21 April 2011

Ajifungua na kumtumbukiza mtoto chooni

Na Rehema Mohamed

MKAZI wa Mikocheni Bi. Happy Freddy (28), anashikiliwa na Polisi mkoa maalumu wa Kinondoni kwa kosa la kumtupa mtoto wa kiume wa siku moja na kumsababishia
kifo.

Kamanda wa Mkoa huo Bw. Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8.20 mchana Mikocheni 'A'.

Alisema mtoa taarifa, Bi. Shadya Ally (18) ambaye ni wifi wa mtuhumiwa huyo alitoa taarifa za tukio katika kituo cha polisi Osterbay.

Alisema mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake Mikocheni A alisikia uchungu na kumuomba wifi yake huyo amsindikize hospitali.

Alisema wakiwa njiani eneo la Kanisa la walokole mtuhumiwa alimwambia wifi yake anajisikia haja na kwenda chooni karibu na eneo hilo kujisaidia na yeye kumsubiri nje.

Alisema ghafla Bi. Ally akiendelea kumsubiri wifi yake alisikia sauti ya mtoto ikilia na kuamua kumfuata na kukuta mtoto wa jinsia ya kiume kikiwa kimeegeshwa pembeni mwa tundu la choo.

Alisema baada ya kuwasha tochi ya simu yake ya mkononi alimwona vizuri mtoto na kwamba mtuhumiwa alimsukuma mtoto ndani ya choo kwa mguu wake akidai ameharibika.

Alisema mwili wa mtoto huyo iliopolewa chooni na majirani wa eneo hilo kwa kushirikiana na polisi.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamla na Mtuhumiwa anahojiwa na polisi.

2 comments:

  1. kama hamtaki kuzaa watoto mnakimbilia nini kuwa na wanaume wakati mkijua kuwa mimba ni matokeo ya mausiano ya ngono mnazofanya?

    ReplyDelete
  2. ole wako na wenzio wengine wenye vitendo kama vya kwa kuna wenzio nao walifanya hivyo leo wanatafuta watoto hadi kwa waganag wa kienyeji na kwa viongozi wa dini hawapati.kuna watu leo wanatoa hadi machozi ya damu kwa kukosa watoto pengine nao walichezea maisha kama wewe. lakini kumbuka adhabu yako ni hapa hapa duniani. lakini na nyie wanaume mnaowarubuni wanawake kwa kuwapa chipsi mayai acheni tabia hiyo vinginevyotumieni kondom basi muepuke mabalaa haya. mbona kondom zipo kila mahali hadi kwenye kiosiki. Ngono mfanye wawaili adhabu apate mmoja. Na nyie akina dada msidanganyike jamani mbona mnazidi rundika magunia ya dhambi duniani

    ReplyDelete