Na Jane
Edward, Arusha
Kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge
wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), imefutwa kwenye Mahakama ya
Hakimu Mkazi jijini humo
Uamuzi wa
kuifuta kesi hiyo ulitolewa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Bi. Devotha
Msofe, baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Elianenyi Njiro, kuieleza
mahakama hiyo kuwa hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Bw. Njiro
alisema; "Mheshimiwa Hakimu, hatuna nia ya kuendelea na kesi hii hivyo
tunaiondoa mahakamani kwa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai kama kilivyorekebishwa mwaka 2002,"
alisema.
Hakimu Msofe
aliridhia uamuzi huo na kumuachia huru Bw.Lema chini ya kifungu hicho cha
Sheria ya Makosa ya Jinai.Wakili wa
pande zote waliridhika na uamuzi huo wa mahakama kumuachia huru Bw. Lema ambaye
alikuwa nje kwa dhamana.
Akizungumza na
Majira nje ya mahakama , Bw. Lema alisema alikuwa akijua kesi hiyo ya
kutengenezwa ndiyo maana mashahidi walikuwa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu
wa Polisi Wilaya.Alisema kwa kuwa kesi hiyo
imefutwa kwa kifungu kidogo cha sheria, hataogopa kusema ukweli na kuachiwa
kwake kutamfanya ashirikiane na wapigakura kuharakisha maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment