* Sasa atamani kumwona
LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo anadaiwa kuwa na hofu dhidi ya mwanamke aliyezaa naye mtoto, ambaye amejulikana kwa mara ya
kwanza kuwa, ni mwanafunzi mrembo wa kingereza.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 25, wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka jana, aliishitua dunia baada ya kuelezwa kuwa baba, lakini bila ya kutajwa mama wa mtoto huyo.
Wakati huo alisema kuwa, mtoto wake atalelewa chini ya uangalizi usiokuwa wa kawaida na baadaye ilielezwa kuwa, amemnunua mtoto kwa kumtuliza mama yake kwa mkataba wa kutoa pauni milioni 10, ambazo kwa fedha za Tanzania, ni zaidi ya sh.bilioni 22.
Lakini, chanzo kimesema kuwa, mwanamke huyo hataki kumwacha mtoto huyo ambaye alipatikana baada ya kukutana na nyota huyo siku moja kwenye klabu ya usiku.
Mwanamke huyo amekuwa akimpigia simu Ronaldo akimweleza kuwa, amebadili mawazo na kwamba, anataka kurudisha fedha zake.
Mwanamke huyo amekuwa na msongo wa mawazo kufuatia uamuzi wake wa kukubali kulipwa fedha.
Moja ya kipengele katika mkataba huo ulioandaliwa na wanasheria wa Ronaldo, kinataka asijadili jambo hilo na mtu yeyote, ikiwemo familia na rafiki zake.
Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo kwa sasa amekuwa na uchungu kwa kumkosa mtoto na haoni kama fedha alizopewa zimemletea furaha.
"Mara kwa mara amekuwa akimpigia simu usiku wa manane. Amekuwa akimlilia na kumwomba akubali kumwona mtoto," chanzo kilicho karibu na mwanamke huyo kililiambia gazeti la Sunday Mirror.
"Kulikuwa na makubaliano ya kutowasiliana naye, lakini hata hivyo imekuwa tofauti.
"Humpigia simu baada ya mechi kumpongeza kwa jinsi alivyocheza, akitumaini kuwa, kuna siku anaweza kuwa karibu naye.
"Anahisi kama ameuza nafsi yake. Amekuwa na maisha ya kimilionea, lakini hawezi kuwaambia rafiki zake na familia yake ukweli kuhusu ni kitu gani kilitokea na hilo linamfanya ajisikie mpweke."
Rafiki wa Ronaldo, ambaye alihamia Real Madrid kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya pauni milioni 80 mwaka 2009, alisema: " Kwa jinsi ilivyokuwa, ni chaguo lake, maamuzi yake."
Ronaldo aliwahi kumwelezea mwanamke huyo aliyezaa naye kuwa, ni mwanamke aliyekaa naye siku moja wakiwa watupu hotelini na kufurahia penzi.
Baada ya kujua kuwa ni mjamzito, aliwasiliana naye kupitia wakala wake, Jorge Mendes.
Baada ya kuzaliwa na kupimwa vinasaba ili kujua kama ni mtoto wake wa damu kweli, wakati akiwa katika michuano ya Kombe la Dunia akiichezea Ureno nchini Afrika Kusini, ilitangazwa katika Facebook Julai 3, kuwa, amekuwa baba.
Mtoto huyo alionekana kwa mara ya kwanza hadharani katika mechi ya Real Madrid Desemba 8, akiwa na umri wa miezi sita.
Alikuwa amebebwa na mama yake Ronaldo Dolores mwenye miaka 55, ambaye amekuwa akimlea mtoto huyo pamoja na dada za Ronaldo, Elma na Liliana Catia.
Rafiki huyo aliongeza: "Kwa kiasi fulani mama wa mtoto ameweza kuwasiliana naye na kutaka kumwona mtoto.
"Atamwambia kuhusu maisha ya umilionea aliyonayo sasa, pamoja na safari nyingi za kwenda katika klabu za usiku London.
Rafiki zake wanachukulia kuwa, alishinda bahati nasibu, na mwenyewe amekuwa akijifanyisha hivyo.
Lakini, amekuja kugundua kuwa, hana nafasi ya kumwona mtoto wake ambaye anakua. Kama wataendelea kuzungumza kama hivi, anaweza kujikuta akizidi kuumia zaidi na zaidi.'
Ronaldo akiwa na Manchester United, alitwaa nayo ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya na alipigia kura kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA 2008.
Ronaldo akiwa katika msimu wake wa pili Real, sasa amekuwa juu kwenye orodha ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga, akichuana na Lionel Messi.
kumbe tamaa ya pesa sio sisi waafrika tu ! haya dada ndio ushafanya biashara mtoto huyo na unachotaka ni kuwa nae ronaldo ili umchune zaidi kwa kuwa huko kwenu ulaya baba itabidi akupe nyumba na kumtunza mtoto ambapo kwa mtu kama huyo ataambiwa akupe pesa ya mtoto sio chini ya paundi 3000 kwa mwezi ! lakini jua hao wabrazili ni kama waafrika ....wajanja .dada umetoka kapa hapo
ReplyDeleteRonaldo si Mbrazil, ni Mreno jifunze utafiti
ReplyDeleteHuyu dada ameanza kuishiwa na pesa kwa maisha ya anasa aliyonayo, keshapiga hesabu kuwa kama Ronaldo atakubali basi ataishi nae kwa mwezi na na baada atampeleka mahakamani na kuanza kulipwa kila kitu, hii ikiwa pamoja na 20% ya kipato cha Ronaldo mpaka mtoto atimize miaka 18 - 20, hebu piga hesabu wewe mwenyewe atapata kiasi gani, hana usongo wa mawazo ni muongo ila hawa jamaa hasa wanawake wa ulaya na Marekani wao pesa mbele, huko ukioa bora uwe unapata income suport hapo utaishi na mkeo mpaka kufa, lakini ukiwa na kipato kidogo tu, jua huna mke na mtoto, sheria zinashinikiza miiddle Class kuishi bila mahusiano na kugombana kwa kuweka sheria kuwa mwanamke ndio mwamuzi katika nyumba. ndio maana siku hizi hakuna ndoa na wanaozaa kwa wingi ni wale wasiofanya kazi au mke na mume wote wanakipato cha juu. usioe au kuishi na mwanamke asiesoma au kufanya kazi utajuta, Ronaldo alilijua hilo mapema, ndio maana alimpa 10m na akahama Uingereza. Lakini Rafiki yangu Thiery Henry wa arsenal yalimkuta, salama yake naye alikimbia Uingereza, wee shauri yako kukimbilia wanawake wa kizungu au Waingereza utajuta kuringa.
ReplyDelete