23 January 2012

Programu masoko kusaidia wakulima vijijini

kuwafikia wananchi milioni 15


Na Ibrahimu Hamidu

SERIKALI imeazimia kuinua sekata ya kilimo nchini ili kuongeza uzalishaji
na pato la Taifa.

Elimu kuhusu  kilimo bora na umwagiliaji ikitolewa kwa wananchi, wanaweza kuondokana na umaskini kwa kuwa, hawana ulelewa wa kutumia kilimo kusaidia maendeleo katika maendeleo ya sekta nyingine.

Ili kufanikisha hilo,  Programu mpya ya Miundombinu ya Masoko, uongezaji thamani na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) ilizinduliwa kusaidia lengo hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Bw.William Lukuvi akizindua program hiyo anasema,  itadumu kwa miaka  miaka saba 2011/2012 hadi 2017/2018.

Anasema,   programu hiyo itaangalia   katika miundombinu ya mifumo ya masoko, uendelezaji wa huduma za kifedha vijijini  na uratibu wa programu.
Uchambuzi  wa kiuchumi uliofanyika unaonesha kuwa, program hiyo itakuwa na matokeo mazuri kwani huduma zake zitawafikia zaidi ya wananchi milioni 15.

”Serikali imeshirikiana na wabia wa maendeleo mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo , benki ya maendeleo ya afrika  na umoja wa mapinduzi ya kijani afrika,”anasema  Bw. Lukuvi

Utekelezaji wa MIVARF utaongeza fursa za masoko ya mazao ya kilimo pia pato la wazalishaji wadogo 500,000 watakaoshiriki katika  programu.
Anasema,  program hiyo itaongeza fursa za huduma za kifedha kwa wananchi 500,000, kaya 20,000  watakaoshiriki katika mafunzo na kuboresha asasi za akiba mikopo na benki ya jamii.

Anasema,  itasimamia na kudhamini utoaji mikopo kwa sekta ya kilimo kufikia shilingi bilioni 350 kwa kushirikisha na benki za biashara nchini ambapo itawafikia  wakulima zaidi ya 250,000 na vikundi vya wajasiliamali  zaidi ya 16,500.

Anasema,  program hiyo itatekelezwa kwa mtindo wa kutumia vigezo mbalimbali ili kupata ushiriki unaokidhi mahitaji halisi badala ya kupeleka huduma kwa mazoea.

“Utekelezaji wake utaongozwa na utayari wa mikoa, halmashauri za wilaya, watoa huduma wa sekta binafsi, wakulima, wazalishaji na wafanyabiashara wadogo kutumia fursa zilizopo katika program anasema na kusisitiza kuwa,

“Uelewa mzuri wa washiriki kuhusu vigezo vitakavyotumika ni muhimu sana ili kujihakikishia ufanisi katika utekelezaji,kwa wale ambao watakuwa hawakukidhi vigezo itatolewa fursa ya kurekebisha upungufu utakaojitokeza ili kufikia vigezo na kuanza utekelezaji bila kuchelewa” anasema Bw. Lukuvi

Anasema,  vigezo hivyo vimewekwa bayana kwa watendaji wote ili wavielewe na kutoa wito kwa uongozi wa program kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa umakini na kusingatia weledi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wake.

Anasema,  kilimo  kitaendelea kuwa sekta kiongozi katika uchumi nchini inayotoa ajira asilimia 77.5 ya watanzania wote na kuchangia asilimia 95 ya chakula.

Anasema,  hatua  zilizochukuliwa  kilimo ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji,kuongeza ruzuku ya pembejeo na utekelezaji wa program hiyo.

Anasema,  pamoja na mafanikio yaliyopatikana wakulima wengi vijijini bado wanakabiliwa na changmoto  za uzalishaji duni, ukosefu wa masoko, mawasiliano na uchukuzi dhaifu, ukosefu wa huduma za vyombo vya fedha na uwezo mdogo wa kujiwekea akiba.

Anasisitiza kuwa,  MIVARF ni mojawapo ya juhudi za serikali kuwasiadia wakulima hasa wanaoishi vijijini kuondokana na umasikini kwa kuwaongezea kipato pia  kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.

Bw.Lukuvi anasema, programu hiyo  ni mwendelezo wa mafanikio yaliyopatikana  katika utekelezaji wa uendelezaji wa mfumo wa stakadhi ghlani.

“Katika hizo takwimu kumekuwa na mafanikio katika mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani ambapo wakulima walioshiriki waliweza kupata bei nzuri kwa wastani wa mara mbili au tatu zaidi ya bei wakati wa mavuno” anasema  Bw.Lukuvi.

Akitolea mfamo bei ya zama alitoa mfano wa kilo moja ya mahindi kuuzwa shilingi 357 badala ya shilingi 150 wakati wa kuvuna na mpunga kuuzwa 850 kwa kilo badala  ya 257.

Alisisitiza kuwa,  katika kipindi cha utekelezaji wakulima 4,066 waliweka mazao yao yaliyofikia tani 15,600 zilizowawezesha kupata mikopo ya shilingi bilioni 4.1.

Katika kuimarisha mfumo huo maghala 13 ya kuhifadhi mazao ya kilimo  kukarabatiwa, pia  masoko 24 yalijengwa  kwa sera za vijijini zenye na  kuongeza uwezo wa kufikisha mazao sokoni wka gharama nafuu.

“Ukarabati wa barabara uliofanywa uliwezesha kupunguza muda wa safari kwa mkulima kutoka  saa moja na nusu kwa trekta au saa sita kwa mkokoteni wa punda hadi nusu saa kwa magari magari madogo ya abiria, “ anasema.

Anasema,  programu hiyo iliwezesha halmashauri 16 kupitia na kurekebisha taratibu za ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi ili kuongeza ufanisi  wa vyanzo vya  mapato.

Asasi za akiba na mikopo zilizowezeshwa ziliongezeka toka 180 mwaka 2005 hadi 276 mwaka 2010,  katika wilaya 22 huku katika kipindi hicho wanachama waliongezeka toka 35,581 kuwa 117,524 na amana, hisa na akiba kzikiongezka toka bilioni 1.68 kuwa bilioni 19.72.

Anasema,  ni lazima kuboresha sekta ya kilimo na kubuni fursa zaidi za kuongeza kipato kwa wananchi, fursa hizo ni pamoja na masoko ya mazao ya kilimo maeneo ya vijijini, kuongeza tija katika kilimo na sekta za uchumi vijijini na kuwawezesha wananchi kuhimili ushindani katika utandawazi.

Anasema,  bima ya mazao ni chombo kinachoweza kutumiwa na wazalishaji wa mazao ya kilimo ili kujilinda na upotevu unaoweza kusababishwa na majanga ya asili kama ukame, mafuriko au upotevu unaosababishwa na kushuka kwa bei za bidhaa za kilimo.

“Ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya kilimo ,ni muhimu kwa  mawakala wa bima kupitia mamalaka ya mapato nchinikiano na mamlaka ya hali ya hewa) kuwa na bima ya mazao ili kupunguza utegemezi wa udhamini wa mikopo ya sekta ya kilimo” anasema bw.Lukuvi

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar,  Affan Othman Maalim alimuahidi waziri kutumia vigezo vilivyopo katika program hiyo ili kuepuka upendeleo na kuhakikisha program hiyo inafanikiwa

No comments:

Post a Comment