20 December 2012
Mtoto wa Dkt. Salmin amkana ndugu 'jambazi'
Na Mwandishi Wetu
MTOTO wa pili wa Rais mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, ameibuka na kukanusha vikali kuwa Bw. Kassim Ramadhan Juma (27), aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya
habari kukamatwa kwa ujambazi si ndugu yao katika familia.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mtoto huyo Bw. Amin Salmin, alidai kusikitishwa na kijana huyo kutumia vibaya jina la baba yake wakati hatoki katika familia yao.
Alisema mama wa kijana huyo anayejulikana Bi. Salma Kasu, wakati akiolewa na baba yake mwaka 1990, tayari mtoto huyo Bw. Juma alikuwa amezaliwa akiwa na umri wa miaka 22.
“Wakati baba yangu akimuoa mama yake, kijana huyu alikuwa na miaka 22 ina maana baba alimkuta, iweje leo ajiite mtoto wa Amour tena katika mambo yake mabaya yasiyofaa katika jamii, huku ni kumchafua mzee wetu na kumpa presha,” alisema Bw. Salmin.
Aliongeza kuwa, yeye anawatambua vizuri ndugu watatu, aliowataja kwa majina ya Abal, Hamoud na Salama, ambao baba yake amezaa na mama wa kijana huyo.
“Huyu ndugu jambazi hatumtambui kabisa katika familia yetu, namuomba sana huyo kijana na wenzake wasiendelee kutumia jina la baba yangu kwa maovu yao na kumchafua,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment