Na Rehema Mohamed
CHAMA Cha Wananchi
(CUF) kinasikitishwa na tukio la kuchomwa moto kwa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, jijini Dar es
Salaam.Pia chama hicho
kimelitaka Jeshi la Polisi na mamlaka za usalama wa taifa kupambana na matukio
hayo. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi Agosti 24, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa katika vyombo vya habari Dar es Salaam jana,imeeleza kuwa
haiwezekani taifa linakumbwa na matukio ya kushambuliwa nyumba za ibada na
hatua thabiti za vyombo vya dola hazionekani.
Ilieleza kuwa raia
wanaofanya vitendo vya namna hiyo wamo miongoni mwetu na wasiolitakia mema
taifa hivyo ni wajibu wa vyombo vya dola kubaini matukio hayo kama yanafanywa
na mtu mmoja mmoja, vikundi vidogo au ni mitandao mibaya yenye lengo la kujenga
chuki na uhasama baina ya Watanzania wenye dini na madhehebu mbalimbali.
Ilieleza kuwa, kama
uhalifu huu unafanywa na mitandao, vyombo vya dola vinawajibika kujua mwanzo na
mwisho wa mitandao hiyo, wafadhili wake na malengo yao."Pamoja na
vyombo vya dola kuliita tukio hili kuwa ni 'jaribio la kihalifu,' CUF inaona
kuwa huu ni mwendelezo wa mashambulizi dhidi ya nyumba za ibada na hujuma dhidi
ya raia wasio na hatia na Jeshi la Polisi liwatafute wahusika kokote waliko na
kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake," ilieleza.
Ilibainisha kuwa, CUF inaungana na Watanzania
wote wenye mapenzi mema na nchi yao na wanaopinga vitendo vinavyoweza
kuhatarisha amani ya nchi kulaani vikali tukio hilo
No comments:
Post a Comment