Na Mwandishi Wetu
KATIKA kile kinachoonekana kusogeza huduma bora zaidi kwa wananchi
na kutambuaumuhimu wa afya zao, Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) kupitia vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt imezindua
kampenimaalumu iitwayo ‘Nyumbani Ni Nyumbani’
kwa ajili ya kupeleka bidhaa hizo zisizo na kilevi kwa Watanzania wote. Akizindua
kampeni jijini Dar esSalaam jana,
Meneja Bidhaa zisizo
na vileo wa TBL, Consolata Adam alisema, wamezindua kampeni hiyo maalumu ili
kuhakikisha vinywaji visivyo na kilevi vinamfi kia kila mtu. "Tumeamua kuzindua
kampeni hii ili kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa vinywaji vya
Grandmalt na Vitamalt katika matumizi ya kutunza na kulinda afya
zao.
"Kampeni hii itahusisha mabalozi wa Grand Malt na Vita Malt kwa pamoja
kutembea nyumba kwa nyumba na kuhakikisha ujumbe huu unamfi
kia kila mtu katika nyumba yake ambapo pia kutakuwa na fursa ya kujishindia na
kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa kampeni
hiyo," alisema. Consolata alisema, vinywaji hivyo ni vizuri zaidi kwa afya
ya mwanadamu kwani vimetengenezwa vikiwa na virutubisho
vya kila aina na vinafaa mno hata kwa mama mjamzito.
" Tu n a omb a Wa t a
n z a n i a wasishangae pale watakapokutana na watu wetu ambao watakuwa wanawatembelea
majumbani kwao, kwani lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya
kutambua faida za kutumia
kinywaji cha Grand Malt na Vita Malt
katika kulinda afya yake ili tuweze kujenga desturi ya kuwa na matumizi bora
kwa ajili ya kujenga afya zetu, alisema.
Naye Ofi sa
Uhusiano wa TBL,Doris Malulu alisema hii ni kampeni ya kwanza kuzinduliwa na vinywaji
hivyo kwa lengo moja la kuwawezesha Watanzania kutumia bidhaa
hizo zenye faida kubwa kwa mwili wa mwanadamu. "Tunataka vinywaji hivi vipatikane
kila mahali na pia kuwasaidia Watanzania umuhimu wa
kuvitumia kwani vina faida kubwa kwa wote, kuanzia hata kwa mtoto,"
alisema Doris. Kampeni hiyo ya Nyumbanini
Nyumbani inatarajiwa kuanza katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,
Arusha, Kilimanjaro, Mtwa r a , Do d oma , I r i n g a ,Morogoro, Mbeya na
Shinyangaambapo itaanzia mji wa Kahama.Vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi vinazalishwa na kusambazwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment