11 October 2013

SUMAYE 'AWALIPUA' UPINZANI



 Na Andrew Ignas
  Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, amesema baadhi ya wabunge wa upinzani, wameugeuza ukumbi wa Bunge kama sehemu ya malumbano, matusi badala ya kujenga hoja ambazo zitachochea maendeleo kwa wananchi.

Bw. Sumaye aliyasema hayo Dar es Salaam juzi katika mahojiano maalumu na Majira juu ya maoni yake kuhusu madai ya upinzani wanaotaka Rais Jakaya Kikwete asisaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013.
Alisema upo umuhimu wa wabunge hao kutii kanuni za Bunge ambalo ni chombo kinachoheshimika badala ya wabunge hao kupotosha maana nzima ya Bunge kwa ajili ya malumbano.
" Vyama vya upinzani vinashindwa kutumia fursa walizonazo ndani ya Bunge ili kujenga hoja ambazo zitachochea maendeleo ya wananchi badala yake ni watu wa kupinga na kukashifu hoja zenye tija kwa jamii," alisema Bw. Sumaye.
Akizungumzia suala zima la tozo ya laini kila mwezi, Bw. Sumaye aliitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kupunguza makali ya maisha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wakati huo huo, Bw. Sumaye amelaani vikali hatua ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, kutaka Rais apunguziwe madaraka ya kuteua viongozi.
  "Rais anastahili kubaki na mamlaka hayo kwa kuteua baadhi ya viongozi kama Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri, Gavana wa Benki Kuu, Jaji Mkuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wengineo," alisema Bw. Sumaye.

6 comments:

  1. Wasivyo na busara wanaweza kukashifu hata ushauri huu kwa nguvu zote.

    Wajenge hpja za msingi sio kupotosha wananchi na kudakia kila hoja ili kujijengea umaarufu.

    Tunapenda upinzani wenye nguvu lakini sio upinzani maarufu

    ReplyDelete
    Replies
    1. NDG YNG MAONI YAKO HEBU CHUKUA HIYO SENTENSI YAKO YA KWANZA NA UIELEKEZE KWAKO.UNAUJUA MCHAKATO WOTE KUELEKEA RASIMU YA KATIBA?WW AMBAYE SIO MPINZANI KWA SASA TWAMBIE MCHAKATO WA KATIBA UPO SAWA NA UNAPITIA NJIA ZIPI?KUPATA MUSWADA WA SASA KUELEKEA KTK MABARAZA USHIRIKISWAJI UKOJE?JE NI WA KISHERIA AU HISANI.USIKURUPUKE ANGALIA NA WW UNAWEZA KUWA MPINZANI! NAUKAITWA HUNA BUSARA.

      Delete
    2. Rafiki usija ukafikiri kwamba hatujui mambo. Tunaandika tu kwa kifupi kuwazindua watu. Tunaelewa michakato yate ya constituional amendments ya marekani, Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine zilizoendelea.
      Kinachofanyika sasa hivi ni busara ya kitanzania kuepusha shari kwa njia ya mazungumzo na muafaka. Waswahili wanasema mheshimu kichaa asije akakuaibisha.
      flexibility iliyopo ni kuepusha migogoro isiyo na tija. Na hiyo ndiyo hulka na utamaduni wa nchi yetu.
      Mabadiliko ya sera ya vyama vingi hayakutokana na maoni ya wengi bali busara na hekima na utashi wa Watanzania.
      Mabadiliko ya katiba pia yatafuata utashi huo huo.
      Jufunze ndugu kuwa maraisi wetu wote waastaafu na mawaziri wao wanaishi ndani ya nchi. Wanashiriki shughuli zote za kijamii kama kawaida. Hakuna mkimbizi. Hii inatokana tu na misingi ya haki tulijijengea kama Watanzania.

      Tuendelee kukwepa miatafaruku isiyo na tija. na ndio mkondo huo raisi wetu anaotaka kuuchua sio kwamba anawaogopa wapinzani sana lakini analinda "political culture" ya watanzania

      Delete
  2. INGEKUWA VIZURI IWAPO WAJUMBE WA TUME YA KATIBA WANGEKARIBISHWA IKULU NI VEMA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI WAJIPANGE WAELEZE HIYO RASIMU IMEPUNGUA NINI KIASI KUIFANYA ISISAINIWE NA RAIS IKUMBUMBUKWE MAWAZO YALIYOPEVUKA NI YALE YATAKAYOKIDHI MATAKWA YA KIZAZI CHA KESHO NA KESHO KUTWA IWAPO MAONI YATALENGA KUWAJENGEA MAZINGIRA YA KUINGIA IKULU TU HUO NI UBINAFSI ULIOKIDHIRI

    ReplyDelete
  3. Na kama wataingizwa ikulu na katiba basi hawatatoka! Itakula kwenu mnaowashabikia

    ReplyDelete
  4. Best unajisikiaje ukitabiri watu kutusiana, kufarakana na kuuana alafu lisitokee badala yake vicheko na raha tupu. Baada ya hapo uanze kulalamika kuwa upande wako umerubuniwa.

    Siasa mchezo mchafu. Chukua tahadhari!

    ReplyDelete