10 June 2011

Wawili wafa, 10 wajeruhiwa ajalini

Na Daud Magesa,Mwanza

WATU wawili wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani Kwimba kwenda Mwanza kuacha njia na kugonga miti.Miongoni
mwa waliojeruhia katika ajali hiyo ni pamoja na Padri mmoja wa Kanisa Katoliki wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza.

Ajali hiyo ilitokea Jana saa 4:00 asubuhi katika barabara ya Mwanza-Shinyanga, kwenye kijiji cha Nyang’holongo Wilaya ya Misungwi na kulihusisha basi dogo aina ya Mitsubishi, lenye Namba T 312 BZD mali ya George Mkisi mkazi wa Mwanza.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, Ofisa Mnadhimu wa Polisi, Nonosius Komba alisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi wa basi uliosababisha dereva kushindwa kulimudu wakati akimkwepa mwendesha pikipiki.

Baada ya kushindwa kumkwepa mwendesha pikipiki gari liliacha njia na kugonga miti miwili iliyokuwa kando ya barabara na kuababisha vifo vya watu wawili papo hapo baada ya paa la gari hilo kung’oka.

Waliofariki katika ajali hiyo walitajwa kuwa ni pamoja na kondakta wa basi
hilo, Khalfan Kassim (23) mkazi wa Nyegezi jijini hapa na mwanaume mmoja jina halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-40.

Majeruhi walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
(BMC) na watatu kati yao hali zao ni mbaya

Majeruhi ambao hali zao ni Ladslaus Charles (23) mkazi wa Malya Kwimba, Padri Kabipi Narcis wa Ukerewe na mwamnaume mmoja ambaye jina
halikufahamika.

Wengine ni Jane Titus (45) mkazi wa Shinyanga, Mustapha Kulwa (24) wakala  wa mabasi wilayani Kwimba, Chakupewa Zepharine (45) mkazi wa Kahangala
wilaya ya Magu na Theresia Mulabele (28) mwalimu wa Shule ya Sekondari Malya.

Majeruhi wengine ni Matumo Bathelomew (28), mwalimu wa Chuo cha Michezo Malya Kwimba, Sindano Daniel (34) fundi pampu na  kazi wa Bwiru pamoja na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Malya aliyetajwa kwa jina moja la Felister.

Dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kusababisha ajali na vifo kwa uzembe.

No comments:

Post a Comment