MKAZI wa Kimara, Dar es Salaam, Bw.
James Hussein Hassan (45), jana amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala
akikabiliwa na mashtaka mawili, anaripoti Rachel Balama.Mashtaka hayo ni kujifanya askari wa
Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na kukamatwa na sare za Jeshi la Polisi.
Ilidaiwa na wakili wa Serikali, Bw.
Nasor Katuga mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Minde kuwa,
Agosti 14 mwaka huu, eneo la Kinyerezi Mnara wa Voda, mshtakiwa alifanya
udanganyifu wa kujitambulisha kwa Inspekta Gabriel Chiguma kuwa yeye ni askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Katika shitaka la pili, inadaiwa Agosti
14 mwaka huu, eneo la Kinyerezi Mnara wa Voda, mshtakiwa alikamatwa na sare za
polisi ambazo ni kofia, mkanda, jaketi pamoja na nembo ambavyo vyote ni mali ya
jeshi hilo.
Mshtakiwa alikana mashtaka na kurudishwa rumande baada ya
kukosa wadhamini. Alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye makazi ya kudumu
ambao watasaini hundi ya sh. milioni saba kila mmoja. Kesi hiyo iliahirishwa
hadi Septemba 5 mwaka huu
No comments:
Post a Comment