- AMTAKA MAGUFULI,WADAU KUFIKIA MWAFAKA
- ARUDISHA MSAMAHA WA ASILIMIA TANO MIZANI
Na Darlin Said
Waziri Mkuu , Bw. Mizengo Pinda ,
amesitisha utekelezwaji wa agizo la Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli la
kuondoa msamaha wa tozo kwa uzito wa magari uliozidi ndani ya asilimia tano ya
uzito unaokubalika kisheria.
Bw. Pinda alitoa uamuzi huo Dar es Salaam jana siku moja baada ya
Chama cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA), kutangaza uamuzi wa kupaki magari yao wakipinga agizo hilo.
TATOA pamoja na Chama wa Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani
(TABOA), walipinga agizo la Dkt. Magufuli kutaka magari yanayobeba uzito wa
tani tatu na nusu na kuendelea, kupimwa mizani bila msamaha wa tozo uliozidi
ndani ya asilimia tano ya uzito uliokubaliwa kisheria.
Alisema kutokana na sakata hilo,
amelazimika kuunda kamati ambayo itakutana na wadau TATOA na TABOA ili kupata
ufumbuzi wa mgogoro uliojitokeza.
"Kwa kuwa bado kuna mgogoro kati ya Wizara ya Ujenzi,
Wasafirishaji wa malori na mabasi kuhusu utekelezwaji wa kanuni 7(3), ambao
wanasema haitekelezeki kirahisi, naiagiza Wizara ikutane na wadau. "Wakae
na kujadili namna bora ya kutekeleza kanuni hii, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, waunde timu ya wataalamu ambao watakutana na
wawakilishi wachache wa TATOA na TABOA ili wapitie kanuni hizi kwa lengo la
kupata mwafaka," alisema Bw. Pinda.
Aliongeza kuwa, mwezi mmoja unatosha kwa Wizara na wadau hao,
kukamilisha kazi hiyo na utaratibu uliokuwepo awali kabla ya tangazo la
Serikali uendelee kutumika.
Aliitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kupanga utaratibu
mzuri wa kupima magari hayo katika mizani ili kuondoa msongamano katika kituo
kimoja.
"Wakati umefika kwa Wizara husika kukagua mizani na kuangalia
ubora wake kwani hicho ndio chanzo kikuu cha mgogoro uliopo... baadhi ya
watumishi katika mizani si waaminifu, wanapokea rushwa hivyo Wizara iangalie
namna ya kutatua tatizo hili," alisema.
Akizungumzia barua
iliyoandikwa mwaka 2006 na Waziri wa Miundombinu (wakati huo), Bw. Basil
Mramba. Barua hiyo ilitoa nafuu ya punguzo la asilimia tano ya uzito wa 'Axel'
za magari utakaosomwa kwenye mizani ili kufidia kasoro za mizani kutopima kwa
usahihi uzito wa magari.
Alisema
msamaha huo ulikuwa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani, sura ya 168, toleo
la 2002 na kanuni zake za mwaka 2001 za Usalama Barabarani juu ya ukomo wa
uzito wa magari.
"Ingawa Bw. Mramba alifanya hivyo kwa
nia njema, wasafirishaji wakatumia fursa hiyo vibaya kwa kuongeza mizigo kwenye
magari yao kwa
sababu kuna msamaha wa asilimia tano," alisema.
Bw. Pinda alisema, kutokana na hali hiyo Dkt.
Magufuli aliamua kufuta muongozo wa barua hiyo na kujielekeza katika sheria na
kanuni za Usalama Barabarani za mwaka 2001.
Sheria hiyo inasema uzito uliozidi lakini upo
ndani ya asilimia tano ya uzito unakubalika kisheria, magari hayo yanapaswa
kupunguza mzigo, kupanga mzigo na ikishindikana watatakiwa kulipia uzito mara
nne ya tozo ya kawaida.
Awali Bw. Pinda
alisema, Serikali haitaruhusu malori na mabasi kuzidisha mizigo kama nafuu wanayoitafuta kwani barabara zilizopo zina
uwezo wa kudumu miaka 20 kwa magari yaliyobeba uzito unaokubalika kisheria. mzia
mgogoro huo, Bw. Pinda alisema chanzo chake ni baada ya Dkt. Magufuli kufuta
No comments:
Post a Comment