07 January 2013
Stewart, Bausi nusura 'wazichape kavukavu'
Na Speciroza Joseph, Zanzibar
KATIKA hali iliyowaacha midomo wazi mashabiki wa soka walioshuhudia mechi kati ya Miembeni FC na Azam FC, makocha wa timu hizo nusura warushiane ngumi baada ya kujibishana wenyewe kwa wenyewe.
Kitendo hicho kilitokea kwenye Uwanja wa Amaan juzi usiku, wakati timu hizo zikicheza mchezo wao wa pili wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo hadi dakika 90 zinamalizika Azam Fc waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza visiwani hapa.
Makocha hao Salum Bausi wa Miembeni na Stewart Hall wa Azam FC wakati wa mapumziko waliwafuata waamuzi kupeleka malalamiko yao, lakini kabla hawajamaliza wakaanza kujibishana wenyewe kwa wenyewe.
Kitendo hicho kilitafsiriwa tofauti na wapenzi wa mpira kwa kuita si kitendo cha mpira kwa makocha hao wakubwa kujibishana na kutaka kupigana uwanjani wakati timu zao zikienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Vurugu hizo ziliendelea japo waliamriwa na makocha wao wasaidizi, majibishano yaliendea hadi katika milango ya vyumba vya kubadilishia nguo hali iliyosababisha waamuliwa na kusimamiwa ili wasiingiliane vyumbani.
Kabla ya kuanza kipindi cha pili mwamuzi aliyekuwa analalamikiwa Ally Amary Kisaka aliwaita makocha hao kwa pamoja na kuwatoa kwenye mabenchi kwa kuwapa kadi nyekundu wakakae jukwaani, walitekeleza amri hiyo na kuacha timu zikiwa chini ya wasaidizi wao.
Benchi la Miembeni lilibaki chini ya Saidi Kwimbi huku Kali Ongala alisimamia upande wa Azam FC kwa mafanikio na kupata ushindi.
Baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha Bausi alisema sababu ya kutokea ugomvi huo kocha Stewart alimtukana kitendo kilichompandisha hasira na kuanza kujibishana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment