Na Fatuma Rashid
Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limewasilisha rasmi suala la madai ya
aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya klabu hiyo katika Kamati ya
Hadhi ya Wachezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Boniface Wambura alisema FIFA imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake
hiyo, baada ya kupokea vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za
Marekani pamoja na vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote
alizokuwa akiidai klabu hiyo.
Wambura alisema kwa taratibu za FIFA, hivi
sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka pande hizo mbili na badala yake,
Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger, kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na
kuziarifu pande husika. Zwanziger kitaaluma ni mwanasheria.
Aliongeza kuwa Papic, aliyeinoa Yanga kwa
vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko yake FIFA akidai hadi mkataba
wake unamalizika klabu hiyo, ilikuwa haijamlipa dola 10,000 za Marekani.
Katika sakata hilo, uongozi wa Yanga uliwahi kuulizwa
kuhusu madai hayo ambapo walisema hadai chochote, huku wakiongeza kwamba kocha
huyo alikuwa analipwa kila baada ya miezi mitatu na walionesha hati zote za
malipo waliyokuwa wakimlipa
No comments:
Post a Comment