18 December 2012
Pinda akagua mradi wa umwagiliaji
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ametembelea mradi wa umwagiliaji wa Ugalla na kusifu juhudi za wananchi wa kata
hiyo katika Wilaya mpya ya Mlele, mkoani Katavi.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ugalla juzi baada ya kukagua mradi huo, Bw. Pinda aliwashukuru wakazi hao kwa kuibua mradi huo ili waweze kunufaika na maji ya Mto Ugalla.
Aliwataka wakazi hao kuheshimu uamuzi wa kutoa eneo hilo kwa mradi ili kuepuka migogoro ya umilikaji kifamilia na ukoo.
Akitoa maelezo kwa Bw. Pinda, Mhandisi Mkazi wa Umwagiliaji Kanda ya Mbeya, Bw. Elibariki Mwendo, alisema wamejenga tangi la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 530,000 ambazo zinaweza kumwagilia hekta 225.
Alisema mitambo ya kupandisha maji kwenye tangi itaendeshwa kwa nguvu ya umeme wa jua na ule unaozalishwa kwa upepo.
Mradi huo uliibuliwa na wananchi mwaka 2007, umegharimu
sh. milioni 778, utahudumia watu 3,077 na unamilikiwa na wanachama 146.
Bw. Pinda leo atendelea na ziara yake katika Kata ya Sitalike ambako atahutubia wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment