10 December 2012
EWURA, wadau kujadili bei za umeme
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeandaa mkutano ambao utajadili marekebisho ya bei za umeme unzozalishwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Haruna Masebu, ilisema mkutano huo utafanyika Desemba 10 mwaka huu na utashirikisha wadau mbalimbali.
Alisema EWURA itakusanya maoni ya wadau juu ya marekebisho
ya bei za nishati hiyo kuanzia mwaka huu hadi 1015.
“Katika kukamilisha mchakato huu, tunawaalika wadau wote kuhudhuria mkutano huu ambao utafanyika katika Ukumbi wa
Karimjee, Dar es Salaam, kuanzia saa nne asubuhi,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment