30 November 2012

Majambazi 10 wakamatwa Dar *Wakutwa na SMG, gari, simu ya upepo


Na Angelina Faustine

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia majambazi sugu 10, waliokamatwa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam na Pwani wakiwa na silaha mbalimbali za moto walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu na mauaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema kati ya majambazi hao watatu ni raia wa Burundi na saba Watanzania ambao wengine walikamatwa Ikwiriri, mkoani Pwani.

Alisema majambazi hao walikamatwa katika msako mkali ambao ulifanywa na jeshi hilo wakiwa na bunduki aina ya bunduki SMG yenye namba UG 7261, moja ikiwa imefungwa hirizi nyekundu
pamoja na risasi 12.

“Hawa majambazi pia walikutwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba ya usajili T 745 AZB, simu moja ya ya upepo aina
ya GP 340, mtalimbo wa kuvunjia milango, kofia aina ya ballet yenye nembo ya uhamiaji, koti moja la polisi, bastora moja
aina ya Chinese na nyingine aina ya Berreta,” alisema.

Aliongeza kuwa, majambazi hayo yalimtaja mtu aliyewaleta jijini Dar es Salaam kufanya uharifu kuwa ni Rashid Mselem 'Chidi', mkazi wa Pugu, ambaye alikamatwa na pikipiki aina ya Baja aliyokuwa akiitumia kufanya uharifu.

Aliwataja baadhi ya majambazi hao kuwa ni Mnaziri Abduliksrim, Uwimana Gervas, Issa Shabani, Ilahunda Francis wote raia wa Burundi pamoja na Rashid Hussein mkazi wa Magomeni, Dar
es Salaam.

Katika hatua nyingine, Kamnda Kova aliwataka wananchi watoe taarifa ya mtu au watu wanowatilia mashaka kwani jeshi hilo limejipanga kupambana na watu wanaovunja amani na utulivu.

1 comment:

  1. HALI YA UJAMBAZI WAKATI WA UTAWALA WA RAIS BENZAMIN MKAPA ILIKUWA WAKUTISHA RAIS KIKWETE ALISEMA CHINI YA UTAWALA WAKE NI MWIKO MAJAMBAZI KUTAMBA SIELEWI KIKWETE ATAKAPOKUWA ANAMNADI MGOMBEA URAIS WA CCM ATAJITETEA VIPI KUHUSU UJAMBAZI

    ReplyDelete