*Rostam Aziz atajwa hukumu ya ICC
Na Mwandishi Wetu
WAKATI serikali ikisubiriwa kutoa msimamo kama ama italipa sh. bilioni 185 kama tuzo kwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans au la, imebainika kuwa
moja kati ya mitambo husika katika sakata hilo bado ni mali ya Richmond Development Company (RDEVCO L.L.C).
Taarifa za uchunguzi zilizolifikia Majira zimethibitisha pasipo shaka kuwa mtambo huo wa kutumia gesi wenye namba TM2500 bado ni mali ya Richmond, na kuna kipindi kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamishia mkataba wake kwa Dowans ililizuia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lisinunue mtambo huo kwa kuwa ni mali yake.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimelieleza Majira kuwa kulingana na vielelezo vilivyopatikana, wakati wote serikali ilipokuwa inadhani inashughulika na Dowans, kumbe ilikuwa bado inacheza na Richmond ile ile.
“Nakwambia hawa ni ndugu moja, na hizi taarifa tuinazopata ni pale tu waliposhindwa kuelewana. Kwa hiyo tara serikali ikimlipa Dowans, fedha za walipa kodi zitakuwa zinaingia Richmond, kilisema chanzo chetu kimojawapo.
Oktoba 14, 2006 kampuni ya RDEVCO L.L.C ya Texas, Marekani ilitiliana saini mkataba na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ya Costa Rica ili kuhamisha mkataba kati yake na TANESCO, kuhamisha umiliki wa mitambo hiyo na kuikabidhi mikoba yote kuhusiana na uendeshaji, uzalishaji na uuzaji wa umeme wa dharura.
Tangu wakati huo, Dowans imeendelea kutambuliwa kuwa ndiyo iliyokuwa inatekeleza majukumu ya Richmond na hata baada ya mkataba wake kusitishwa na serikali, ndiyo ilikwenda Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC-Court) dhidi ya TANESCO na kudai fidia, hatua ambayo imesababisha shirika hilo la umeme kuhukumiwa kulipa sh. bilioni 185.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria wameshangaa hatua hiyo wakisema kuwa Richmond na Dowans bado ni washirika na kubainisha kuwa licha kuwapo kwa mkataba huo wa kuhamishiana majukumu, uliosainiwa na Dkt. Mohamed S. Huque kwa niaba ya Richmond na HenrySurtee kwa niaba ya Dowans.
Wanasheria hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini wamelieleza gazeti hili kuwa miaka miwili baada ya mkataba kati ya kampuni hizo kusainiwa, Richmond iliiandikia barua TANESCO kuitaarifu kuwa isinunue mtambo huo kutoka Dowans (kama ilivyokuwa imesikia uvumi), kwa sababu mtambo huo bado ni mali yake.
Barua hiyo iliyoandikwa na Kampuni ya Wanasheria ya KLPATRICK STOCKTON LLP Oktoba 18, 2008 kwa niaba ya RDEVCO, L.L.C ilisema: “Lengo la barua hii ni kuifahamisha TANESCO kwamba Dowans si mmiliki wa mtambo mmojawapo katika eneo hilo, GE TM2500 S/n 481-364, 7LM2500-PE-MDW GE Unit. Mtambo huo unamilikiwa na RDEVCO, L.L.C.”
Barua hiyo iliyosainiwa na Thomas Philip Wilson kama wakili wa RDEVCO, L.L.C ilielekezwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Idris Rashid na kupokewa Oktoba 20, 2008.
“Kitendo cha Richmond kuzuia kuuzwa kwa mtambo huo, kimetoa mwanga kuwa kampuni hiyo iliyoshindwa kazi na kuhamisha mkataba wake, bado ni mmiliki halali wa mitambo hiyo, jambo ambalo linathibitisha kuwa kampuni hizo bado ni ndugu, na huenda malipo yanayodaiwa kwa serikali yanakwenda kwa Richmond.
Katika hatua nyingine, wakati swali la ‘Dowans ni nani’ likiulizwa bila majibu, imefahamika kuwa jina la Rostam Aziz limetajwa katika hukumu ya ICC akielezewa kama mtu mwenye ‘ushawishi’ kiasi cha kuhamishia mkataba kwa kampuni hiyo (kutoka Richmond) bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.
Kulingana na vyanzo mbalimbali, ICC ilikubaliana na hoja kuwa Bw. Aziz alikuwa na ‘nguvu’ nyingi na ushawishi mkubwa hadi kubadili mkataba kwenda kwa ‘rafiki yake na yeye mwenyewe’ kupitia kwa mdai (Dowans) na kumlainisha Waziri wa Nishati na Madini ili amlazimishe mwakilishi wa TANESCO, Bw. J. C Lottering kusaini mkataba kati yake na Richmond Juni 23, 2006.
Taarifa kutoka ndani ya Kampuni ya Uwakili ya Rex Attoneys iliyowakilisha TANESCO katika shauri hilo, zinasema kuwa ICC ilipokea kiapo cha Bw. Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa NET Group Solutions, kuwa hata kwa kutumia sheria ya kimataifa ya zabuni, ambayo ni ya wazi, isiyo na ufanisi na ndefu, TANESCO ingeweza kuingiza mitambo hiyo, bila matatizo, na kwa kipindi kifupi kuliko miezi 18 iliyodaiwa na Waziri wa Nishati na Madini.
Hata hivyo, vyanzo vyetu vimelieleza gazeti hili kuwa pamoja na TANESCO kushindwa katika shauri hilo, kampuni ya Rex Attoneys imeishauri serikali kupinga hukumu hiyo katika mahakama za Tanzania kwa hoja kwamba suala la muda wa kuingiza mitambo na uhalali wa mkataba husika ni kinyume cha sera ya serikali na maslahi ya umma, mambo ambayo hata hivyo hayaelezwi katika vifungu vya sheria.
Katika ushauri wa kampuni hiyo kwa TANESCO ambayo gazeti hili limeona, wanasheria wa Rex Attoneys wameshauri kuwa hatua hiyo inawezekana kutokana na mazingira yafuatayo:
“Kwa kuwa ICC iliridhika na ushahidi wa Bw. Lottering aliyedai kutishiwa ‘jambo baya’ endapo asingesaini mkataba kati ya Richmond na TANESCO, na kuwa Bw. Rostam Aziz alitumia nguvu na ushawishi kuhamisha mkataba bila kufuata sheria.
“Lakini mtazamo huo utategemea na utayari wa mahakama za Tanzania kwa kuwa hakuna sheria nchini inayozungumzia sera ya serikali kama hoja za kubatilisha malipo kwa Dowans.
Je Watanzania wenzangu kuna mahali ambapo Kikwete katajwa ndie mmiliki wa Dowans? Slaa amekuwa mwehu baada ya kukosa urais sasa amebaki kila siku Kikwete yupo mdomoni kwake. Wamiliki ndio hao wametajwa hapo juu,amueni wenyewe.
ReplyDeleteslaa siyo mwehu wewe ndo mwehu ambaye unaropoka tu hovyo,jua kwamba slaa huwa haongei kitu bila kuwa na uhakika nacho,kama ni uongo mbona huyo kikwete hajibu chochote kuhusiana na kauli ya slaa?au unaleta ushabiki wa chama,ndo nyinyi wamojawapo mnaosababisha nchi yetu kuendelea kudidimia na mikataba mibovu.
ReplyDeleteKwani kwenye story hii unayocomment wewe Annony January 4, 2011 10:12 PM Slaa katajwa wapi? Na wewe mwehu zaidi.
ReplyDeleteUsitegemee Kikwete atajwe kwa majina.Unapoona Rostam''ana ushawishi kubwa..na hata 'kumalinisha'waziri wa madini na nishati..unadhani huo ushawishi mkubwa anaupata wapi?..Watanzania waamke na kukataaa dhuluma hizi...Ushabiki wa itikadi za kichama hautatusaidia hapa....kumbuka watakaolipa hela hizi ni watz wote bila kujali wanataoka chama gani.Kikwete anaijua Dowans vizuri maana vyombo vya usalama viko chini yake na vinampa taarifa kamili.
ReplyDeleteWewe unayesema Slaa huwa hasemi uongo umesahau madai ya Lori la kura toka Africa Kusini liliojaa kura? Mbona hatujawahi kuliona? Slaa na Chadema wanapaswa kutambua kuwa camapiagns zimeisha wasubiri 2015.
ReplyDeletewatanzania tusiwe watu wa kumlaumu slaa bila kujua nini anaongea, unatakiwa usome na ujue jamaa anasema nini ndio umlaumu, kikwete na rostam lao ni moja, kweni genge la mafisadi ni kina nani, huo ni mchezo wa wajanja kujinufaisha kupitia serikali ya wanyonge na kwa ridhaa ya jk
ReplyDeleteSijui lile gobole langu bado linafanya kazi......
ReplyDeleteHi, wale wenzangu vijana wa zamani tuliopitia Ruvu, Mlale, Mafinga, Makutupora, Oljoro..... hivi kweli mnavumilia ujinga huu? hebu amkeni basi! Watu wanatajwa, na hawajawahi kubisha, halafu sie tunaacha Dowans ilipwe!
kuhusu lori alisikia tetesi kama raia wengine, aliifahamisha polisi kwani kisheria na kiutaratibu ndiyo inayoweza kuthibitisha hilo. Si lazima jina litajwe ndipo ujue dowans ni ya nani. Jiulize, makampuni yote yanajulikana kwa majina ya wamiliki wake, now why not dowans?
ReplyDeleteNdugu watanzania tukubali kutokana na hali iliyopo na inayoendelea ni ngumu. Kukumbatia huu ukumbavu wa Dawans hautusaidii chochote. Rais kashindwa kututetea wananchi wake kaamua kukumbatia ufisadi. Na sisi tumuonyeshe ya kuwa kutokana na ukimya wake hatuwezi kuvumilia. Angekuwa mstari wa mbele kuwa na maamuzi ya kuchukua hatua haya mambo yasinge mkuta. Sasa aamke ashirikiane na wananchi aepukane na hawa mafisadi.
ReplyDeleteAwaambie hawa mafisadi kila mtu achukue msalaba wake. Rais aamue kuchukua msalaba wa watanzania. Ashirikiane na bunge kutekeleza majukumu yake. Haya mambo ya siri siri ndio hayo yanamchafua na kumuumbua. Dr Slaa anauchungu na Tz, ya leo na umasikini, na hali ya mtanzania ilivyo. Anajiuliza ni kwa nini Mtanzania hapigi hatua siku zote ni kudanganywa tu. Hotuba yake ya mwaka mpya hakuweza kulifafanua alipita juujuu tu. Ninawaomba ndugu zangu watanzania hili swala la Dawans si la chama cha CCM,CHADEMA, CUF WALA TLP. Tushirikiane wote tujie serikali yetu inafanya nini katika kumsaidia huyu mtanzania ili aweze kutoka kwenye ulimwengu wa giza na kuingia kwenye ulimwengu wa kisasa. Wanaomlaumu Dr SLAA hao ni watanzania wa IKULU ambao wanamshauri Rais upumbvu ili akae mbali na wananchi wake.
Rostam Aziz alikuwa mweka hazina wa CCM ambayo JK no mwenyekiti wake, Rostam uyo uyo ndo shareholder Vodacom ambapo Ngeleja alikuwa mwanasheria wa Vodacom akaamia Madini na richmond ikapita..get a connection??? bado tu huamini hii ni syndicate???yani Kikwete, Lowassa,Rostam na Chenge??? hawa watu ni balaa!!!
ReplyDeleteRais wetu hahusiki kabisa katika sakata hili, yeye kama mtendaji mkuu wa serikali hupokea mapendekezo toka kwa wasaidizi wake akiwemo waziri mkuu ambe katika sakata hili alikwisha ondoka pamoja na mawaziri husika.Kama angekuwa anahusika asingewaondoa hao kwa ajili ya kulinda nafasi yake maana wangeweza kwenda nao ili kulinda siri.Suala hapa ni vyombo vya dola ambavyo havitekelezi majukumu yake kama habari hii iliondikwa iko wazi je ni kwa nini vyombo vya dola visichukue hatua ya kuwakamata wote na kuwafungulia mashtaka?ushahidi gani ambao unatakiwa?.Waziri wa Nishati kwa nini nae asitoe ukweli wa kampuni hizo na wamiliki wake?Hizi ni zama za utandawazi habari unaweza ficha kesho wikileaks wanatoa ...Takukuru,usalama wa taifa ,polisi ...amkeni katika usingizi mzito kuhusu suala hili.
ReplyDeleteKatika suala hili kwa nini serikali ya Tanzania inaogopa kupeleka hukumu hii mahakama kuu kuendelea na kesi, kwani kwenye mahakama za ushuruhisi mmoja wapo hasipokubali anaruhusiwe kuendelea na kesi kwenye mahakama.Hatuwezi kumtegemea mwasheria mkuu wa serikali kwani mmemsikia kuhusu suala la katiba na jaziba za kijaruo au kikurwa, Jaji Werema hawezi kutwambia tunaongea kama bata wakati sisi tunaona tunaibiwa, na tumekubali kwamba yeye anaongea kama bata kwasababu hajui kabisa suala la Richmond kwani yeye alisoma hukumu tu lakini hakufanya utafiti kujua huu mradi ulianzia wapi. Ndugu msimtaje Dr Slaa mwehu kwani suala hili analijua fika anachoongea anakijua, kwanza hutakiwi kuwa na elimu ya chuo kikuu kumhusisha kikwete na Richmond kwani ili suala lazima lilijadiriwa kwenye baraza la mawaziri, sasa leo rais hawezi kutwambia halijui, analijua fika tunachoomba kikwete twambie nani mmiliki wa kampuni hii.
ReplyDeleteDooh! Takukuru walishamsafisha richmond, na usalama wa taifa wao ni washika kibendera kuangalia nani ataotea katika kufunga goli na polisi kwa utaalamu huu wa sasa wako nyuma sana bado hajaona ndani hadi sasa na magazeti yanaoandika na kutoa ya ndani polisi ndio hustuka ....na hufuatilia kwa kutaka kuzuia sio kuchunguza...Bado tuko nyuma sana itachukua muda kujua na kusahihisha..tusubri.
ReplyDeleteHivi watanzania tutaendelea kuwa wajinga mpaka lini? Kwani hakika zingelikuwa nchi zingine tayari wangeshaanga maandamano kupinga maskini kuchagiwa gharama kubwa za umeme kwa ajili ya kuwalipa Dowans. Ni ukweli usio pingika kwamba Rostam na Kikwete ni kama chanda na pete. Hawa lao ni moja. Haiwezi kutokea hata siku moja Kikwete akaamua jambo kinyume na Rostam kwani dili zao ni moja. Mafisadi wanamtandao ndio waliomfikisha Kikwete hapo alipo. Fedha zao ndizo zilizompeleka ikulu sasa unategemea Kikwete apinga Dowasons wasilipwe? yeye mwenyewe Kikwete ana mkono wa share kwenye Dowasons sasa kweli atapinga Dowasons wasilipwe. Watu wanafikiri Slaa analipuka halipuki hata kidogo. La mhimu badilisheni katiba ili hata kama Rostam, Kikwete na kundi lao la mafisadi wakituhuju mali zetu kwa mgongo wa mkataba wa Dowason siku moja fedha zetu zirudi ninajua tutabadilisha serikali 2015 na hapo ndipo hawa wanaofiri nchi yetu kana kwamba ni yao pekee yao watakapokiona cha moto.
ReplyDeleteChonde chonde Kikwete si ulirudisha fedha zilizoibwa na Kigoma Malima wakati ule hata Baba wa Taifa akakupa credit sasa ni wakati wa kuonyesha kwamba Nyerere hakukosea kukupa credit ila kama umeingia kwenye genge la mafisadi tutakuona siku moja ukiingia jela. Ibeni sana lakini ipo siku yenu tu. Ukweli ni kwamba Dowason ina mkono wa Kikwete na Rostam. Hatuutaki ufisadi huu wa wazi wazi wa kudhurumu mali ya watanzania.
Yatupasa watanzania tuungane tuache itikadi kwani hata wale wa CCM fedha anazopata Rostam na Kikwete wao hawataambulia hata shiling moja wao na watoto wao walia na kusaga meno kupitia ongezeko la bill za umeme. Acheni itikadi tuokoe nchi kwenye mikono ya mafisadi maana hawana huruma mafisadi. CUF, CCM, Chadema na wale wote walio wazalendo unganeni kupinga ufisadi wa Rostam na Kikwete na wanamtandao wenzao
Ni aibu rais kuhusishwa na kashfa yoyote kama hii. Mnaomtetea mna lenu. Mtu mzima hawezi kujitetea? Rais ndiye mtu pekee Tanzania mwenye uwezo wa kutoa majibu sahihi. Tunamfadhili ili atupatie majibu. Tumempa majeshi na watumishi wema, kwa nini hataki kuwatumia kumpa majibu yanayoulizwa na wananchi?
ReplyDeleteWatanzania tunakwenda wapi?
Sio swala la uchaguzi kwisha hapa, tunataka mali zetu zitunzwe. Hatutaki watu wagawane mali zetu?
Hakuna kitu kinacho kera kama maslahi. Maasiikini TZ ni kwa nini hakuna mchana wala jioni kila siku ni alfajiri, asubuhi, haya mtongotongo yatakwesha lini? Na familia ijue baba au mama kaenda kazini? Watoto wanajiuliza ikifika tarehe 10 hata nauli hakuna huyu baba au mama anakwenda kazini au kuzurura mjini. Dr Slaa uzi huo huo usichoke kututoa haya matongotongo baba mpaka kielelweke. Wanaosema umechanganikiwa ndio wao wamechanganiwa. Bado wapo kwenye kipindi cha Mrema na NCCR, HAPA HABADILIKI MTU MSIMAMO MMOJA TU. Hapa Rais ajue kuwa kuna watanzania wa Ikulu na wauraiani. Ngoma nzito.
ReplyDeletewale wanao mtetea Raisi hapa, ndo walewale wanao danganywa kwa Kofia na Tishet za njano na kijani. na washangaa hata hawaogopi kutetea huu upumbavu. Mungu wangu jamani pana laana Gani Tanzania??.
ReplyDeleteSielewi kazi ya Rais Kikwete ni nini. Hivi tuna haja na mtu wa namna hii aendelee kuongoza Taifa hili? Kwa hakika ameshindwa kazi, na taasisi pekee inayoweza kumwondoa madarakani kwa haraka kabla hajaipeleka hii nchi kwenye uharibifu ni jeshi la wananchi.Kwa nini hatuna kina Jery Rowlings wa Ghana huko. Hivi jeshi wanafanya nini hadi sasa au hawana uchungu na hii nchi?. Hivi Rostam Azizi ni rais wa nchi gaani na kwa nini hakamatwi pamoja na hayo yote?
ReplyDelete(Sijui lile gobole langu bado linafanya kazi......
ReplyDeleteHi, wale wenzangu vijana wa zamani tuliopitia Ruvu, Mlale, Mafinga, Makutupora, Oljoro..... hivi kweli mnavumilia ujinga huu? hebu amkeni basi! Watu wanatajwa, na hawajawahi kubisha, halafu sie tunaacha Dowans ilipwe!)
Huyu mtoa maoni ninamuunga mkono, Tulisota mwaka mzima na wala hatuja fanya mazoezi siku nyingi. Tuanzie kwa walimu wetu.
Rais hawezi kuongea wakati bado anachakachua barabara ya serengeti pia. Mie sijui mnalalamika nini badala ya kuonyesha kwa vitendo. Watanzania jirani zangu, mimi ni mkenya lakini rais wenu hafai, kazi yake ni kula upepo tu Bilila lodge kempinsik, huko serengeti. nyie mnapiga makelele huko wenzenu wanatanua. Msije shangaa kuambiwa yeye anamkono katika hoteli hiyo ya kifahari ndo maana hata anachochochea kujengwa barabara huko serengeti. Hata hilo sakata la dowans anahusika. kimefika kipindi waafrika tuongee kwa sauti moja kuwafilisi viongozi mafisadi na wale wanaokumbatia mafisadi.
ReplyDeleteHadi wakati huu,JK haamini kama yuko Ikulu na pengine hajui nini kinaendelea ndio maana majibu ya watu wake hayapati majibu na hivyo kuhusishwa moja kwa moja na maovu yote yanayoendelea hadi sasa,nawashauri watanzania majibu tunayo wenyewe na tutayapata mara tutakapokomaa vilivyo kudai katiba mpya iliyoandaliwa na kuridhiwa na watanzania wote sio kamati ya kikwete ambayo itakuwa tayari kufanya kazi kumfurahisha yeye na hao watu wake wanaohusishwa na ufisadi.Tumempata rais kivuli anayeumizwa na umasikini uliopo ndani ya watanzania tena kwa kusababishwa na wachache waliojipendelea kwa kutumia madaraka yao,ofisi zao na kuchota fedha za wananchi bila hofu huku mwenye dhamana na mamlaka ya kudhibiti hayo akiwa kimya bila kuchukua hatua.Ni kweli kuwa mtuhumiwa wa ufisadi kwa mujibu wa vyanzo vya habari hawezi kukwepa na watanzania wanapawsa kujua hivyo kwa vile hajakanusha na kuwaambia watanzania nani mmiliki kama siyo yeye JK na wenzake,ninamuomba rais wetu kivuli Dk.Slaa mwenye uchungu na nchi hii aendelee kuwaelimisha watu juu ya yanyoendelea, muda mfupi ujao watamuelewa na kukubaliana na yote anayoyasema.Wanaomtetea JK ungewajua pengine ufahamu wao ni mdogo na kwakweli ndio hasa serikali anayoiongoza ingependa kuwaona watanzania wote wakiwa hivyo,yaani wajinga wasiojua haki zao,wajibu wao kwa Taifa na wajibu wa kiongozi kwao.
ReplyDeleteNI AJABU SANA KWA TANZANIA KUONGOZWA NA VIPOFU NA WEZI. RAIS KIKWETE NI KIPOFU NA MWIZI. AMEIBA KURA ZA KUMWEKA MADARAKANI, ANALIIBIA TAIFA NA WATU WAKE KWA KULIPA DOWANS AMBAYO NI MALI YAKE NA ROSTAM AZIZ, ANACHOTAKIWA NI KUNGOLEWA MADARAKANI TUU. JESHI LETU TUKUFU LA WANANCHI HAMYAONI HAYA MAOVU? HAKUNA TAASISI YEYOTE ITAKAYOWEZA KUMWONDOA HUYU KWA HARAKA NA KWA AIBU, NA HAWA KINA ROSTAM KAMA SIYO MASHUJAA WETU JESHI LA WANANCHI. WAJIBU WENU NI KULINDA MIPAKA YETU, KATIBA YETU NA SASA WAJIBU WENU MPYA NI KUOKOA HII NCHI NA HUYU ADUI MWOVU KIKWETE. NASIKIA TANESCO WAMESHAANZA KULIPA HIZO PESA KWA KULAZIMISHWA YA KIKWETA. NAJIULIZA HIVI KIKWETE KAKOSA NINI, AU NI ILI KUMFURAHISHA ROSTAM AZIZ, LOWASA NA GENGE LAKE OVU LA WEZI?
ReplyDeleteBob Marley aliimba na wimbo wake kweli unadhihirisha, "we are mental slaves". Let us stand firm and emancipate ourselves from this mental slavely. Akili tunayo, nguvu tunazo na utashi tunao, why not organise ourselves to fight these thieves out of the regime and drive them to prison. Tunagonja nini watanzania wenzangu wakati nchi inaporwa na tunazidi kuwa masikini. Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO naye ni fisadi mkubwa maana amehusika na wizi mkubwa na ufisadi wakati wa ujenzi wa minara ya mawasiliano ya iliyokuwa Celtel(sasa Airtel), Vodacom na tiGO. Hizi kampuni zililipa Contractor kufanya kazi hii ya kupeleka umeme kwenye minara yao ya mawasiliano lakini huyu Contractor hakutumia hata Senti moja kulipa TANESCO ili umeme upelekwe kwenye minara ya mawasiliano badala yake walilipwa mafisadi wa TANESCO pesa kidogo akiwemo William Mhando na wakaiidhinisha laini za umeme na kupelekwa kwenye minara TANZANIA yote.Si Ajabu serikali kumpa ukubwa maana wanajua ni rahisi kukamilisha mambo yao kama unavyoona sasa kuhusu haya malipo kwamba TANESCO tayari imeshaanza kutenga pesa za malipo. Halafu hawa PCCB sijui wanafanya nini maana wamepewa taarifa nyingi za ufisadi TANESCO na viongozi walio madarakani lakini cha ajabu mpaka leo hakuna wanachofanya, PCCB nao ni mafisadi na nasikia ukiwapelekea jambo la kuchunguza, inakuwa umewapelekea mlo wa kujishisha maana watapata hongo ya kutosha kutoka kwa wanayemchunguza.
ReplyDeletekwani hoja hapa ni nini? "NANI MMILIKI WA RICHMOND",jibuni hoja nyie wehu kama slaa. Au labda mwandishi kakosea awaombe radhi?
ReplyDeleteNashukuru kwa comment zote za wasomaji. Sasa mimi natoa mpango kazi na sio kulalama tu.
ReplyDeleteJumatatu ya tarehe 10 Jan., ntakuwa na mkutano na waandishi wa habari kulieleza taifa nia ya kuandamana nchi nzima kupinga ufisadi huu uliokithiri (Dowans, Richmond, EPA, Kagoda, Meremeta, Kiwira, TICS, Air Tanzania n.k.) maana sisi watanzania tumeonyesha udhaifu mkubwa mno wa kushughulikia/ kutatua masuala ya kitaifa. Tumeweka mbele itikadi zetu za kisiasa. Halafu tumekuwa tukisahau mambo kadhaa makubwa yanayofunikwa na mengine.(Vitambulisho vya kitaifa, shirika la reli, Mikataba mibovu ya madini, uwajibikaji serikalini n.k.tumeyaweka kapuni??). Mabadiliko yeyote katika jamii, huhitaji wachache kuumia au kupoteza maisha yao. Mimi ninajitolea na ntakuwa "Nyerere au Mandela" wa Tanzania ijayo. Naomba ushirikiano wako katika kila hatua ntakayoipiga. Jibu ni kumuondoa Kikwete na serikali yake ktk madaraka. Haiwezekani jambo ambalo halina kichwa wala miguu linaongelewa kwa muda sasa, Rais umenyamaza tu na badala yake unaomba wananchi tukubaliane na bei za umeme uliopanda. Stupid!! Chenge amepanda kiburi hadi anajiita yeye ni Rais wa Afrika! Waziri wa madini anaulizwa ataje wamiliki wa Dowans, anajibu kwa kiburi Nenda BRELA kaulize?? Naibu wake anasema yeye halijui sakata zima, eeeh!! Idiot!! Kwa taarifa tu, ufisadi mwingine unanukia katika mradi wa kufua umeme mkoani Singida ambao serikali itamiliki 51% na mwekezaji 49%. Naibu waziri anaulizwa usambazaji nchi nzima utakuwaje, anasema itategemea uwezo wa mwekezaji?? Huu ni ujinga wa hali ya juu na ni ufisadi mwingine kwa nchi yetu. Serikali itamiliki 51% na mwekezaji 49%, sasa nani mwenye nguvu hapo?? Kama Kiwira serikali haikuwa na umiliki wowote, bado ililipa mishahara ya wafanyakazi wa mgodi wa kiwira itakuwa huu mradi ambao inamiliki sehemu kubwa?? Acha utoto Nyalandu!! Udodoki huu utaisha lini. La kiwira, waziri mkuu, Pinda akasema bungeni kuwa atamshauri Rais ili waurudishe mradi huo serikalini; hiyo ndiyo dawa ya tatizo hilo?? Sasa mie nataka vitendo na sio comments tu maana hata wananchi wa vijijini wenye hali ngumu hawazisomi. Tukifanya maandamano na mabadiliko watayasikia na watakuwa nasi. Pili, Mnaotoa comment, huu sio muda wa kuongelea itikadi zenu za kisiasa!! Hakuna Kikwete au Slaa hapa. Ni mali ya wananchi wa kitanzania!! Period!! Mabadiliko ni sasa, amka ndugu yangu mtanzania, Usidanganyike!!.
Nashukuru kwa comment zote za wasomaji. Sasa mimi natoa mpango kazi na sio kulalama tu.
ReplyDeleteJumatatu ya tarehe 10 Jan., ntakuwa na mkutano na waandishi wa habari kulieleza taifa nia ya kuandamana nchi nzima kupinga ufisadi huu uliokithiri (Dowans, Richmond, EPA, Kagoda, Meremeta, Kiwira, TICS, Air Tanzania n.k.) maana sisi watanzania tumeonyesha udhaifu mkubwa mno wa kushughulikia/ kutatua masuala ya kitaifa. Tumeweka mbele itikadi zetu za kisiasa. Halafu tumekuwa tukisahau mambo kadhaa makubwa yanayofunikwa na mengine.(Vitambulisho vya kitaifa, shirika la reli, Mikataba mibovu ya madini, uwajibikaji serikalini n.k.tumeyaweka kapuni??). Mabadiliko yeyote katika jamii, huhitaji wachache kuumia au kupoteza maisha yao. Mimi ninajitolea na ntakuwa "Nyerere au Mandela" wa Tanzania ijayo. Naomba ushirikiano wako katika kila hatua ntakayoipiga. Jibu ni kumuondoa Kikwete na serikali yake ktk madaraka. Haiwezekani jambo ambalo halina kichwa wala miguu linaongelewa kwa muda sasa, Rais umenyamaza tu na badala yake unaomba wananchi tukubaliane na bei za umeme uliopanda. Stupid!! Chenge amepanda kiburi hadi anajiita yeye ni Rais wa Afrika! Waziri wa madini anaulizwa ataje wamiliki wa Dowans, anajibu kwa kiburi Nenda BRELA kaulize?? Naibu wake anasema yeye halijui sakata zima, eeeh!! Idiot!! Kwa taarifa tu, ufisadi mwingine unanukia katika mradi wa kufua umeme mkoani Singida ambao serikali itamiliki 51% na mwekezaji 49%. Naibu waziri anaulizwa usambazaji nchi nzima utakuwaje, anasema itategemea uwezo wa mwekezaji?? Huu ni ujinga wa hali ya juu na ni ufisadi mwingine kwa nchi yetu. Serikali itamiliki 51% na mwekezaji 49%, sasa nani mwenye nguvu hapo?? Kama Kiwira serikali haikuwa na umiliki wowote, bado ililipa mishahara ya wafanyakazi wa mgodi wa kiwira itakuwa huu mradi ambao inamiliki sehemu kubwa?? Acha utoto Nyalandu!! Udodoki huu utaisha lini. La kiwira, waziri mkuu, Pinda akasema bungeni kuwa atamshauri Rais ili waurudishe mradi huo serikalini; hiyo ndiyo dawa ya tatizo hilo?? Sasa mie nataka vitendo na sio comments tu maana hata wananchi wa vijijini wenye hali ngumu hawazisomi. Tukifanya maandamano na mabadiliko watayasikia na watakuwa nasi. Pili, Mnaotoa comment, huu sio muda wa kuongelea itikadi zenu za kisiasa!! Hakuna Kikwete au Slaa hapa. Ni mali ya wananchi wa kitanzania!! Period!! Mabadiliko ni sasa, amka ndugu yangu mtanzania.
Hivi kwanini jina la kikwete likitajwa kwenye tuhuma zozote watu wanakuwa wakali sana?,Dr Slaa alitaja orodha ya mafisadi pale mwembe yanga temeke huyo kikwete yumo,na walitishia kwenda mahakamani nani kaenda mpaka leo?,hawa jamaa wafuatao ni hatari sana ktk nchi yetu Kikwete,Lowasa,Rostam(huyu ndiyo mwizi namba moja hata KAKODA NI YAKE)
ReplyDeleteTUACHE USHABIKI WA KISIASA mtu kama mwizi ni mwizi tuu na aitwe hivyo mwiziiii,ukiwaliza Dowans ni nani hawasemi ni ,ukisema ya kikwete watu midomo juu ,tuambiane ya nani basi? FUKKY SEEK!
Mandela wala Nyerere hawakuwa anonymous katika jambo lolote lenye maslahi ya taifa na dunia kwa ujumla,ungeanza kumuondoa madarakani Mkapa kwanza aliyemuachia Kikwete zahma hizo ulizozitaja hapo juu,Kikwete ataondoka madarakani 2010 baada ya muda wake kumalizika
ReplyDeleteKosa kubwa walilofanya ccm ni kuchuka hela ya kampeni kwa kina R/A sasa wenyewe wanataka hela zao,watazirudishaji wasipowekeza katika mikataba hewa?
ReplyDeleteWatanzania tuamke saa ya ukombozi ni sasa. Tusipoamka sasa haw a mafisadi wataendelea kututesa. Hii hoja hapo juu ya Gazeti hili zuri Yatosha kabisa kumfunga paka kengele. Rostam huyo katajwa mchana kweupe. Lazima ajutie kwa nini amekuwa mvurugaji wa Amani ya nchi yetu.
ReplyDeleteAcheni hizo kumlaumu Kikwete, huo sio UTANZANIA bali ni kuendekeza sera za chama, tuliyasikia mengi wakati Mwinyi na Mkapa wapo madarakani, tunachotaka ni ushahidi, posting hii habari kwa wikileaks mtapata majibu, eti Slaa ana uchungu wa nchi, kakwambia nani, kama aliweza kupora mke wamtu tu je ataweza kuachia nchi yetu? huyo ndio hafai kabisa, sisi tunajua nini kipo nyuma ya Slaa lakini tunaangalia hii digmatism itaishia wapi.
ReplyDeleteWewe unayetaka kuambiwa mitambo ya nani hujasoma hapo juu wamiliki ni nani? pengine ukishasoma haikai akilini kutokana na ushabiki wako, lipo jina la Kikwete? leo ukiambiwa Kikwete ni baba yako utaamini? si utataka atoe ushahidi wa kuthibitisha kama wewe ni mwanae? Tunachosema waliovurunda na mikataba mibovu mmewaacha mmemkazania Kikwete tu
ReplyDeletenyie wote mnaomtuhumu kikwete ni njaa zenu ndo zina wasumbua, hamna lolote la kufanya sasa mnataka kuchafua nchi hii, pumbavu zenu kafieni mbele, nimewatukana kwa kuwa na nyie mmemtukana Raisi wa wananchi, eti kipfu na mwizi, mwizi mwenyewe na kipofu ni wewe na sliaa wako na chadema kwa ujumla, shenzi.
ReplyDeleteJibu la yote tunayotendewa ni kuandamana......
ReplyDeleteNa maandamano yenyewe tuseme kikwete hatumtaki hajiuzulu...
Nani mpka ajiuzulu ndio maandamano yaishe..
Unachekesha Kikwete kachaguliwa na Watanzania kwa asilimia 65% (sitini na tano) na huyo mbwa wenu kachaguliwa kwa asimia 25% na hiyo hoja ya kusema kaibiwa kura tuliitegemea maana toka tunaanza tumeanza uchaguzi wa vyama vingi Mrema,Lipumba,Mtikila,Mbowe na sasa Slaa hakuna aliyekubali kushindwa kila mmoja amesema ameshinda lakini kaibiwa kura hivyo hilo si geni,jaribuni muone kama tutakubali Kikwete aachie ngazi kwa ajili ya maandamano yenu. UPOFU HUO RAIS KISHAPATIKANA TENA KWA ASILIMIA KUBWA USILINGANISHE NA IVORY COAST AU KENYA AMBAPO ASILIMIA NDOGO SANA IMETEMBEA
ReplyDeleteWewe Anony mwehu nini? Ati tuandamane hatumtaki Kikwete! Kakwambia naaaaani kama Kiwete hatumtaki. Sisi ndio wenye nchi hii na wewe na genge lako la kihuni tunawasubiri muingie barabarani. Gobore langu linawasubiri!!!
ReplyDeleteTumejiwekea sheria na kanuni tokea Mwalimu , AH, Mkapa na hakusubutu mdudu kuinua kidore. Au unatumiliwa wewe kuvunja amani hapa Bongo. Mark my words, man..! Tunakujua, tunakufaatilia na tunaku-time halafu tutajua nini tutakufanya!!!
Huoni? Ni Kikwete pekee baada ya baba wa taifa ndie alietupa fursa kurekebisha katiba, nini tena unataka?
Lete fikra za kimaendeleo na zinazodumisha amani sio ulete fujo hapa!!! Shit!
Yeyote anayesema Kikwete hafai basi akatafute mwanamme amsugue!! Alah! Iwapo raisi kachaguliwa na watu wake, nyinyi wengine musopendezewa ni kuwa hata ateremshwe Mungu hapa mutamkataa. Na huyo Slaa wenu si atatuchukulia wake zetu na wabinti wetu huyu?? Si bora mafisadi wale hela kuliko kula mabinti zetu na wake zetu.
ReplyDeleteHuu ni ushenzi wa mwisho mtu kuchukua mke wa watu. Tukimweka serikalini huyu atakushana wanapenda ushenzi watuharibie jamii. Watu Kama Slaa watupwe bahari zenye mapapa waone kibko yao! Sasa vipi utamfananiza na Kiwete mtu huyu - Kwa rangi ya ngozi yake au luga tu?
ANAETAFUTA MWANAUME WA KUSUGUA NI WEWE AMBAE UNA HAMU. BONGO KUNA VIDUME TANGAZA BIASHARA YAKO.
ReplyDeleteKikatiba Rais kishapatikana hao wehu wana ndoto za mchana. Bongo gani unaitaja wewe uliyekuja na matongo ukafundishwa kuchamba? si ndio nyie mnakojoa kwenye chupa za uhai kisha mnatupa barabarani? mnanuka hata tukipanda daladala tabu,Hii DARISALAMA haikuwa hivyo kabla washenzi nyie hamjaingia humo
ReplyDeletekama kikwete akitaka kuoa,atapata wake wengi kweli du!,hivi inakuwaje mwanaume mzima unatoa pumzi zako zote na nguvu kumtetea mwanaume mwenzio ilihali naye anamdomo inatia shaka tuambiane jamani,unafika kuona mwengine mbwa ila mwingine anafaa kuitwa binadamu!,kweli bongo tambalale ,tujenge hoja tuache matusi na kauli zisizokuwa na tija kwenye mjadala,kama kweli unaakili jenga hoja kutukana ni dalili ya kuishiwa kufirisika kabisaaa,hayo mliendika hapo juu yanatija gani kwa watanzania!?
ReplyDeleteNdugu yangu hiyo ndio taarifa iliyoweza kujibu comment zote hapo juu na sijui anamaanisha nini au umeelewa nini. Lakini ndio akili za kilevi sio kosa lake. Waandishi wa gazeti la majira muwe wavumilivu kuna kisirani kinataka kutunyima uhuru kwenye hii page. Cha ajabu hata Dar es salaam imemshinda kuandika.
ReplyDeleteKama unatangaza na unataka kujua ni bongo ipi nenda VIP utachagua unavyotaka.
ReplyDeletejamani, akili ndogo tu inasema: kama wakubwa wakishindwa kuwaajibisha wadogo waliokosea, na wakaenda mbali zaidi hata kukaa kimya tu au kuwatetea wakosaji, basi tafsiri ya tendo hilo ni moja kati ha hizi tatu:
ReplyDelete1. wakubwa wametuma wadogo watende makosa hayo kwa manufaa binafsi,
2. wakubwa sio viongozi safi na makini; au
3. wakubwa hao wanawaogopa wadogo wanaokosa.
Hayo yote ni aibu na udhaifu mkubwa kwa viongozi. kwa swala la richmond, wakubwa wote wa serikali na ccm party hawawezi kukosa lawama. napendekeza mali zao ziuzwe zifidie hasara kubwa wanayotupa sisi walipa kodi na wananchi. halafu hawana hata moral authority ya kusimama hadharani kujitetea!!