Na Jovin Mihambi, Chato
WACHIMBAJI wa dhahabu zaidi ya 15 wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ya ndani ya shimo wakati wakichimba dhahabu katika machimbo ya
Mwambo, Kata ya Makurugusi wilayani Chato Mkoa wa Kagera.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kuhusu tukio hilo baadhi ya wachimbaji walikuwa karibu na shimo hilo walisema tukio hilo limetokea juzi asubuhi, lakini taarifa nyingine zinakanusha idadi hiyo, zikisema waliokufa ni pungufu.
Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo na hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa waliingia katika shimo hilo kwa wingi na mara moja kutokana na taarifa za kuwepo kwa dhahabu nyingi.
"Watu hao waliingia katika shimo hilo kwa wingi tena kwa kwa kubanana" alisema.
Hata hivyo baadhi ya viongozi waliozungumza na Majira kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini walisema kuwa watu waliokufa ni watatu na wala sio 15 na tayari maiti mbili zimeopolewa katika shimo hilo.
Akizungumza na Majira, Ofisa Mtendaji wa Kata Mukurugusi, Bw. Fabian Sugwa
aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Bw. Kulwa Geni mkazi wa Ngokoro wilayani Bariadi, Bw. Pita Misungwa (Mapala Bariadi) na pia alimtaja mmoja ya watu waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Bw. Bukasi Magoa(Nyarugusu Geita).
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Khadija Nyambo alisema kuwa katika tukio hilo waliofariki ni watu wawili na tayari miili yao imeopolewa kutoka shimoni.
Alisema kuwa katika shimo hilo kulikuwa na watu wengine wanne lakini hadi sasa hawajulikani walipo.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa eneo hilo waliliambia gazeti hili kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya watu kufunikwa na kifusi bila kuyatolea taarifa kutokana na mgodi huo kutokuwepo kisheria.
USTAARABU GANI HUU? MBONA MNATUKANA? KUWENI NA ADABU MNAPOTUMIA VYOMBO VYA KUELIMISHA JAMII. UKITUKANA NDIO WAONEKANA SAWA NA HILO TUSI ULILOTUKANA.
ReplyDeleteNDIYO MAADILI MNAYOWAFUNDISHA WATOTO WENU/WADOGO ZENU NA JAMII KWA UJUMLA? HEBU TUTUMIE VYOMBO HIVI KAMA WENYE AKILI TIMAMU. KWA NINI UMTUPIE LAWAMA MWINGINE WEWE UMESAIDIA NINI AU KUSHAURI NINI? AU MNASUBIRIA KUFANYIWA? HATUTATOKA TULIPO KWA STAILI HII YA KUSUBIRIA NINI KIMETOKEA HALAFU TUTUKANE BADALA YA KUWAONEA HURUMA WALIOPATWA NA MATATIZO NA KUTOA USHAURI WENYE TIJA. SIJAFURAHIA MATUSI KWA KWELI. JIREKEBISHENI MLIOTUKANA. MUNGU HAPENDI.