Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imebaini ufisadi mkubwa baada
kupitia vitabu vya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kwa
mwaka 2011/2012 zinazoonesha sh. milioni 13.8, zililipwa mishahara kwa
watumishi hewa, anaripoti Anneth Kagenda.
Pia kamati hiyo imebaini halmashauri hiyo
inadaiwa sh. milioni 138.3 na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za
Mitaa (LAPF).Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajab Mbarouk Mohamed, aliyasema hayo
wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hiyo, Dar es Salaam jana na
kusisitiza kuwa, hali katika halmashauri ya Urambo si nzuri kwani fedha
zimeliwa kwa kiwango cha juu.
Alisema kamati yake pia imebaini sh. milioni
287 ambazo ni madai ya walimu na zaidi ya sh. bilioni moja ambazo zilitakiwa
kupelekwa katika Mfuko wa Wanawake, Vijana na vijiji tangu kipindi hicho
hazijapelekwa.
Aliongeza kuwa, halmashauri hiyo ina miradi
26, ambayo kati ya hiyo, 11 ina dosari mbalimbali ambazo ni pamoja na kukosekana
kwa stakabadhi zinazothibitisha mapokezi ya fedha husika.
“Tunaiagiza halmashauri hii pamoja na mambo mengine, iwachukulie hatua
wote waliohusika na ufisadi wa fedha za mishahara hewa na kuhakikisha fedha
zote ambazo hazijapelekwa kwenye mifuko husika, zinapelekwa haraka
iwezekanavyo,” alisema
No comments:
Post a Comment