08 June 2012

Power tiller yaokoa wakulima Kondoa


Na Peter Mwenda

MATREKTA madogo (Power tiller)  yameongeza ufanisi katika kilimo cha mazao wilayani Kondoa na kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti na ufuta.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa, Bw. Nicolus Kombe aliambia majira kuwa matrekta madogo yanayonunuliwa na Halmashauri hiyo kutoka Kampuni ya Kubota yamekuwa imara kutokana na ardhi ya Wilaya ya Kondoa.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya  Kondoa mpaka sasa imekwisha nunua matrekta madogo 89 kuviuzia vikundi vidogo vidogo vya ushirika vya wakulima wadogo wamekopeshwa.

"Wakulima wadogo wilayani Kondoa wameongeza kiwango cha kilimo kutoka majembe ya mkono na sasa wanatumia matrekta ambayo yameongeza ufanisi wa usafiri, kufua umeme, kubeba mazao" alisema Mkurugenzi huyo.

Meneja Masoko wa kampuni ya Kubota, Bw. David alisema kampuni yake imekuwa ikitoa mikopo ya matrekta madogo katika wilaya mbalimbali nchini kupitia Halmashauri na maombi ya vikundi hivyo yanaongezeka siku hadi siku.

Mratibu wa kikundi cha Mshikamano chenye trekta moja alisema imekuwa mkombozi kwa wakulima wa wilaya ya Kondoa kwani mkulioma aliyekuwa akilima ekari mbiuli za alizeti sasa analima ekari 20.

No comments:

Post a Comment