Na Rashid Mkwinda, Mbeya
WATU 11 wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara wanashilikiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Rungwe, Bw. John Mwankenja (50).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Mbeya jana Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Bw. Advocate Nyombi alisema kuwa,sanjari na kukamtwa kwa wtu haoa pia jeshi hilo limekamta bunduki aiina ya SMG yenye namba za usajili 786474 ikiwa na risasi 37.
Alisema kuwa bunduki hiyo inadaiwa kutumika kwa katika mauaji hayo yaliyofanyika Mei 19, mwaka huu saa 2:30 Kiwira wilayani Rungwe.
Bw. Nyombi alisema kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi limefanya msako wa siku 10 na kuwanasa watuhumiwa hao wakiwa na SMG hiyo.
Alisema kuwa silaha hiyo ilikamatwa Mei 31,mwaka huu saa 10: 00 alasiri ikiwa na risasi 37 na nyingine 17 katika magazine, moja ikiwa tayari katika chemba. Pia kulikutwa jaketi moja kubwa rangi ya bluu lenye kofia ya kujificha sura na kofia nyeusi aina ya mzula.
Bw. Nyombi alisema kuwa ndani ya jaketi kulikutwa funguo 27 ambazo zinasadikiwa kutumika katika vitendo vya uhalifu na uchunguzi zaidi unafanyika ili kuwanasa watu walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.
Awali, Bw. Nyombi alisema kuwa marehemu Mwankenja aliuawa kwa kupigwa risasi tano kichwani akiwa ndani ya gari aina ya Nissan Double Cabin yenye namba za usajili T 127 ACZ mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe.
No comments:
Post a Comment