Na Fatuma Rashid
Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zilizochezwa mwishoni mwa wiki
iliyopita jijini Dar es Salaam, timu za Yanga na Simba zimeingiza jumla ya sh.
milioni 182.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Boniface Wambura alisema Yanga katika mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting
iliyochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000.
Wambura alisema katika mechi hiyo, jumla ya
watazamaji 16,492 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh.
22,630,921.58.Alisema viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000, na Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 14,369,796.61.
Alisema katika mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,507,248.26, tiketi sh.
3,117,215, gharama za mechi sh. 6,904,348.96."Kamati ya Ligi sh. 6,904,348.96, Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,452,174.48 na pia Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 2,685,024.59," alisema.
Wambura alisema katika mechi ya Simba na JKT
Ruvu iliyochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 87,901,000,
ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.Aliema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo walikuwa 15,780 na viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000,
sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
21,051,025.92 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
13,408,627.12.
"Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 10,703,911.48, tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi
sh. 6,422,346.89, Kamati ya Ligi sh. 6,422,346.89."Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 3,211,173.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,248,789.67 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,248,789.67,"
alisema.
Wakati huo huo, Wambura alisema mechi ya
ligi hiyo kati ya Mbeya
City na Coastal Union,
iliyochezwa Jumamosi Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 16,959,000
huku kila klabu ikipata sh. 4,035,229.
Alisema
mgawo wa mechi hiyo ulipelekwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
2,586,966, uwanja sh. 2,051,811.57, tiketi sh. 696,290, gharama za mechi sh.
1,231,086, Kamati ya Ligi sh. 1,231,086, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 615,543, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mbeya (MREFA) sh. 478,756
No comments:
Post a Comment