. Na Amina Athumani
WAGOMBEA wawili wa nafasi ya urais na
Kamati ya Utendaji walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamewekewa pingamizi kuwania nafasi hizo katika
uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27, mwaka huu.
Akizungumza Dar
es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema waliopingwa ni
Wallace Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus Lufano anayewania
ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili, ambayo ni Mikoa ya Mara
na Mwanza.
Alisema aliyempinga Karia ni Shamsi
Kazumari wa Dar es Salaam, wakati Lufano anapingwa wa Samwel Nyalla wa Mwanza.Wambura alisema pamoja na mambo
mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba na Azam TV wakati akijua
kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu kisheria kusaini mkataba huo.
Alisema naye Nyalla, ambaye pia ni
mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe kupitia Kanda hiyo anampinga,
Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
Wambura alisema
Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Hamidu Mbezeleni itakutana
leo saa 4 asubuhi kusikiliza pingamizi hizo ambapo wawekaji pingamizi na
waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe ndani ya muda kwa vile uwakilishi
hautakiwi
No comments:
Post a Comment