Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi, amekiri ndani ya Jeshi la Polisi kuna askari ‘feki’ aliowapa
jina la “Makanjanja”, kama ilivyo katika sekta nyingine ingawa Serikali
haipendezwi na hali hiyo.Dkt. Nchimbi
aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu tume iliyoundwa na jeshi hilo kuchunguza matukio yaliyolalamikiwa dhidi
ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro pamoja na
Kigoma.
Alisema
kutokana na hali hiyo, wataanza kufuatilia kwa kina askari waliostaafu au
kufariki ili kujiridhisha kama walirudisha sare walizokuwa wakizitumia wakiwa
kazini.Aliongeza kuwa,
vitambaa vya sare za polisi vinapatikana katika maduka mbalimbali hivyo mtu
yeyote anaweza kununua, kushona na kuweka nembo za polisi hivyo ni vigumu
kudhibiti hali hiyo.“Ndani ya Jeshi
la Polisi kuna askari makanjanja (Feki), kama ilivyo kwa sekta nyingine, hakuna
mtu anayependa wawepo, hivi sasa askari ambao watapatikana na makosa ya
uhalifu, viongozi wanaohusika kuwasimamia watashushwa vyeo na wahusika
watafukuzwa kazi,” alisema Dkt. Nchimbi.
Alisema
ameipitia ripoti ya tume ambayo imewasilishwa kwake na kufuata ushauri
uliotolewa wa kuwachukuliwa hatua askari waliohusika na matukio mbalimbali kwa
kuwafukuza kazi na wengine kuvuliwa madaraka.Dkt. Nchimbi alisema askari saba
wamefukuzwa kazi kwa sababu ya kujihusisha na matukio ya uhalifu ambao wengine
walikamatwa na bangi mkoani Kilimanjaro, fuvu la kichwa cha Binadamu (Morogoro)
na kusababisha mauaji ya wafanyabiashara Mjini Kasulu, mkoani Kigoma.
“Tukio la askari polisi wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU), mkoani Arusha Ex F.1734 CPL Edward na G. 2434PC George
wa Kituo cha Polisi Ngarananyuki, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, walifukuzwa
kazi baada ya kukiri kosa la kusafirisha bangi kwa kutumia gari la polisi,”
alisema.Aliongeza kuwa, gari la polisi PT 2025,
aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa likisafirisha bangi yenye uzito wa
kilogramu 540, yenye thamani ya sh. milioni 81 ambalo lilikamatwa mkoani
Kilimanjaro, Mkuu wa Kikosi Mrakibu wa Polisi Ramadhani Giro, amevuliwa
madaraka aliyokuwa nayo.
“Mrakibu Giro alishindwa kusimamia
maofisa walio chini yake, askari mwingine Inspekta Isaack Manoni, amesimamishwa
kazi na kuagiza ashtakiwe kijeshi akidaiwa kumtorosha mtuhumiwa hatari Ex
F.1734 CPL Edward, aliyekuwa dereva wa gari la polisi ambalo lilikamatwa na
bangi, Kilimanjaro,” alisema.Alisema askari wengine wawili, Inspekta
Salimu Juma Kingu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na Inspekta Mikidadi
Galilima, wote wamepewa onyo kali katika utendaji kazi.
Dkt. Nchimbi aliongeza kuwa, askari
mwingine ASP Francis Duma PF.15828, aliyekuwa kiongozi wa kukamata gari ambalo
lilibeba bangi, amepandishwa cheo kuwa Mrakibu wa Polisi.Alisema Inspekta Jamal Ramadhani na
Inspekta Juma Mpamba ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Upelelezi, Wilaya ya Mvomero,
mkoani Morogoro, wamevuliwa madaraka kwa kuonesha udhaifu katika utendaji kazi
kwa kutowasimamia kikamilifu askari walio chini yao baada ya kukamatwa na fuvu
la kichwa cha binadamu.
Hata hivyo, Dkt.
Nchimbi alisema Mkuu wa Kituo cha Upelelezi Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma,
ASP Bendarugaho, amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini kwenye kusimamia
upelelezi wa jalada la kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Sigwavumba ambapo
upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke
sasa kama walinda usalama wako hivi, nadhani iko haja ya kufanya utafiti wa kina ili kubaini ni kitu gani kinawafanya walinzi hawa wa amani hasa siku hizi wanafanya vitendo hivi. Ni je wanatumwa na wakubwa wao au wanajituma wao wenyewe. Bila ya kufanya utafiti wa kina na kujua chanzo cha kufanya hivyo wananchi watakosa kabisa imani na vyombo hivyo ambapo vituklo kama hivyo vikizidi kuendelea kila kukicha.
ReplyDelete