongoro Mahanga |
22 | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto | Sophia Simba | Umi Ali Mwalimu |
23 | Wizara ya Habari, Vijana na Michezo | Emmanuel John Nchimbi | 1. Dr. Fenella Mukangara |
24 | Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki | Samuel John Sitta | Dr. Abdallah Juma Abdallah |
25 | Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika | Prof. Jumanne Maghembe | 1. Christopher Chiza |
26 | Wizara ya Maji | Prof. Mark James Mwandosya | Eng. Gerson Lwinge |
27 | Mahusiano na Uratibu. | Stephen Wassira | |
28 | Mazingira | Dr. Terezya Luoga Hovisa | |
29 | Uwekezaji na Uwezeshaji | Dr. Mary Nagu |
25 November 2010
Baraza la mawaziri 2010.
Baraza la mawaziri hili hapa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
tuna waombea mawaziri utekelezaji mwema wa majukumu yao.mgosingwa
ReplyDeleteKwa kuwa wengine hatujui utendaji wao, hatuwezi kulaumu au kusifu uteuzi. Tunawapa muda tuone utendaji wao. Hata hivyo, ninashauri kuwa pale rais atakapoona asiyewajibika kwa ufanisi basi mtu huyo aondolewe mara moja siyo kusubiri mpaka avurunde zaidi
ReplyDeleteJana nilisema Rais Kikwete atatuonyesha usanii wa CCM...si mmeona? Sasa tuna Mawaziri na Manaibu wao 50!!! Kwanza,ameunda Wizara mpya ambayo sio lazima iwepo,Wizara ya Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu ambayo amemkabidhi Mh.Stephen Wassira.Wizara hii itapoteza mishahara ya Kiserikali bure...usanii mtupu! Kuna haja gani ya kuwa na Ofisi mbili zinazoshughulikia Uratibu? Kwani ni uratibu wa nini hasa kama si vyeo vya kupeana tu? Pili,Mh.Rais si msikivu.Kuna haja gani ya kuwa na Wizara mbili zinazoshughulikia mambo ya nje? Kwani Afrika Mashariki ni NDANI?Jambo lingine ni kuwa hadi sasa Mh.William Lukuvi ana vyeo vya kitaifa vitatu:Mbunge wa Ismani,Mkuu wa Mkoa wa Dar na Waziri Mteule wa Sera,Uratibu na Bunge.Hii haki jamani? Ye kwani nani hasa? Kwakuwa mi si mnafiki napongeza kwa moyo wangu wa dhati uteuzi wa Prof.Anna Tibaijuka,Dr.John Pombe Magufuli na Dr.Harrison Mwakyembe ambao wote wapo kwenye Wizara Stahiki..Ila hakukuwa na sababu ya kuigawa Wizara ya Miundombinu.Kwa hawa wateule,mambo yangewezekana...Mzigo mzito mpe
ReplyDeleteMsukuma!Kilichofanyika hapa si lolote ila kuunda ajira mpya tu.Kwanza kubadilibadili Wizara namna hii kunaleta tabu kubadili majina ya majengo ya ofisi na hata 'platenumber' za magari ya waheshimiwa.Pia haionyeshi muendelezo wa majukumu ya kiserikali...kila siku mambo yanaanza upya!Mh.Kawambwa ni mtalii wa Wizara mbalimbali? Kwanini asitulie sehemu moja tumpime uwezo wake? Mh.Sitta,ile Ofisi ya Spika kule Urambo aigeuze Ofisi ya Afrika Mashariki.Kwakuwa wengi ni wapya tusubiri ili tuone meupe na meusi yao.Tuwe na subira...Mh.Kikwete ingia na timu yako Uwanjani.
Mhariri, Majira
ReplyDeleteAhsante kwa hii taarifa. Fanya kazi ya uandishi ya ziada kwa kutuwekea picha za wateuliwa husika.
Wizara 29, GDP ya Tz below USD 25 billion, hapa kidogo JK ume overlook!
ReplyDeleteKwa nini usijenge kikosi kibunifu cha wachapa kazi kama wizara chini ya 15, ndani yake manaibu mawaziri proffesionals kushughulikia matatizo na maendeleo mbali mbali ya nchi.
Pia, ungelipamba baraza lako kwa kuwaingiza qualified opposition MPs kwa lengo la kuwa wewe ni Raisi wa raia wote, wakiwemo wasiokuchagua.
Hata hivo unastahili CREDIT kuweza ku double Tz per capita GDP within 5 years!
Be focused, economy inaweza ikawa legacy nzuri ya utawala wako!
Sina tatizo na wasifu wa mawaziri walioteuliwa wala ukubwa wa baraza hili. Tatizo lipo kwenye uwekaji vipaumbele. Hotuba ya Raisi inaonesha kuwa kwa miaka mitano serikali itafanya kila kitu. kwa jinsi hiyo ni lazima awe na baraza kubwa kama hili la mawaziri. Sitarajii mawaziri hawa watafanya miujiza kufanya makubwa yanayoonekana kwa kugawana ka-sungura tulikonako na kwa kubembeleza huruma ya majirani ambao pia wanaotea uzembe wetu ili wanufaike na tulichonancho. Laiti Raisi na washauri wake wangechagua vipaumbele vichache kulingana na uwezo tulionao, vipaumbele ambavyo vikitekelezwa vitainua uwezo wetu wa kufanya makubwa zaidi msimu ujao, angegundua kuwa hahitaji mlolongo wa mawizara kama huu.
ReplyDeleteKusifu ni baada ya kuona utendaji wa kazi. Natumaini watafanya kazi kwa ajili ya/ na Watanzania na sio ubinafsi.... jamani ufisida Tanzania umezidi!!! Naomba nyie mawazili kufanya kazi kwa kushirikiana na Watanzani.
ReplyDeleteMimi namuunga mknono Dr. Slaa, katibu wa Chadema, kuwa uteuzi unaozingatia "USWAHIBA" badala ya uwezo wa mtu ni hatari kwa kuwa unalenga kumpatia kila rafiki Uwaziri.Mawaziri wanaotokana na bunge ni hatari sana!!!
ReplyDeleteHONGERA SANA MHE. RAIS KWA BARAZA LAKO TUKUFU LA MAWAZIRI 2010-2015. ILA CHAGA DEV.MAN HAWATAKAA WAFURAHIE KWANI UCHU WAO WA KUINGIA IKULU UMEGONGA MWAMBA. SASA MUDA UMEFIKA KWAO KWENDA KULA MIHOGO HUKO KEWENYE MAJIMBO YAO HASA MHE... KAMA ALIVYODAI KWAMBA AKIINGIA IKULU BASI ANGEKUNYA CHAI NA MIHOGO ILI KUBANA MATUMIZI ILI FEDHA YAKE AIPELEKE KULETA MAENDELEO YA WANACNCHI. MBONA ALIPOKUWA MBUNGE HAKULA MIHOGO BUNGENI ILI MARUPURUPU YAKE AWPELEKEE WANACHI WALIOMCHAGUA????
ReplyDeleteNA HAO CHADEMA WANAODAI KABWE KAKIKOSEA HESHIMA CHAMA CHAKE, JEE HAO WABUNGE WA CHADEMA HAWAJAWAKOSEA HESHIMA WANANCHI WALIOWAINGIZA BUNGENI NA HATIMAYE KUJISAHAU KWAMBA WALIAPA NINI...?
ReplyDeleteWIZARA NYETI KAMA,ELIMU,ULINZI,FEDHA,MAMBO YA NDANI,SAYANSI NA TECHNOLOGIA,KILIMO ZIKO KWA AKINA NANI???? KIKWETE KADHIIRISHA UDINI ALIOKUWA ANAUKATAZA,HONGERA KIKWETE KWA KUWEKA MBELE UDINI
ReplyDeleteHakuna jipya ni uswahiba atakiona cha moto, kwa sasa tunaongelea mabadiliko ya katiba na yatakuja kwa nguvu ya umma na si kuomba kwa JK
ReplyDelete