LONDON, Uingereza
MLINZI wa klabu ya soka ya Manchester City, Kolo Toure, amezipuuza habari za kugombana na mchezaji mwezake wa zamani katika klabu ya Arsenal, Emmanuel Adebayor, wakiwa mazoezini na kusema kuwa, suala hilo tayari
'limesahaulika'
Toure na Adebayor walikamatana kwa kutaka kupigana mazoezini na kuwalazimu wachezji wenzao kuingilia kati kuwatenganisha, wakati wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Arsenal uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Toure, ambaye alicheza pamoja na Adebayor Gunners, amelipuuza tukio hilo na kuliita ni dogo, ingawa alikiri kuwa, yeye na Adebayor wamekuwa na kawaida ya kuzozana."Ilikuwa ni ugomvi uliotokana na rafu mbaya," Toure alilimbia gazeti la The Sun.
"Sote tulikuwa na hasira, lakini tulikuja kutulia. Wachezaji wengine na kocha, walikuja kututenganisha.""Tayari imesahaulika. Kwa vyovyote, mimi na Adebayor haikuwa mara ya kwanza na haitakuwa mara ya mwisho.""Katika Arsenal, tulikuwa mara kwa mara tukizozana. Tunajuana vizuri, pengine vizuri zaidi."
Mchezaji mwenzao, Mario Balotelli na Jerome Boateng, nao habari yao iliwahi kutawala kwenye vyombo vya habari, baada ya kugombana mazoezini msimu huu.Adebayor, pia aliwahi kuzozana na beki wa City, Vincent Kompany, katika mechi ambayo City, ilifungwa mabao 2-1, dhidi ya Wolverhampton Oktoba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment